Tusiwavuruge Viongozi wa CHADEMA kwenye maamuzi Muhimu kuhusu Arumeru Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusiwavuruge Viongozi wa CHADEMA kwenye maamuzi Muhimu kuhusu Arumeru Mashariki

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Imnyagi, Jan 21, 2012.

 1. I

  Imnyagi Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Moja ya sifa kubwa ya chama chochcote makini cha siasa ni uwezo wake katika kufanya maamuzi sahihi kama ambavyo chama hiki kimekuwa kikifanya kwa nyakati zote.

  Kumekuwa na suala la kifo cha mbunge ambaye haijalishi alishindaje inagawa kuna tetesi nyingi kwa vijana wa Arumeru ambao walipigia CDM. Lakini Nasari hakushinda kama walivyotegemea kwa madai kuwa inaaminika kuwa kijana huyo aliuza timu kama ilivyo kwa baadhi ya wanasiasa wenye tamaa ya Fedha na kukosa uadilifu na wengine walisema dogo aliitwa na wazee wakamwambia ampishe mkubwa ili akipata wizara fulani amkumbuke dogo katika ufalme wake na pia maendeleo yatakuja jimboni kama sumari atakuwa waziri na kama ataendelea kushindana na mkubwa huyo wao wana mbinu nyingi ya kuweza kulichukua jimbo hilo na hivyo ni bora akamate mshiko aendelee na masomo haya siyo maneno yangu ni ya baadhi ya vijana ambao ni wapiga kura wa jimbo hilo.

  Kuna mambo kadhaa nataka tuangalie kabla ya kumpitisha Nasari kwenye keybord bila kusubiri Busara na hekima za viongozi makini wa CDM. Kufanya maamuzi sahihi ya mtu atakayepeprusha bendera ya chama.

  CDM. Wanaandamwa na shutuma za ukabila, udini na ukanda kulingana na mawazo ya wasiopenda chma hiki hivyo tusitoe mwanya wowote wa kuwapa magamba upenyo wowote ule.

  Kumtea mtu kama Nasari ambaye alishakuwa mgombea ambaye kushindwa kwake kuna kasoro nyingi ikiwemo mwenzake alikuwa mgonjwa lakini bado akapita kuna hatari ya kulipoteza tena jimbo hilo.

  Kumteua Nasari wakati alishawahi kuwa mgombea tayari kutakuwa na madhaifu mengi ambayo ccm walishayaona na wakayatumia kumshinda hata sasa wanaweza kuyatumia na kumsambaratisha kabisa na CDM. Jimboni humo.

  Sina uhakika sana uwezo wake Binafsi yeye Nasari kama ni yeye tu ndiye mwenye mvuto na haiba ya kupeperusha Bendera ya CDM. Jimboni pale au aling'arishwa na chama chenyewe kama ilivyokuwa kwa madiwani waliofukuzwa. Hapa nazungumzia Quality ya mgombea na Quality ya chama pia.

  Ni vizuri kama tungeacha siasa za kishabiki makundi na ukabila katika kukishauri chama kuhusu mgombea bora kama kilivyofanya huko Igunga kikaleta matokeo mazuri kabisa na ule nauona kuwa ulikuwa ushindi.

  Viongozi wa Chama wapewe nafasi na suport kutoka kwa wanachama ili apatikane mgombea makini wa kuleta ushindi jimboni pale tuweke hisia zetu pembeni kwanza maana tunaweza kuwachanganya viongozi wetu wakatupatia Sauli badala Daudi halafu tukajuta baadaye hivyo tusiwavuruge viongozi wetu kwa hisia zetu kali na kuwachugulia mgombea kwenye keybord tuwape nafasi ya kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya chama na masilahi ya Taifa na siyo tuwashinikize kwa ushabiki zaidi pasipo kuchambua mambo kiundani.

  Zaidi sana tumalize kwanza msiba wa mzee Sumari itakuwa ni busara na adabu zaidi badala ya kuanza kupiga kampeni chafu za kichinichini tusiwe kama watoto ambao wanagombea urithi wakati baba hata hajazikwa bado.
  Nina imani kubwa na CDM.kwa uwezo wake na uzoefu wake kitatumia busara zaidi kuliko kufuata ushabiki,mashikinikizo na kampeni chafu za kichinichini.

  Mungu Ibariki CHADEMA.

  Mungu Ibariki Tanzania.
   
Loading...