singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
KATIKA siku za karibuni, kumekuwa na taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari kuhusu mradi wa bomba la mafuta kutoka Tanga kwenda Hoima nchini Uganda.
Gharama za mradi huo zinakadiriwa kuwa kiasi cha zaidi ya shilingi trilioni 10 za Tanzania; huku kukiwa na ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja takribani 20,000.
Kwa wafuatiliaji wa vyombo vya habari, ni wazi watakuwa wameona dalili za ushindani mkali kati ya Tanzania na Kenya kwenye mradi huo. Awali, Kenya ilikuwa ifanye mradi huo na Uganda kabla ya baadaye Serikali ya Rais Yoweri Museveni kubadili uamuzi wake na kugeukia Tanga – Tanzania.
Tumeanza kuona dalili za upotoshaji wa mradi huo zinazofanywa na wenzetu wa Kenya. Japo hakuna uhakika kama kuna mkono wa serikali ya nchi hiyo au ni watu wa sekta binafsi wanaoona Tanzania itafaidi.
Raia Mwema
Kwa mfano, taasisi moja ijulikanayo kwa jina la Serengeti Watch imetoa taarifa ya kuupinga mradi huo kwa madai kuwa utapita katika Mbuga ya Serengeti na hivyo kuathiri mazingira ya eneo hilo.
Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali imetoa taarifa hiyo huku ikifahamu fika kwamba bomba hilo halitapita katika mbuga hiyo. Njia ambayo inafahamika kwamba bomba hilo litapita ni ile ya Mwanza, Kagera, Singida nk na hakuna mahali ambapo itapita kwenye mbuga hiyo au chini ya Ziwa Victoria.
Wenzetu pia wameamua kufanya propaganda ya kuonyesha kwamba mradi huo ukipitia Tanzania utakuwa aghali zaidi, kwamba Bandari ya Tanga ni ya hadhi ya chini na uongo mwingine chungu nzima.
Rai yetu kwa serikali ni kwamba inatakiwa ipiganie mradi huo kwa njia zote zinazokubalika vitabuni. Kenya ni jirani zetu na wenzetu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na hivyo mradi huu hautakiwi kuwa chanzo cha uhasama wa kudumu.
Uamuzi wa kutumia Bandari ya Tanga ulifanywa na Serikali ya Uganda baada ya kuzingatia ushauri waliopewa na wataalamu wa kigeni. Tanzania haikutumia njia zozote za ulaghai au fitna kupata mradi huu.
Ni wazi kwamba vyombo vyetu vya habari na asasi zisizo za kijamii zinatakiwa sasa kuwa makini na propaganda zinazofanyika kuchafua jina la Tanzania na kutaka kukosesha taifa letu mradi huu.
Hili ni jambo lenye maslahi kwa taifa letu. Kwenye mambo kama haya, tunatakiwa kuweka tofauti zetu za kisiasa, kiitikadi, kidini na kijamii pembeni na kusimama pamoja kuhakikisha tunafaidika. Kwenye hili tunasema; umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu