Tupike biriani ya nyama ya ngo’mbe

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,897
Reaction score
67,394
Hello mliomba nipike biriani hili hapa saa sita tu lishaiva linasubiri walaji mje

Kwanza niliandaa mchele kisha nikauloweka kwa mda wakati nyama inaiva mchele huu ni ule wa basmati baada ya hapo nikauchemsha ule mchele baada ya mda nikaanza kupika kwa kuunganga niliweka mafuta kisha nikaweka mchele na nikaweka rangi yangu nilio itaka

Nikaweka moto mdogo sana yaani ili uive pole pole

Baada ya hapo nyama ilikuwa teyar ishaiva nikaanza sasa kutengeneza sotojo la birian yaan kuipika birian yenyewe sasa

Nikaweka mafuta kisha nikaweka nyama baada ya kuweka nyama nikaweka pilau mix pamoja na kiungo cha birian

Baada ya hapo nikachukua nyanya nilio brendi lakini wakat na brend sikuweka nyanya pekee niliweka hoho na karoti kwa pamoja ndipo nika brendi

Baada nyanya kutokota vizuri nikaweka 🍅 paste kisha nikaweka vitunguu ambavyo nilivi kaanga mwanzoni kisha nikaweka pembeni ili vijichuje mafuta

Nikavichanga vizuri kisha nikaweka na mtindi hapo nikakoroga vzr nikaacha sotojo liichemke baada ya sotojo kuiva ndipo nikaweka kwenye poti

Hivyo

Baada ya hapo nikaipua na wali wangu na kuweka kwa poti teyar kwa kuliwa

Karibuni usikose ndizi muhimu 😆
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…