Tuseme yatosha sasa kuinufaisha Kenya

Tuseme yatosha sasa kuinufaisha Kenya

mkwapuaji

Member
Joined
Jan 6, 2012
Posts
49
Reaction score
20
Tanzania tuseme yatosha kuburuzwa na Kenya kwa mazao ya kilimo. Tuifanye Tanzania iwe Tanzania kwa sasa.

Hivi tumeacha biashara yetu ikatawaliwa na Kenya kwa makusudi au ni bahati mbaya, hasa ya kupeleka mazao ya kilimo nje ya nchi na bara la Afrika.

Bei za mazao yetu ya kilimo zinapagwa na wakenya huko Kenya na ikiwa hawatakuja kuychukua basi bei hudorora mfano Mbaazi, Mahindi n.k Ukienda Mang'ola kwenye vitunguu ni gari za Kenya utazikuta mpaka unaweza kufikiri upo Kenya yaani mpaka huwa najiuliza tumeiacha nchi yetu holela namna hii...

Kuna haja ya kuchukua hatua za haraka kulizuia hili kwani kila siku mkulima wa Tanzania ataendelea kugandamizwa na mawakala na madalali wa kutokea Kenya

1/ Yafaa sasa tuweke kodi kwenye mazao yetu na bidhaa zetu ziendazo Kenya na nchi jirani. Hii imekuwa ikiwarahisishia wanunuzi wa nje kuja kuchukua mazao kwani yamekuwa yakipatikana kwa bei rahisi na hata wakiyafikisha kwao gharama bado inakuwa ndogo na hivyo kuyauza kwa bei sawa na mazao yao.

2/ Kuanzisha mfumo wa udhibiti holela wa uuzaji mazao kwa wakulima. Nadhani kunapaswa kuwa na chombo kinachowasaidia wakulima wetu kuuza na kupanga bei za mazao yao. Hii itasaidia kuzuia wachuuzi hasa wa nje kwenda moja kwa moja mashambani kumlaghai mkulima.

3/ Kutanua wigo wa masoko kwa mazao ya kilimo ya Tanzania nje ya mipaka yetu. Tumekuwa na utegemezi wa soko moja hasa Kenya kwa mazao yetu. Sasa ni wakati tunapaswa kuwaza nje kabisa ya Afrika Mashariki kibiashara. Kahawa ya Tanzania ipelekwe USA, UK, SAUD ARABIA, GERMANY.... na watanzania sio wakenya. Kahawa ya Tanzania ipewe mlinganyo sahihi na bidhaa za nchi nyingine sio kama bidhaa ya Kenya. Mbaazi za Tanzania zipelekwe India na makampuni ya Tanzania sio kama sasa wanavyoamini kuwa ni bidhaa ya Kenya

4/ ATCL ianzishe ndege za mizigo. Hapa ndio pia wenzetu walipotuacha. Makampuni makubwa ya ndege za mizigo yanatua katika viwanja vya Kenya. Hii imesababisha karibia kila bidhaa muhimu kwa wenzetu basi kuna haja ya kuipeleka Kenya ili iweze kupelekwa nje ya bara Afrika kwa haraka. Rai yangu kwa Mheshimiwa rais afikirie pia kununua ndege za mizigo ili hata kama makampuni ya wenzetu hayapendi kutua kwetu basi tubebe vyetu wenyewe na kuvipeleka.

5/ Watanzania tuache fikra mgando ya kuona kuwa nchi za wenzetu hatuaminiki kama wakenya. Wafanyabiashara wa Tanzania pia wao ndio wamekuwa chanzo cha kuifanya Kenya kutufanyia kila kitu. Leo pesa nyingi za kigeni huingia Kenya kwa bidhaa zinazoenda nje ya nchi hiyo japo zimetoka Tanzania. Uchumi wa nchi yetu umekuwa ukidorora kila wakati huku wanaouua ni watanzania mwenyewe na sio setikali yao kama wanavyodhani.

