Tushiriki kutangaza utalii wetu kimataifa

talentbrain

JF-Expert Member
Oct 5, 2009
1,188
759
Habari za weekend wadau wote na wazalendo wote wa nchi hii. Niwatakie weekend jema.

Nikiwa nimetulia leo nyumbani, nimepitia thread tofauti hapa na kuguswa na jinsi Mungu alivyoijalia nchi yetu na vivutio lukuki tena zaidi ya viwili kwa kila mkoa.

Bahati mbaya ni kwamba si kuwa havifahamiki nje ya nchi tu bali hata kwa watanzania. Baada ya kuguswa na hali hii, na kubaini fursa ya kiuchumi inayoweza kupatikana kwa nchi yetu kama tutavitangaza vivutio vyetu kimataifa nikaona nije na hoja kadhaa na wadau mtaongeza kwa kadri mtavyoona inafaa.

1. Tutumie thread hii kuotodhesha na ni vema tukaweka picha na maelezo ya kujitosheleza kwa vivutio vyetu.

2. Watanzania na hasa wazalendo tukajiunga na forums za kimataifa na kuaza kuvitangaza vivutio tutavyoviorodhesha hapa. Mfano. Wakijitokeza watu 20 wakajiunga na forums kubwa ulimwenguni na kupost post mbili kila siku ni wazi tutafikia malengo.

3. Tuelekezane links za vivutio vyetu na kama hakuna website nzuri za utalii ni fursa sasa kwa wenye interest kwa biashara hii kuzianzisha na watafaidika sana kwakuwa industry hii inakuwa kwa speed sana.

Niwaombe wadau tuchangie mawazo na hata kuweka vivutio hapa na pia mwenye link ya forums au website za kimataifa zenye kuruhusu comments waziweke hapa. Nimepitia website nyingi na kubaini jinsi wenzetu Kenya na Nigeria walivyo aggressive kwenye kuitangaza nchi yao.

Ni muda sasa tuitangaze nchi yetu popote bila aibu. Tukumbuke kuwa neema tunayoitaka tutaipata kama serikali na wananchi watapata kipato.

Wasallam. Weekend njema.
 
Kalambo water falls in Rukwa Region. The second longest water falls in Africa
1460885675224.jpg
 
1460888047101.jpg
1460888086511.jpg
Gombe National Park from the lake view. The park is a home of endangered chimps. It is also a habitat for different types of apes.
The park is situated 16km from Kigoma town along the lake Tanganyika shore.
You can only reach there by boat.
 
Upo sahihi sana mdau juzi kati hapa wadau tulikuwa tunajadili kuhusu saanane island ndio yakaibuka na mengine kama hili la kuutangaza utajiri huu wa vivutio vya utalii hongera kwa kuleta uzi huu.Tatizo linakuja wapi vipo vitengo vimepewa dhamana hii na mishahara wanalipwa je sisi kama wananchi wa kawaida tufanyaje kuwa amsha watu hawa?
 
Back
Top Bottom