Tupeane uzoefu jinsi ya kuishi na mwanamke bila kumpiga makonde

Coke Zero

JF-Expert Member
Mar 30, 2015
1,024
541
Habari zenu wakuu,

Naomba tujulishane jinsi gani naweza kuishi na mwanamke mkorofi na mbishi bila kumshushia makonde, yani nilisha apa kwamba sitokuja kumpiga mwanamke lakini kinachoendelea hapa nadhani siku sio nyingi mtu atakula kibano heavy,

Nimechoshwa kabisa na hizi tabia za huyu mwanamke, yani najaribu kujishusha lakini hamna kinachofaa.

=======

Mwanamke ni rafiki kwanza. Unadhani alipokubali kuishi na wewe akiki zake zilikuwa safarini? Wala.Alikuwa na akili timamu.

Sasa basi, ndo maana mtu hamuoi dada yake au mtoto wa mama mwingine walielelewa pamoja.Wewe unavyoona vinakukela kwake, na ye hivyo hivyo vipo anavyoona vinamkela kwako.Kwa sababu mmekulia mazingila tofauti. Unajua kosa kubwa la wanaume wengi, wanajengea akili za wenzao. Akipita tukani akaingia na kitu eti ataonekana boya, wengine nasikia hata mboga hawezi akapitia.

Na mara zote mwanamke huharibika mwanzoni kutokana na maisha unayoishi wewe.Wengi wa wanaume wanapotongoza huigiza mapenzi ya dhati,na akishapata anasahau.
Jali familia yako, hizo kazi wanazosema ni za wanawake hazipo hata moja.

Mwanamke unamleta ili awe mshauli wa kimawazo na msaada mkubwa.Vile vile aliyeoa ndo anaejua umhimu wa mwanamke ndani.

Usijifanye kidume,piga nae stori,kama una nafasi msaidie kazi,kama mna watoto usimsusie, kaa nao, wapigishe story wacheke.

Watoto ni wa ajabu sana ujue,wakikupenda hata mama yao atakosa pa kuanzia kukuchukia,fanya vitu vingi kwa niaba ya watoto,na anapokosea, mueleze kuwa na wewe sio malaika, ukikosea akueleze,na umuombe awe muelewa akikosea ukamwambia akuelewe.

Af,mambo yenu yaishie ndanibmkisha sameheana usiwe wa kumkumbusha kumbusha yaliyopita.

Hawa viumbe ni kweli huenda kuna nati Mungu hajakaza kichwani mwao,lakini ukimuendea taratibu ni watu wazuli mno.

Ukifika hatua ambayo ukichelewa hali mpaka uje, haogi mpaka muoge wote,hawezi kufanya jambo bila kukuhusisha, ukikwama tu mueleze mshauliane, siyo kwenda vijiweni na kukopa kopa hela bila yeye kujua na kukushauri;utaenjoy maisha nakwambia.

Tengeneza tu mazingira ya kila siku kuwa mpya kwake, usione kwa vile unakaa nae huna time nae.Ulivyokuwa ukimfanyia wakati mnatongozana, viendelee.

Mnunulie tu vitu vidogo vidogo, mtoe out,unajua hawa unakuwa muwazi hata mkifika mkanywa tu soda mkaongea atafurahi,haendi huko kufata chips kuku.

Ukirahisisha maisha ndoa tamu tu.
Mwanamke hata kama ana 70 years anapenda kutongozwa tongozwa tu

Kwanza kabisa nikupe pole kaka yangu ewe mwanaume mwenzangu kusema kweli kuishi na mwanamke kunahitaji akili ya ziada na moyo wa uvumilivu,

Mimi nimeoa mnamo mwaka juzi ukweli kama kumpiga nimeshampiga haswa hadi ikafikia mahala tukatengana akakimbilia kwao wakati huo ana ujauzito wangu wa miezi 9,
Ila kama unavyofahamu ukishazoea kuishi na mwanamke ambae unampenda na kumthamini ni vigumu kuishi bila yeye ukizingatia ndio kwanza ana ujauzito wa mtoto wangu wa kwanza,