Ifike wakati Taifa la Tanzania Liishi, liwaze, na liamue kama TANZANIA
 
Mkuu, it's easier said than done, we acha sisi tulime na kuuza mazao yetu mahali tunapoona tunafaidika "willing buyer willing seller"
Sa hvi nipo mto wa mbu naelekea nairobi kupeleka kitunguu ni biashara huru hiyo unasema ya marekani na india ifanye kwanza uone changamoto zake.
 
Tanzania tuseme yatosha kuburuzwa na Kenya kwa mazao ya kilimo. Tuifanye Tanzania iwe Tanzania kwa sasa.

Hivi tumeacha biashara yetu ikatawaliwa na Kenya kwa makusudi au ni bahati mbaya, hasa ya kupeleka mazao ya kilimo nje ya nchi na bara la Afrika.

Bei za mazao yetu ya kilimo zinapagwa na wakenya huko Kenya na ikiwa hawatakuja kuychukua basi bei hudorora mfano Mbaazi, Mahindi n.k Ukienda Mang'ola kwenye vitunguu ni gari za Kenya utazikuta mpaka unaweza kufikiri upo Kenya yaani mpaka huwa najiuliza tumeiacha nchi yetu holela namna hii...

Kuna haja ya kuchukua hatua za haraka kulizuia hili kwani kila siku mkulima wa Tanzania ataendelea kugandamizwa na mawakala na madalali wa kutokea Kenya

1/ Yafaa sasa tuweke kodi kwenye mazao yetu na bidhaa zetu ziendazo Kenya na nchi jirani. Hii imekuwa ikiwarahisishia wanunuzi wa nje kuja kuchukua mazao kwani yamekuwa yakipatikana kwa bei rahisi na hata wakiyafikisha kwao gharama bado inakuwa ndogo na hivyo kuyauza kwa bei sawa na mazao yao.

2/ Kuanzisha mfumo wa udhibiti holela wa uuzaji mazao kwa wakulima. Nadhani kunapaswa kuwa na chombo kinachowasaidia wakulima wetu kuuza na kupanga bei za mazao yao. Hii itasaidia kuzuia wachuuzi hasa wa nje kwenda moja kwa moja mashambani kumlaghai mkulima.

3/ Kutanua wigo wa masoko kwa mazao ya kilimo ya Tanzania nje ya mipaka yetu. Tumekuwa na utegemezi wa soko moja hasa Kenya kwa mazao yetu. Sasa ni wakati tunapaswa kuwaza nje kabisa ya Afrika Mashariki kibiashara. Kahawa ya Tanzania ipelekwe USA, UK, SAUD ARABIA, GERMANY.... na watanzania sio wakenya. Kahawa ya Tanzania ipewe mlinganyo sahihi na bidhaa za nchi nyingine sio kama bidhaa ya Kenya. Mbaazi za Tanzania zipelekwe India na makampuni ya Tanzania sio kama sasa wanavyoamini kuwa ni bidhaa ya Kenya

4/ ATCL ianzishe ndege za mizigo. Hapa ndio pia wenzetu walipotuacha. Makampuni makubwa ya ndege za mizigo yanatua katika viwanja vya Kenya. Hii imesababisha karibia kila bidhaa muhimu kwa wenzetu basi kuna haja ya kuipeleka Kenya ili iweze kupelekwa nje ya bara Afrika kwa haraka. Rai yangu kwa Mheshimiwa rais afikirie pia kununua ndege za mizigo ili hata kama makampuni ya wenzetu hayapendi kutua kwetu basi tubebe vyetu wenyewe na kuvipeleka.

5/ Watanzania tuache fikra mgando ya kuona kuwa nchi za wenzetu hatuaminiki kama wakenya. Wafanyabiashara wa Tanzania pia wao ndio wamekuwa chanzo cha kuifanya Kenya kutufanyia kila kitu. Leo pesa nyingi za kigeni huingia Kenya kwa bidhaa zinazoenda nje ya nchi hiyo japo zimetoka Tanzania. Uchumi wa nchi yetu umekuwa ukidorora kila wakati huku wanaouua ni watanzania mwenyewe na sio setikali yao kama wanavyodhani.

