Tuongee kiume, mwendokasi wamefeli

choupa moting

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2016
Posts
1,508
Reaction score
2,577
Habarin za mchana waungwana, poleni na majukumu ya kujenga taifa letu pendwa la Tanzania.

Niende kwenye mada husiku, nimekua mtumiaji wa mwendokasi mara nyingi ninapoenda kwenye mizunguko yangu. Kuna vitu haviko sawa na sijui kwanini havifanyiwi kazi na mamlaka husika inayotoa huduma hii. Sisi kama wananchi na wanufaika wa hizi huduma lazma tusema ukweli maana hatupandi bure, tunalipa pesa hivyo huduma mnazotupatia lazma ziendane na mnachochukua kwetu. Kuna hizi kero ambazo mara nying nakumbana nazo na abiria wanapiga kelele kila siku ila hamna dalili ya kutatuliwa.

1. Magari kupita vituoni yakiwa tupu wakati abiria wapo wanasubiri. Hii imekua kero ya muda mrefu sijui tatizo ni nini. Inawezekana vp magari yanazunguka tu na abiria wapo vituoni hawachukuliwi. Na kwanini kama kuna tatzo kuhusu hili msitoe tamko. Nadhan namna nzur ya kuoandoa dukuduku kama hizi ni kuwasiliana na abiria kuwaeleza mustakabal wa mambo ila sio kama mfanyavyo.

2. Vituo vya mwendo kasi kutokua na sehem za kukaa abiria. Logic ya mwendo kasi mwanzo ilikua ni kufika na kupanda kwenye gari kias ambacho hakuna haja ya kuwa na siti au sehem za kukaa wakat wa kusubir gari, lakn kwa sasa watu wanasubiri vituoni mpaka lisaa limoja au zaidi. Hivi mnategemea abiria awe amesimama muda wote huo? Laki pia kuna wagonja ambao kwao afya inawanyima uhuru wa kusimama muda mrefu. Ina maana hamulioni hilo kweli?

3. Magari kujaza abiria kupita kiasi. Hii ni mbaya sana hata kiafya, kumbukeni kwenye mchanganyiko wa watu wengi vile kuna wagonjwa ambao kwa namna moja au nyingne wanaweza kuambukiza wengine. Magonjwa kama TB na mengine yanayoweza kuambukizwa kwa njia ya hewa ni hatar kwenye mikusanyiko kama hii. Kwanini muwe kisababishi cha maambukizi ya magonjwa?

Kwa namna hizi kero zilivyo za muda mrefu na hakuna mabadiliko ya aina yoyote tuongee tu kiume kwamba MWENDOKASI WAMEFELI.
 
ushauli ni kwamba abiria wanatakiwa kutoa malalamiko yao sehemu husika
 
Huduma zetu badala ya kuimarika kadri siku zinavyo zidi, ila huku imekua kinyume siku zimapo zidi kwenda zinakuwa mbaya. Mfano hao UDART mwanzo walianza vizuri, Ticket na Card ilikua ni automatic now mambo yamekua manual badala ya kwenda mbele wao wanarudi nyuma
 
Huu ni ukweli, management ya UDART/DART imefeli [emoji817]%. Wameshindwa kuanzia ku-manage wafanyakazi wao, vituo, magari na hata hizo tiketi wanazotuuzia.

Ni aibu kwa mradi mkubwa kiasi hicho, uliogharimu mabilioni ya shilingi kuishia kuwa kero kwa watu wa Dar es salaam, ni aibu kwa serikali kufumbia mambo kushindwa kwa UDART.

What the heck is going on with a black race?
 


Madereva kuwa na kauli chafu na kufunga milango kabla abiria hawajamalizika na baadhi yao kubanwa milangoni, wakilalamika wanawajibu hizi siyo daladala mlizozoea
 
Kazi ngumu mpe msukuma, msukuma kapewa udart.
 
Kama tumewezaivuruga nchi toka kwa wakoloni walitujengea misingi imara ya uchumi, kipi tuweze,mswahili hawezi fanya kitu kikafanikiwa.
 
Laiti kero na shida zetu zingegusa viongozi kusingekuwepo na shida.Hulka ya mwafrica ni ngumu sana kushughulika na kisichomgusa.Usitegemee kiongozi watoto wake wanasoma Feza akatatua tatizo la elimu,au anywae MAJI ya CHUPA akajua shida ya maji vijijini. Atumiae helicopter na mav8 akatatua kero ya usafiri,atibiwae Nje akatatua tatizo La Afya hakuna kitu kama hicho tembea Africa ya weusi nzima, ukuti.Shida za Africa ufanana nchi zote.
 
Hayo yote uamesababisha jpili nichelewe kuzika. Total failure. Halafu ukipita yard yao pale mabasi kibao yamelala tu pale
 
Kwani Hapo dar- mmegongelewa misumari simuhame tu' mwishowe mtaambiwa mtembee kwa miguu' kama wale walioambiwa wapige mbizi hakuna wakuwasikiliza kilio chenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…