Tusisikitike sana kwa kukosa tuvipendavyo maishani.

Mkwaruzo

JF-Expert Member
Feb 21, 2011
563
98
Kupenda ni jambo muhimu
katika maisha ya
mwanadamu, kwa sababu
asilimia kubwa ya matendo
ya mtu huongozwa na
mapenzi. Miongoni mwetu kuna watu wanapenda
waume/wake zao, mali,
watoto, magari vyakula,
vinywaji, michezo na pengine aina fulani ya maisha. Baadhi yetu tuko tayari kupoteza maisha kama tutaachwa na wapenzi au kukosa mambo tuliyoyapenda.

Pamoja na kwamba moyo
hupata maumivu pale mazuri yanapokosekana, bado kuna ukweli juu ya madhara ya kujitakia yanayoweza kuepukwa na mtu anayeumia kwa kiwango cha kukosa usinginzi, kulia mara kwa mara kiasi cha kushindwa
kufanya kazi zake kama kawaida. Kupenda kwa kiwango cha kushindwa kujizuia na kuvumilia ni hatari kwa afya ya mwanadamu, kwani uchunguzi unaonesha kuwa
watu wengi wanaosumbuliwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, moyo na wale wenye magonjwa yasiyoonekana kitalaamu pamoja na wanaokufa ghafla ni athari za msongo wa mawazo utokanao na kukosa mazuri wanayohitaji katika maisha yao.(Jiulize ni kipi kinachokutia simanzi moyoni mwako).
Kisaikolojia kuutesa moyo kwa sababu mpenzi wako kakukataa ni matokeo ya kufikiri vibaya kwani ushahidi uliopo miongoni mwetu unaonesha kuwa mapenzi si kitu cha kudumu kwa miaka mingi na anayesema anaweza
kupenda jambo moja milele
kwa kiwango kilekile ni mtu
anayejiwekea mtengo
utakaomnasa mwenyewe na kumtesa. Watu wengi tunaowaona
wakipagawa baada ya
kupewa talaka na waume
zao au kuondolewa mambo
fulani waliyokuwa
wanayapenda ni wale walioyachukulia mapenzi
kama kitu cha kudumu
kisichoweza kubadilika, huku
wakisahau ukweli kuwa
wanayopenda kwa wakati
huo hawakuzaliwa nayo na wala hawakuyapenda kabla.
Licha ya kuwepo kwa
umuhimu wa kujiaminisha katika kupenda kwa msingi wa muda mrefu, mtu hatakiwi kukataa mabadiliko yanapotokea kwani ni wazi kwamba tuliyopenda tulipokuwa watoto si yale tunayopenda sasa.
Hivyo ni jukumu la kila mtu
anayetaka kuwa salama na
maumivu ya moyo ya kumkosa ampendaye ni kuwa tayari kubadilika kutoka kupenda kitu cha awali mpaka kijacho, kuliko
kung’ang’ania wazo moja na kujitesa nalo.

Historia ya mafanikio ya watu inaonesha kuwa waliokuwa tayari kuacha walivyovipenda na kuanza mambo mapya ndiyo waliofanikiwa. Mafanikio na
usalama wa maisha unataka
mtu awe jasiri wa kupokea
changamoto zinazohusu
mapenzi. Ikiwa umekaa na mwanaume kwa muda mrefu na ukabaini kuwa hana mtazamo wa kimaendeleo, uwe tayari
kukubali mabadiko ya kumwacha na kuanza maisha mapya. Rafiki yangu, unaumia kwa sababu mpenzi wako ameamua kuachana na wewe na sasa unafikiria kujiua, hebu kaa chini ufikirie kabla ya kuwa na huyo maisha yalikuwa hayaendi? Kama sivyo kinachokuumiza hasa ni nini mpaka unashinda unalia na kuutesa moyo wako? Tambua kuwa dunia ina vitu vingi sana vya kupenda, ambavyo vimeumbwa kwa ajili ya mwanadamu, usipopenda hiki haina maana hakuna cha kukufaa kipo na asipokupenda ndugu yako wapo marafiki watakaochukua nafasi ya mapenzi moyoni mwako na maisha yatasonga mbele kwa mafanikio makubwa, unachotakiwa ni kujiamini.
Nafuatisha samahani kutokana na urefu wa topic.
 
Back
Top Bottom