Ifike wakati Taifa la Tanzania Liishi, liwaze, na liamue kama TANZANIA
Kenya hatutaiweza kamwe tz biashara inaendeshwa kisiasa Kenya biashara inaendeshwa na soko
 
Ngoja tukimaliza kununua wapinzani tutalifikiria hilo
 
You are right!

Biashara ni mikakati, biashara ni mipango, lakini biashara ni vita na fitina na ata ujasusi ndani. Angalia nchi za wazungu wanavyotumia mbinu zote hata mauaji na vita ili kufanikisha biashara. Niko Arusha malori ya Kenya hata mabovu yamejaa kubeba mahindi.

Hivi kwa nini watanzania wasipeleke hayo mazao Kenya na kwa nini magari yetu yasitumike ili kuongeza ajira na kipato? Mbona magari yetu yanatumika sana kupeleka bidhaa Kongo, Zambia nk kwa nini Kenya inakuwa hivyo?

Nilisimuliwa jinsi ambavyo watanzania wakipeleka mazao kama machungwa nk wanavyowekewa vikwazo vya makusudi hivyo kushindwa kuuza. Kuna rafiki yangu Rubani aliniambia kuna kipindi kulikuwa na marubani wa kitanzania wengi kiasi Kenya, wakabaguliwa kwa kupewa ndege zilizozeeka zinazokaribia kuisha muda wake wa kuruka na hivyo baada ya muda marubani hao wakakosa kazi.

Najua hii ni mikakati ambayo nchi inaifanya kwa manufaa yake. Lengo langu ni kuonyesha kuwa hata sisi tunaweza kuwa na mikakati yetu ili kuongeza sehemu ya mapato ya biashara hasa mazao na bidhaa zetu.

Lakini kubwa zaidi ni serikali kufanya jitihada za kutafuta masoko na kuwawezesha watanzania kumudu biashara za kimataifa. Mfano inasikitisha kuona wakulima hawana soko la mbaazi, wakati kuna sehemu mbalimbali duniani mbaazi zinahitajika. Serikali inashindwaje hili?
 
Unatoa povu wakati unajua Wakenya ndio wenye bei nzuri.
Kwani wanakuja kuomba
 
Kuongea ni rahisi sana Tanzania bado haijawa tayali na hayo mambo,tumekalia siasa za maji taka na kukomoana hakuna tunaloliwaza zaidi ya kuwamaliza wapinzani,acha tuendelee kuburuzwa na wanaojua nini maana ya kukuza uchumi
 
Namba 3 na 4 ndio suluhisho la maana.
 
Sijui hiyo Tathmini umetoa wapi?Kahawa haiuzwi kenya,kitunguu ya Tanzania huwezi uza ulaya kwa sababu ya standard ya madawa yanayotumika kupiga kwenye kitunguu hivyo huna njia zaidi ya kuuza kenya,Mbaazi sijui ulikuwa unavuta nini?mbaazi inaliwa india na siyo kenya na wanunuzi wakubwa ni pamoja na Mo dewji,mahindi ya Tanzania haitakiwi tena kwa sababu baada ya Tanzania kuzuia ya Zambia iligika kenya na hivyo kuonyesha ina kiwango cha hali ya juu(kwa sababu wanatumia mbegu bora kwa wingi).hiyo akili yako ya kimagu ya kudhani anayenunua mali yako ni adui na siyo mteja mungu akusaidie.
 
You are right!

Biashara ni mikakati, biashara ni mipango, lakini biashara ni vita na fitina na ata ujasusi ndani. Angalia nchi za wazungu wanavyotumia mbinu zote hata mauaji na vita ili kufanikisha biashara. Niko Arusha malori ya Kenya hata mabovu yamejaa kubeba mahindi.

Hivi kwa nini watanzania wasipeleke hayo mazao Kenya na kwa nini magari yetu yasitumike ili kuongeza ajira na kipato? Mbona magari yetu yanatumika sana kupeleka bidhaa Kongo, Zambia nk kwa nini Kenya inakuwa hivyo?

