Tupia jina la mwalimu aliyekuwa mnoko shuleni/chuoni kwenu

Masau bwire wakati anafundisha shule ya msingi Gilman Rutihinda. Alikuwa mkuda sana.
 
Ebwana Mtwara girl's kuna tisha alikua anaitwa sir maulid second master, alikua ni mnoko shule nzima hakuna. Alafu alikua mtaalam wakukamata simu, yaan akikuta unaongea na cm kwanza anacheka alafu anakuacha umalize maongezi baada ya hapo anakun'ganya huku anacheka, kesho paredi unaenda kuivunja mwenyewe kuna mawe special yameandaliwa kwa ajiri ya kazi hiyo.

Alafu sasa ukidoji prepo anakufata bwenn akikuta unaoga upo uchi unakuchapa hivyo hivyo anawaambia pangen mstari wote mnaoga eneo hilo unachapwa fimbo za mikono mkiwa uchi wengine wanamapovu wengine ndo wanaanza, yaaan ilikua raha kweli.

Alafu tuluchokua tunampendea hajui kununa ni best friend, ila ukimuuzi anakuchapa viboko vya maana huku anakupigisha story, tena olewako usimjibu. Yaan anakuchapa huku anacheka, so mwanafunz huna budi kulia huku unacheka.
SHULE RAHA SNA
MLIOSOMA MTWARA GIRL'S HEMBU NJOON
Sir Maulid alikua anawachapa mkiwa uchi?

Sent from my SM-J500F using JamiiForums mobile app
 
NJANGA,KANTALAMBA S.S,alikuwa second master,alikuwa na machale balaa,kila mkibuni njia mpya ya kutorokea anawabamba kiulainii,dah,chanji ndo kijiwe chake ilhali wanafunzi ndo wanaponea!
We usinikumbushe huyu mtu, uko kidedi bondeni yeye yuko kwenye lami anakutambua
 
Hahaha! Ni kweli kabisa mkuu, pale kulikuwa na manunda hatari. Bila shaka wewe ulikuwa Musoma Alliance au Mwembeni. Unakumbuka lile bifu kati ya Mara Sec na Musoma Alliance? Lile bifu ni la kihistoria....tulilikuta lakini hadi tunamaliza shule lile bifu tuliliacha na nafikiri linaendelea hadi leo....uadui wa milele!
lile bifu sisi tulikuwa washiriki/wahanga wakuu ndio tumetia timu. ilikua ikiwa mechi ya kandanda kati ya mara na alliance ilikua haiishi salama
 
Hakuna shule yenye walimu wakali kama jitegemee wakikushindwa wanakusakizia wanajeshi ambao ndio kama walezi na wenye shule. Wengi mmeongea lakini hakuna shule inayogusa pale kwa walimu na walezi wakali.
 
Yani kumbe nawe ni mara sec product ..
Sisi tulikuwa na mkuda mmoja anaitwa mongate..alikuwa shida sana..tulishaandamana kwa ajili Yake hadi kwa mkuu Wa mkoa wapi..alituwinda hakuna mfano ..dawa Yake sasa tukawa hatutoroki mchana Bali usiku kuanzia SAA sita..lakini wapi unaweza kutana nae
Basi unaambiwa kwamba kuna mwalimu anaitwa Bachubila. Jina la utani tulikuwa tunamuita Ruba. Huyu ticha alikuwa hacheki na mtu yeyote yule. Tangu nianze fomu wani mpaka namaliza fomu foo sikuwahi kumuona akicheka. Usiombe ukutane na Ruba hujachomekea shati, hujahudhuria assembly au ukiwa umetoroka shule--utajuta kuzaliwa!

Kuna siku alinitaka niokote makombo ya chakula nimpelekee alishie kuku wake, nikamdis. Siku 1 alinivizia nikiwa natoka DH akanizaba konzi kidogo nizimie! Kisha alinipa adhabu ambayo niliifanya wiki nzima bila ku-attend class. Nilikomaje!

Sasa huyu bwana kiingereza chake kilikuwa na matege. Siku 1 kuna mwanafunzi wa fomu tuu alimpiga mwanafunzi wa fomu wani mbele yake, Ruba akadakia: 'WHY YOU BEAT FORM ONE IN MY FRONT?'. Hapa alikuwa na maana kwamba: 'KWANINI UNAMPIGA FOMU WANI MBELE YANGU?'. Bora hata alipokuwa hajui kiingereza, angekijua angekuwa mnoko zaidi. Kwa kweli mwalimu huyu alikuwa mtata sana, hakuna mwanafunzi shuleni kwetu Mara Sekondari asiyemfahamu huyu ticha mnoko.
 
mkuu huyo morega ni shidaaaaa ndanda boys mbona tulikomaaa....bahati nzuri amehamishiwa pale c tunaingia form6...xo tulienda nae kibishi...!

kwa maoni yangu huyu jamaaa ndo raisi wa walimu wanoko Tanzania
Mara sec tuliminda sana..lakini wapi kama jini. Kuna siku masela wakatega waya nyeusi huku kwenye njia ya nyuma ya mabweni.wakivizia akirudi usiku waya umfanyie mambo..maajabu watu wamekaa hadi SAA NNE wanashangaa anatokea Barbara ya uwanjani..kijana walichoka aisee
 
Yani kumbe nawe ni mara sec product ..
Sisi tulikuwa na mkuda mmoja anaitwa mongate..alikuwa shida sana..tulishaandamana kwa ajili Yake hadi kwa mkuu Wa mkoa wapi..alituwinda hakuna mfano ..dawa Yake sasa tukawa hatutoroki mchana Bali usiku kuanzia SAA sita..lakini wapi unaweza kutana nae
Mimi pia nilipita huko mkuu enzi za mwalimu Salvatory Magessa a.k.a DINGI.
Yani kumbe nawe ni mara sec product ..
Sisi tulikuwa na mkuda mmoja anaitwa mongate..alikuwa shida sana..tulishaandamana kwa ajili Yake hadi kwa mkuu Wa mkoa wapi..alituwinda hakuna mfano ..dawa Yake sasa tukawa hatutoroki mchana Bali usiku kuanzia SAA sita..lakini wapi unaweza kutana nae


Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Kijazi Tanga Technical School,siwezi msahau huyu ikiwezekana akitokea mbele yangu nampanda na tairi aisee....
Mkuu ulikuwaa umewekezaa kwa njeka nini?....maana ugomvi wake mkubwa ulikuwa kwa vidume vyenye tripu zisizoisha za kijijini kwake njekani baada ya kuwatia mimba wadogo zake na ndugu zake kibao...Aisee kama na wewe ni mmoja wao tafadhali kachukuee mtoto wako usomeshe kabla hajaishia kuwa mvuvi....:D
 
Mkuu ulikuwaa umewekezaa kwa njeka nini?....maana ugomvi wake mkubwa ulikuwa kwa vidume vyenye tripu zisizoisha za kijijini kwake njekani baada ya kuwatia mimba wadogo zake na ndugu zake kibao...Aisee kama na wewe ni mmoja wao tafadhali kachukuee mtoto wako usomeshe kabla hajaishia kuwa mvuvi....:D
Ha ha ha ha ha a a a a mkuu emenichekesha sana,kumbe kuna mwenzangu wa mambo ya Kwanjeka na Mkwakwani.Me nilikuwa Faru House.....
 
Back
Top Bottom