mzalendoalltz
JF-Expert Member
- Mar 25, 2015
- 828
- 709
Ndugu, wanaJF, kwa heshima na taadhima napenda kuwasalimu sana.
Nimeona hili tulichangie kwa pamoja na naamini serikali inapitia humu. Tunaona serikali yetu ikiwa na nia kabisa ya kurudisha uzalendo uliokuwa umepotea, tena ni uzalendo wa kuichukulia hii nchi kama ni family members.
Tunaona jinsi Rais wetu na Waziri mkuu wakijitahidi sana kuhakikisha viwanda vya ndani vinaendelezwa ili tuinue uchumi wetu kwa kasi ya ajabu, nawapongeza sana na Mungu awabariki.
Tumeachwa sana na wenzetu wa Kenya ,Uganda, Rwanda N.k ila naamini au wanaosema watanzania ni wavivu yawezekana ikawa ni kweli au si kweli? Lakini zaidi sababu yawezekana ikawa ni serikali ilikuwa haiplay part yake ya kuwasaidia watanzania kisha wakakata tamaa(sisemi tuwasaidie kufanya kazi no, bali kila idara au mtu afanye majukumu yake ipasavyo.
Mfano:
KWENYE BIASHARA;
Serikali lazima ihakikishe inawalinda wafanyabishara wake kwa kutumia tools ilizonazo kwa kuhakikisha zile bidhaa zinazozalishwa hapa nchini zinauzwa bei ya chini, kuliko zinazotoka nje ya nchi. Hili litasaidia sana kuongeza mauzo yao kwa wale wawekezaji wa ndani na kuvutia hata wachina' wajapani n.k badala ya kuzalishia Japan na kusababisha gharama kubwa ya kutoa malighafi Tanzania na hatimaye kurudisha bidhaa iliyokwishatengenezwa na kufanya ijapo wao hupewa ruzuku na ili waweze kuuza kwa bei ya chini na kupata demand ya kutosha.
WAZO hapa tuiombe serikali ili kufanikisha hili lazima iwe na timu kazi ya kufuatilia plan au mipango ya viwanda hivi. Kwanini nasema hivi? Mfano serikali inasitisha uagizaji wa sukari kutoka nje ili kukuza viwanda vya ndani lakini cha ajabu ni kuwa viwanda hivyo havina plan endelevu vipo tu so long as mwenye kiwanda anapata benefit hataki kufanya plan endelevu, kwa maana hiyo lazima serikali iangalie plan za kiwanda husika juu ya uzalishaji je wanahitaji mikopo kiasi gani ili waweze kutekeleza hiyo plan na je serikali inaweza kuwadhamini vip ili waweze kufikia kwenye hayo maazimio?
Na je taifa linahitaji tani ngapi na viwanda vya ndani kwa kutimiza hizo plan, je watafeed demand inayohitajika na kwa bei nafuu na je ikibaki tunaweza kuuza nje ya nchi na hatimaye kupata dolla ambazo mwisho wa siku uchumi utakuwa? N.k.
WanaJF kwa kadri uwezavyo ongeza nyama hapa je serikali ifanyeje?
KWENYE KILIMO:
Lazima serikali ijipange kwa vipi? Si ati leo serikali inaamka na kuanza kusema kilimo kwanza bila mipango haaa..... Kumbuka ili kilimo kifanikiwe ni chain ya vitu vingi na serikali hapa lazima ivifanye.
Mosi, lazima serikali iandae plan kwamba,Tunahitaji kilimo gani na kwa matiki gani? Lazima serikali iandae mazingira yafuatayo;
Mfano kama ni kilimo cha pamba, lazima iandae soko, maana yake nn? Ni pamoja na kutafuta au kuandaa uwekezaji wa viwanda vinavyotumia pamba.
2. Lazima serikali iandae maeneo maalum ya kilimo ambayo yanafaa kwa miundo mbinu ya kilimo na kutoa ruzuku ya miundombinu ya umwagiliaji
3. Lazima serikali ipunguze kodi ya zana za kilimo
4. Lazima serikali i hamasishe viwanda vya zana za kilimo
5. Lazima serikali ijenge miundombinu ya umeme na barabara sehemu za mashamba ya kilimo
Na mengine mengi wanaJF..
Kuna mengi ila kwa kuanzia tunaomba tuishauri serikali yetu katika nyanja nyingine kama ELIMU n.k.
Pia unaruhusiwa kuongeza nyama hapo juuu. Tupunguze kulaumu bali tujikite kwenye maendeleo.
Aksante.