Nilisimuliwa jinsi ambavyo watanzania wakipeleka mazao kama machungwa nk wanavyowekewa vikwazo vya makusudi hivyo kushindwa kuuza. Kuna rafiki yangu Rubani aliniambia kuna kipindi kulikuwa na marubani wa kitanzania wengi kiasi Kenya, wakabaguliwa kwa kupewa ndege zilizozeeka zinazokaribia kuisha muda wake wa kuruka na hivyo baada ya muda marubani hao wakakosa kazi.

Najua hii ni mikakati ambayo nchi inaifanya kwa manufaa yake. Lengo langu ni kuonyesha kuwa hata sisi tunaweza kuwa na mikakati yetu ili kuongeza sehemu ya mapato ya biashara hasa mazao na bidhaa zetu.

Lakini kubwa zaidi ni serikali kufanya jitihada za kutafuta masoko na kuwawezesha watanzania kumudu biashara za kimataifa. Mfano inasikitisha kuona wakulima hawana soko la mbaazi, wakati kuna sehemu mbalimbali duniani mbaazi zinahitajika. Serikali inashindwaje hili?

Hii mambo mnapenda kusema mmesikia kuwa watu wananyanyaswa wakileta bidhaa Kenya mmesikia na nani? Pita pale wakulima market uone jinsi ma lorry yenye usajili wa Tanzania yamejazana yakileta machungwa, enda marikiti upate kuona magari ya Tanzania yamejaa yakimwaga vitungu. Mbona huwa mnapenda kudanganya especially mambo yanayo husu Kenya? Gikomba, the biggest open market in Kenya inatawaliwa na ndugu zenyu wa chagga, wala siku moja hutopata wa kenya wakijadili wawafukuze wa tanzania pale kwa kuwa wanamiliki sehemu kubwa la soko lile, huta wahii skia mkenya akilalama kama nyinyi hapa na kupenda kupewa kila kitu.

Its an open market mkuu, njoo na bidhaa zako utapata wanunuzi, acheni kudanganywa ilhali watanzania wenzenyu wanafanya biashara huku bila ubaguzi.

Kama kuna wafanyabiashara wanaofuatia uzi huu, msikubali 100% kile ambacho mnasoma humu, njooni Kenya mpige biashara, huku hakuna ubaguzi, kuja upige hela usikubali kudanganywa na watu ambao hawajatoka nje ya nchi yao.
 
Tanzania tuseme yatosha kuburuzwa na Kenya kwa mazao ya kilimo. Tuifanye Tanzania iwe Tanzania kwa sasa.

Hivi tumeacha biashara yetu ikatawaliwa na Kenya kwa makusudi au ni bahati mbaya, hasa ya kupeleka mazao ya kilimo nje ya nchi na bara la Afrika.

Bei za mazao yetu ya kilimo zinapagwa na wakenya huko Kenya na ikiwa hawatakuja kuychukua basi bei hudorora mfano Mbaazi, Mahindi n.k Ukienda Mang'ola kwenye vitunguu ni gari za Kenya utazikuta mpaka unaweza kufikiri upo Kenya yaani mpaka huwa najiuliza tumeiacha nchi yetu holela namna hii...

Kuna haja ya kuchukua hatua za haraka kulizuia hili kwani kila siku mkulima wa Tanzania ataendelea kugandamizwa na mawakala na madalali wa kutokea Kenya

1/ Yafaa sasa tuweke kodi kwenye mazao yetu na bidhaa zetu ziendazo Kenya na nchi jirani. Hii imekuwa ikiwarahisishia wanunuzi wa nje kuja kuchukua mazao kwani yamekuwa yakipatikana kwa bei rahisi na hata wakiyafikisha kwao gharama bado inakuwa ndogo na hivyo kuyauza kwa bei sawa na mazao yao.

2/ Kuanzisha mfumo wa udhibiti holela wa uuzaji mazao kwa wakulima. Nadhani kunapaswa kuwa na chombo kinachowasaidia wakulima wetu kuuza na kupanga bei za mazao yao. Hii itasaidia kuzuia wachuuzi hasa wa nje kwenda moja kwa moja mashambani kumlaghai mkulima.

