Tungo: Leo utahonga laki

Tungo: Leo utahonga laki

nentewene

Senior Member
Joined
Jun 9, 2017
Posts
144
Reaction score
94
Leo utahonga laki, kesho atataka dola.
ukimnunulia mishkaki, atadai na kijora.
yani hawasomeki, ni nyingi zao hila.
michekupo hawaridhiki, zitaisha zako hela.

Utampeleka samakisamaki, ila nyumbani hawajala.

Utamkodia pikipiki, ila mkeo daladala
utampeleka Denimaki, kama mtoto wa Kajala.

Mwisho utakua dodoki, na atakufanya fala.

Michekupo hawaridhiki, zitaisha zako hela.

Utalala kwake wiki, ila bado atazila.
Utampa kadi ya benki, bado atadai dira.

Ukijifanya fulubeki, atakuchezea mpira.
achune zako steki, ubakie na kipara.
michekupo hawaridhiki, zitaisha zako hela
 
Back
Top Bottom