Tupeane ujuzi juu ya jambo hili.

bisti

Senior Member
Joined
Aug 29, 2017
Posts
167
Reaction score
152
Kwa mlio na uzoefu wa mambo haya naomba maoni yenu, je? Mahusiano ya kimapenzi yanaweza kudumu bila sex kwa mda mfano miezi 6 na kuendelea kutokana na umbali baina yenu. Na pia uaminifu unaweza hasa Kwa mwanamke hasa awapo mbali? Maoni tafadhali nisiingie kichwa kichwa.
 
Hata zaidi ya miezi 6 ni nyinyi tu wenyewe sema muwe na mawasiliano mazuri
 
Mbona Me Nakaa Miaka Na Miaka
 
haya mambo hayana umbali wala ukaribu

once a slut, always a slut
 
Umbali au ukaribu sio kipimo cha uaminifu, unaeza maliza tu akaenda kumpa na mwingine...
Miezi yote hiyo unakaa bila kupiga? Mmmh
Ndio inawezekana, mimi mbona nina mwaka na miezi sita saivi. Mara ya mwisho mkesha wa pasaka last year.
 
Hata zaidi ya miezi 6 ni nyinyi tu wenyewe sema muwe na mawasiliano mazuri
Asante mkuu wangu, kuna thread nyingi sana humu zinafunguliwa kua wanawake si wa kuamini ndo zikawa zinanipa headache.
 
Umbali au ukaribu sio kipimo cha uaminifu, unaeza maliza tu akaenda kumpa na mwingine...
Miezi yote hiyo unakaa bila kupiga? Mmmh
Mimi naweza bibie na tatizo sina lolote sema namalengo sana na huyo binti. Miezi hiyo nimetolea mfano mkuu.
 
 

Attachments

  • FB_IMG_1505476019997.jpg
    59.2 KB · Views: 48
Kwa sikuhizi uaminifu unaponzwa na umbali wa wapenzi au watu wenye mahusiano.

Waliosoma psychology wanajua kuwa Tabia ya mtu inachangiwa na vitu viwili yaani Asili na Mazingira (Nature & Nurture)

Mwanamke au Mwanaume anaweza kuwa na asili ya Utulivu na Uaminifu kabisa ila akaponzwa na Mazingira anayoishi...hususan watu wa karibu anaoishi nao.

Nafikiri ni bora sana wapenzi wenye malengo waishi pamoja au karibu.
 
Mtakie masomo mema mkuu.....mengine utaona tu matokeo.
 
Mahusiano yote yana changamoto, ila ukiona una wasi wasi kuhusu changamoto hizo kabla hata hujakutana nazo ni dalili tosha kuwa hamtafika popote.
 
Ndio inawezekana, mimi mbona nina mwaka na miezi sita saivi. Mara ya mwisho mkesha wa pasaka last year.
Ni kweli mkuu mimi mwenyewe nina mda tu sijafanya na nipo fiti. Sema ukiwa busy na kazi yeyote tu mi naona kwangu ni Tiba ya kutokutamani ovyo
 
Inawezeka mahusiano yenu kuendelea, ila lazima mkubaliane, kama sio mmoja basi wote muwe na Michepuko...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…