Niliamua kuomba ushauri kwa wakubwa zangu wakaniambia dawa ya kuishi vizuri na mwanamke ni KUMPUUZIA AU PINDI UNAPOKOSANA NAE TU TAFADHALI JITAHADHARISHE NA MAAMUZI YA KUKURUPUKA ,UMEKOSANA NAE ONDOKA NYUMBANI TAFUTA SEHEMU TULIZA MAWAZO UKIRUDI NYUMBANI MPUUZIE KWA KILA ATACHOFANYA WE MPUUZIE TU ,

Kinyume na hapo ndugu yangu utajikuta unapata kesi ambayo haukutarajia aisee nawasihi ambao bado hamjaingia kwenye ndoa hebu fanyeni maamuzi magumu na sahihi otherwise mtaingia leo mtatoka leo leo.
 
Sikutaka kuzungumzia sana kwenye ukorofi wake sababu najua tabia za wanawake zinafanana kwa mbali najua hata wewe mpenzi wako ana tabia ambazo ni za kipuuzi,swali ni je unawezaje kumvumilia pila kumshushia kipigo?
mahondaw wangu hana tabia za kipuuzi, ingawa maudhi ya kawaida yapo...


Ni wa kuwavumilia tu, ukiamua kupiga, utampiga kila siku, na utapiga wangapi... Akileta siyo kaa kimya tafuta cha kufanya.. Au toka kabisa rudi baadae...


Cc: mahondaw
 
Ukipiga unajitafutia kesi we ishi nae kwa akili tu hii imeandikwa kabisa kuwa mpole mwenye akili
 
Habari zenu wakuu.
Naomba tujulishane jinsi gani naweza kuishi na mwanamke mkorofi na mbishi bila kumshushia makonde, yani nilisha apa kwamba sitokuja kumpiga mwanamke lakini kinachoendelea hapa nadhani siku sio nyingi mtu atakula kibano heavy, nimechoshwa kabisa na hizi tabia za huyu mwanamke, yani najaribu kujishusha lakini hamna kinachofaa.
Umpige kwani umemzaa wewe?
Zaa wako upige upendavyo.
Jitathmini kwanza ni kwann anakua mkorofi.
Tazama wapi mnapo pishana kiswahili.
Kupiga kuondoe ktk ubongo wako kabisaaa.
Wakati mwingine mwanamke asipo fikishwa vzr akili humkaa upande tazama wapi umepungua urekebishe,hasira na ukorofi wa mwanamke humaliziwa kitandani kaka.
Mke hupigwi.
 
Umpige kwani umemzaa wewe?
Zaa wako upige upendavyo.
Jitathmini kwanza ni kwann anakua mkorofi.
Tazama wapi mnapo pishana kiswahili.
Kupiga kuondoe ktk ubongo wako kabisaaa.
Wakati mwingine mwanamke asipo fikishwa vzr akili humkaa upande tazama wapi umepungua urekebishe,hasira na ukorofi wa mwanamke humaliziwa kitandani kaka.
Mke hupigwi.
Majibu haya mmh. Unawajua vizuri wanawake wewe. Mmekariri kufikishwa kwamba ndio jibu! Tabia kama hizi zikizidi zinauma kwa kweli. Halafu pia baadhi yetu uvumilivu hutushinda
 
Sikutaka kuzungumzia sana kwenye ukorofi wake sababu najua tabia za wanawake zinafanana kwa mbali najua hata wewe mpenzi wako ana tabia ambazo ni za kipuuzi,swali ni je unawezaje kumvumilia pila kumshushia kipigo?
Punguza jazba mkuu
 
Majibu haya mmh. Unawajua vizuri wanawake wewe. Mmekariri kufikishwa kwamba ndio jibu! Tabia kama hizi zikizidi zinauma kwa kweli. Halafu pia baadhi yetu uvumilivu hutushinda
Kwann unaficha weka wazi watu wajadili kwa kina .
Unaficha basi wewe ndio una matatizo.
 
Kwann unaficha weka wazi watu wajadili kwa kina .
Unaficha basi wewe ndio una matatizo.
Nimeficha nini!? Mwambie mleta mada aseme yote kama anaweza. Mimi sina ujasiri wa kuweka hapa ila nayajua, wanawake sio watu wa kawaida. Inabidi utumie akili ya ziada kuwaelewa na sio kukariri humfikishi
 
Back
Top Bottom