Ndala katuacha pointi 11, tarehe 8/3 tunamfunga zinabaki point 8 ambazo ni kama gemu 3.. tatzo lililopo ni je ndala ataweza poteza mechi 3 na si tushinde zote?! Jibu ni Hapana. Pia timu zilizo nyuma ya Ndala zipo vizuri, Mf. Kagera Sugar ambayo imeshinda mfululizo mechi za karibuni hadi kufika no. 3.
Timu yetu imekosa consistency ndo mana leo tunashinda kesho tunadraw keshokutwa tunafungwa. Eeeh Mungu saidia hili pepo linalotukumba hivi sasa, liwavuruge pia na watesi wetu wote ili tusichekane mtaani.
Mkuu ubingwa ndo basi tena na mechi ambazo zimetukosesha ubingwa ni ile ya Mbeya City na ya Stand united. Sare zile za mwanzo mwanzo nazo zimetucost sana.
Mimi kila mara lawama zangu nazipeleka kwa uongozi, walimwacha Kibadeni akasajili kabla timu haijakomaa akaondolewa, Loga naye alivyokuja akaachwa akasajili kabla hata wachezaji hawatumia akaondolewa, Phiri naye alivyokuja akasajili kabla hata hajatumia wale wachezaji akaondolewa, huyu naye amekuja amekuta wachezaji tayari wapo na analalamika timu haikuandaliwa toka mwanzo kucheza ligi kuu hata akifungwa sababu yake ni kwamba timu hakuiandaa toka mwanzo.
Simba kuna tatizo la muunganiko wa timu, ukiangalia mchezaji mmoja mmoja ni wazuri sana lakini tatizo ni muunganiko, angalia toka ligi ianze tumeshatumia wachezaji zaidi ya ishirini, kwa haraka haraka ni Mapunda, Manyika, yule kipa aliyetoka Mtibwa, Wiliam Lucian, Chollo, Kessy, Baba Ubaya, Shabalala, Banda, Owino, Isihaka, Juuko, Mkude, Kwizera, Kiongera, Tambwe, Mkude, Awadhi, Singano, Kiemba, Chanongo, Miraji Adam, Okwi, Sserunkuma wawili, Hajib, Maguli, yule Messi wa Tanga, Seseme, Kisiga hao niliotaja ni 30 na huenda kuna wengine siwakumbuki, sasa ndani ya mechi 15 unatumia wachezaji 30 pengine na zaidi na sababu ya mejeruhi ni kama wanne tu au watano halafu unatarajia timu iwe na muunganiko wa kueleweka kweli?
Na kama hili swala la kukosa posho kama nalo ni la kweli hali itakuwa mbaya zaidi maana jamaa walioko nyuma yetu wengine tumelingana nao pointi na wengine tumewazidi moja hivyo ikitokea watatu au wanne wameshinda na sisi tukatoa draw au kufungwa maana yake tunarudi nafasi ya nane au ya tisa. Bahati mbaya mechi zinazofuata ni za prisoni ambaye anashika mkia na Yanga ambaye anaongoza hivyo zote ni ngumu. Ni ngumu kushuka daraja lakini safari hii kama wachezaji wasipoamua kupigana ndani ya uwanja hali ni mbaya, viongozi ni kama tayari hawana jipya, kilichobaki ni juhudi za makocha pamoja na wachezaji wenyewe.