3/ Kutanua wigo wa masoko kwa mazao ya kilimo ya Tanzania nje ya mipaka yetu. Tumekuwa na utegemezi wa soko moja hasa Kenya kwa mazao yetu. Sasa ni wakati tunapaswa kuwaza nje kabisa ya Afrika Mashariki kibiashara. Kahawa ya Tanzania ipelekwe USA, UK, SAUD ARABIA, GERMANY.... na watanzania sio wakenya. Kahawa ya Tanzania ipewe mlinganyo sahihi na bidhaa za nchi nyingine sio kama bidhaa ya Kenya. Mbaazi za Tanzania zipelekwe India na makampuni ya Tanzania sio kama sasa wanavyoamini kuwa ni bidhaa ya Kenya

4/ ATCL ianzishe ndege za mizigo. Hapa ndio pia wenzetu walipotuacha. Makampuni makubwa ya ndege za mizigo yanatua katika viwanja vya Kenya. Hii imesababisha karibia kila bidhaa muhimu kwa wenzetu basi kuna haja ya kuipeleka Kenya ili iweze kupelekwa nje ya bara Afrika kwa haraka. Rai yangu kwa Mheshimiwa rais afikirie pia kununua ndege za mizigo ili hata kama makampuni ya wenzetu hayapendi kutua kwetu basi tubebe vyetu wenyewe na kuvipeleka.

5/ Watanzania tuache fikra mgando ya kuona kuwa nchi za wenzetu hatuaminiki kama wakenya. Wafanyabiashara wa Tanzania pia wao ndio wamekuwa chanzo cha kuifanya Kenya kutufanyia kila kitu. Leo pesa nyingi za kigeni huingia Kenya kwa bidhaa zinazoenda nje ya nchi hiyo japo zimetoka Tanzania. Uchumi wa nchi yetu umekuwa ukidorora kila wakati huku wanaouua ni watanzania mwenyewe na sio setikali yao kama wanavyodhani.

Ifike wakati Taifa la Tanzania Liishi, liwaze, na liamue kama TANZANIA
Zinazo kwenda ulaya aikuumi za kenya tuu .aisee wewe ni mjinga kupita maelezo yaani unataka kusema tanzania kilimo kipungue ili vitu tutakavyo lima visiuzwe kenya na ulaya tena mbaya zaidi mfano wako umetolea vitunguu ambavyo ataa kiwanda cha kusindika kitunguu hakunaga kwa maana kitunguu utumiwakaga fresh kama kilivyo.Je unajua pia kuwa vitunguu vya singida vinaobora wake tofauti na ardhi yake tofauti na vyovyote vinavyolimwa Tz na Ataa sehemu nyingi duniani na vinauzwa arabuni na watanzania wenyewe na je unajua kuwa kitunguu ukikemenya au kukikata nusu akifai kutumika siku ya pili sembuse usindike .kwa kuwa kina uwezo wa kukusanya na kuangamiza bacterea wabaya na hivyo kukigeuza sumu kwa afya ya binadamu iwapo atakitumia baada ya masaa 24 .eetii ulipokuwa unaandika ulijua hilo !!?? Wee lazima utakuwa timu v-wonder
 
Sijui hiyo Tathmini umetoa wapi?Kahawa haiuzwi kenya,kitunguu ya Tanzania huwezi uza ulaya kwa sababu ya standard ya madawa yanayotumika kupiga kwenye kitunguu hivyo huna njia zaidi ya kuuza kenya,Mbaazi sijui ulikuwa unavuta nini?mbaazi inaliwa india na siyo kenya na wanunuzi wakubwa ni pamoja na Mo dewji,mahindi ya Tanzania haitakiwi tena kwa sababu baada ya Tanzania kuzuia ya Zambia iligika kenya na hivyo kuonyesha ina kiwango cha hali ya juu(kwa sababu wanatumia mbegu bora kwa wingi).hiyo akili yako ya kimagu ya kudhani anayenunua mali yako ni adui na siyo mteja mungu akusaidie.
Huyu jamaa mleta mada ni mjinga kupita maelezo yaani kama huu ndio uzalendo magu anaodai basi ni hasara kubwa kuliko faida ndio tutakacho ambulia awamu hii .duuuhhh
 
Back
Top Bottom