Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,119
- 24,658
Matokeo ya kidato cha nne 2016 yametoka, tumeona walichofanya hawa vijana!
Kwa miaka ya nyuma ilikuwa ni jambo la kawaida sana kukuta shule za serikali zikiwa zinaongoza kitaifa na hata wanafunzi bora kutoka katika shule za serikali.
Kwa sasa hali imekuwa tofauti, kwa muda wa miaka ya hivi karibuni tunaona ni jinsi gani shule za serikali zinavyozidi kudorora na shule binafsi kuzidi kung'ara kwa kuongoza kitaifa na kutoa wanafunzi bora, huko shule za serikali zikiburuza mkia!
Serikali huku ikiwa imetila suala la elimu bure kwa wanafunzi kwenye shule zao, shule binafsi zimekuwa zikitoza ada kubwa tu na matunda ya hizo ada yanaonekana kwani vijana wengi wanaosoma huko wamekuwa wakifaulu vizuri.
Serikali ina nia nzuri tu kwa kutoa elimu bure kwani lengo lake ni kuhakikisha watoto wote wanapata elimu ya msingi na serikali hadi kidato cha nne!
Lakini ubora wa elimu hii ya bure mbona hauonekani, shule za serikali zinazidi kupotea hata zile kongwe.