mwenye shamba
JF-Expert Member
- May 31, 2015
- 1,027
- 1,892
Nguvu ya Taifa lolote ni Wananchi wake, viongozi waliotokana na ridhaa ya Wananchi wake, utawala unaojali zaidi hali ya maisha ya watu wake na kesho yao, utawala ukiwa haujatokana na ridhaa ya Wananchi ni ngumu kufikia agenda za maendeleo kwa sababu kutakuwa na mpasuko baina ya watawala na watawaliwa.
Moja kati ya mambo ya kuzingatia kwa Taifa lolote kustawi ni umoja wa Watu katika Taifa hilo. Ikiwa kila raia anafurahia kiongozi au viongozi ni rahisi kupokea maelekezo na kuyafanyia kazi nje na hivyo sabotage zinaweza kuwa kubwa ambapo watawala watasema tunahitaji twende hivi lakini wananchi nao watasema hatutaki.
Hali ya mpasuko katika Taifa lolote hutoa mianya ya maadui kujipenyeza pia, mfano ikiwa watawala watajua kuwa hawakubaliki na raia wanaweza ku forge alliance na Mataifa yatakayoutambua utawala wao kwa expense za rasilimali za Nchi husika. Hali hii inaweza kupelekea Nchi husika kuharibikiwa zaidi. Umoja ni nguvu. Ili Nchi yoyote iendelee lazima kuwe na masikilizano baina ya watawala na watawaliwa, waliowengi ambao ndio Wananchi wanapaswa kusikilizwa na sio kupuuzwa. Moja ya rasilimali muhimu kote duniani ni rasilimali watu.
Wito wangu kwa Taifa langu ni vema suluhu yenye maslahi mapana kwa Taifa ikafikiwa, mama Tanzania awe ndiye kila kitu, yeyote anayepaswa kuwajibika either ajiwajibishe au awajibishwe ili Taifa lipone. Mwaka juzi na mwaka jana kulishuhudiwa mabadiliko makubwa ya uongozi kwa Taifa la Uingereza na Ufaransa yote ilikuwa kwa masrahi mapana ya mataifa yao.
Kwa sasa hali ya uchumi wa Taifa letu hauko vizuri, mfumko wa bei ni mkubwa na upatikanaji wa pesa ni mgumu huku thamani ya pesa ikiwa imeshuka. Lazima kupatikane viongozi wenye maono makubwa na wenye uwezo wa kuanzisha mambo mapya ili tutoke kwenye hali hii. Nchi nyingi za Afrika miaka mingi zimeongozwa na watawala pasina kuwa serious na mambo yanayowagusa na kuathiri maisha ya watu wao, ndio maana imekuwa rahisi yeyote kuwa kiongozi pasina kujali uwezo wa kiongozi kuleta mabadiliko ya kiuchumi na maendeleo ya mataifa husika, hii imeifanya Afrika kubaki nyuma sana kimaendeleo. Mambo mengi yanayofanyika Ulaya, Marekani na Asia yangeweza kuwa yashafanyika pia Afrika. Mfano kwa hapa Tanzania mji kama Geita ambao umezungukwa na migodi mikubwa ya uchimbaji dhahabu haukupaswa kuwa na muonekano huu na miundombinu hafifu namna hii, licha ya kuwa karibu na ziwa Bado watu wake wanasumbuka na huduma ya Maji, afya na barabara mbovu! Viongozi wa kiafrika ni kama hawajui wapo katika nafasi hizo ili wafanye nini, hauwezi kukwepa influence za mataifa makubwa kwenye rasilimali lakini unaweza kufanya alliance zenye kuwanufaisha wananchi na Taifa lako, shida ufisadi na rushwa na kujilimbikizia Mali Kwa watawala wengi wa afrika umekuwa ni ugonjwa wa kufisha.
Hizi sera za uchumi zinazofanywa na Mataifa mengi ya Afrika hazitoweza kuwainua waafrika na kuendeleza Nchi zao, mfano Nchi nyingi washirika wa Wachina zimejielekeza kwenye kuimarisha miundombinu ya usafirishaji kama reli, barabara na airport ukitizama kiundani ni uwekezaji wa kimkakati wa Mchina kushika uchumi wa Mataifa hayo kwa kurahisisha usafirishaji wa malighafi na bidhaa kwenda na kutoka China, mnufaika mkubwa ni Mchina kwa sababu karibia kila hatua ni yeye anayeshiriki, mfano ujenzi ni Mchina, mzalishaji bidhaa ni mchina ila mlaji ndo Mtanzania. Ni aina ya uchumi ambao hauna tofauti na ule wa kikoloni enzi zile. Sasa niulize je Watawala hawaoni hilo? Flow ya biashara na movement ya bidhaa na watu inarahisishwa lakini mnufaika mkubwa ni nani? Ikiwa Mchina amejaa kila kona ya Nchi je wazawa wanalindwa vipi? Leo ni kwenye sekta ya madini kesho itakuwa kwenye ardhi na biashara zingine. Je huyu mtanzania wakawaida hatokuwa manamba kwenye Nchi yake mwenyewe, ustawi wa Watanzania utakuwaje ikiwa umemuacha Tembo apigane na Sungura? Uwekezaji wa kigeni sio mbaya ila unahitaji sera safi ili kuwalinda wazawa, uwekezaji unapaswa kuwa wa kimkakati, mfano kama ni uchimbaji wa madini ilipaswa muwekezaji wa kigeni afanye tafiti mwenyewe kwenye maeneo mapya na uwekezaji wake uwe ni ule mkubwa utakaofungua milango ya ajira Kwa Watanzania na kuchochea ukuaji wa Technology.
Mungu ibariki Afrika