Tupitie upya mikataba ya madini na gesi

Musoma Yetu

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
2,633
2,297
Jamani watanzania, nchi hii ilikuwa shamba la bibi kwa kipindi kirefu. Tunaiomba serikali ya awamu ya tano, kwa nguvu iliyoelekeza kwenye watumishi wa umma, vile vile itumike kupitia upya hii mikataba ya madini na gesi , ikiwemo ile sheria ya muswada wa madini na gesi iliyopitishwa bungeni.
 
kwa mkuu huyu huyu wa kaya hili suala ni gumu kama wizara ambayo inaongoza kwa madudu anaogopa kuigusa (ujenzi) itakua hii?
 
Jamani watanzania, nchi hii ilikuwa shamba la bibi kwa kipindi kirefu. Tunaiomba serikali ya awamu ya tano, kwa nguvu iliyoelekeza kwenye watumishi wa umma, vile vile itumike kupitia upya hii mikataba ya madini na gesi , ikiwemo ile sheria ya muswada wa madini na gesi iliyopitishwa bungeni.

Lakini unafahamu vyema sheria za kimataifa za mikataba? jee hio mikataba inaruhusu hicho kipengele cha kuipitia upya maana kuna mikataba imejifunga kwa zaidi ya miaka 100. Kusema ni rahisi kuliko kutenda. Kuhusu mikataba basi Muulize Cuba na issue ya Guantanamo Bay!
 
Tena Raisi afanye haraka sana ili tujue nini kinaendelea kwenye makampuni yanayochimba dhahabu na Almasi mfano GGM, ACACIA, MWADUI, TANZANITE ONE, CATA MINE, na mengine mengi. Pia sheria ya gase na madini ipitiwe upya kabisa. Pia yale maazimio ya bunge ya mwaka jana juu ya IPTL pia yale matrioni ya USWISI yalejeshwe ili tufidie pengo la MCC. Serikali ifanye haraka sana kutafuta wadau watakoanza uchimbaji wa gase mpya iliyogunduliwa hivi karibu ili ianze kuuza nchi za nje na hivyo kuweza kupata fedha za kigeni na kuiimalisa shilingi yetu.

Kama sikosea JK alipoingia 205 alifanya review ya mikataba ya madini enzi Masha waziri wa nishati na madini, vinginevyo ili kuweka kumbukumbu sawa basi mwenye taarifa sahihi atujulishe, ila mie ndivyo ninavyokumbuka kwamba JK alifanya mapitio upya ya mikataba ya madini (compromizing) basi wataalamu wa sheria watujulishe juu ya hilo.
 
Allafu baada ya kupitia.........?kumbuka tulishakubali ku sign bogus treaties
 
Allafu baada ya kupitia.........?kumbuka tulishakubali ku sign bogus treaties
 
Tena Raisi afanye haraka sana ili tujue nini kinaendelea kwenye makampuni yanayochimba dhahabu na Almasi mfano GGM, ACACIA, MWADUI, TANZANITE ONE, CATA MINE, na mengine mengi. Pia sheria ya gase na madini ipitiwe upya kabisa. Pia yale maazimio ya bunge ya mwaka jana juu ya IPTL pia yale matrioni ya USWISI yalejeshwe ili tufidie pengo la MCC. Serikali ifanye haraka sana kutafuta wadau watakoanza uchimbaji wa gase mpya iliyogunduliwa hivi karibu ili ianze kuuza nchi za nje na hivyo kuweza kupata fedha za kigeni na kuiimalisa shilingi yetu.
Mkuuuu nakusikitikia kukuambia usahau.hayo unayoaandika kutokea
 
Lakini unafahamu vyema sheria za kimataifa za mikataba? jee hio mikataba inaruhusu hicho kipengele cha kuipitia upya maana kuna mikataba imejifunga kwa zaidi ya miaka 100. Kusema ni rahisi kuliko kutenda. Kuhusu mikataba basi Muulize Cuba na issue ya Guantanamo Bay!

Mkuu huyu jamaa ni angalizo katoa, maana kama tusipoipitia upya tutajua lini inakwisha muda wake? Ama ni akina nani wanaruhusiwa kujua kilicho kwenye hiyo mikataba? Ni vyema tukajua kilicho kwenye hiyo mikataba hata kama hatutoivunja lakini tujue ilivyo, ama ni watoto na wakubwa tu ndio watapaswa kujua? Maana nina uhakika kama mkataba una miaka 100 hawa walioingia leo hawatakuwa madarakani achia mbali kuwa hai. Huenda ndio maana watu hawataki kutoka madarakani, maana wana mikataba ambayo wazungu wamewalisha yamini kisijulikane kilichomo na hivyo wanaogopa mikataba ikionekana nchi itajaa ghadabu maana sio mikataba ni wizi wa wazi. Na kwa akili zetu hatuthubutu kujua kilicho ndani zaidi ya viongozi wetu. Sasa kama wametunyima hela ni nini tunaogopa kujua kilicho kwenye mikataba yao?
 
Jamani watanzania, nchi hii ilikuwa shamba la bibi kwa kipindi kirefu. Tunaiomba serikali ya awamu ya tano, kwa nguvu iliyoelekeza kwenye watumishi wa umma, vile vile itumike kupitia upya hii mikataba ya madini na gesi , ikiwemo ile sheria ya muswada wa madini na gesi iliyopitishwa bungeni.
nadhani tungeanzia na kuweka migodi iliyobinafsishwa na mwaka ambao serikali ilitiliana hiyo mikataba na wawekezaji.,
then kama kutakuwa na nafasi tujadili juu ya hiyo mikataba na jinsi serikali na wananchi walivyofaidika.
Bila shaka tungepata pa kuanzia.
 
Kuhusu kuitazama upya mikataba hiyo sahau, kwa kuwa baada mataifa ya ulaya kuanza kuiwekea tz vikwazo vya biashara china ndiyo kimbilio lililobaki na hao hao ndiyo wameingia mikataba ya gesi, kuhusu migodi sijui kama ataweza maana watu walishakula 10% siku nyingi
 
Du wadau comments zenu ni interesting kweli. Kama madini tuliingizwa mjini,basi tu sikubali gesi pia kuingizwa mjini
 
Uwezo wa kuvunja mikataba ya kipuuzi hatuna hata kuwajua akina nani walisaini huo upuuzi tunashindwa?
 
Tatizo ni kwamba hii nchi eti mikataba bado ni siri. Hilo ni jipu baya sana kwa taifa
 
Mkuu unachosema ni kweli. Ina maana hata hao walioisaini hiyo mikataba wapo mbinguni au duniani. Mheshimiwa magufuli inatakiwa ashughulike nao mapema kuliko hili la watumishi hewa
 
Na kwanyongeza tu ni kwamba kama raisi amefikia mpaka hatua ya kupungiza mishahara ya maafisa wa mashirika ya umma ili mishahara iendane na hali halisi ya uchumi wa nchi, kwamba kidogo kinachopatikana kisiishie kulipa mishahara minono ya wachache, hivyo basi kwa nia hiyohiyo sheria ya manunuzi ni lazima pia ubadilishwe pia ile zana iliyojengeka siku nyingi ya kusema kwamba mikataba ya madini ni siri nayo pia ibadilishwe na kabla serikali haijaingia mkataba wowote ni vyema ikapitiwa ma wabunge kwakuwa wao pia ni wawakilishi wa wananchi majimboni kwao.

Tukifanya transparance ya aina hii Tanzania itapaa kiuchumi kwa kasi sana.
 
Back
Top Bottom