Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Anaandika Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu
Nilikwenda kushuhudia siku anatoa maelezo polisi. Walikuwa wanadai Juve ndiye aliyeandika ujumbe juu ya mpango wa kumuua Mh. Lema lakini hawakuwa na ushahidi wowote zaidi ya kwamba alikuwa member wa grupu mojawapo lililopokea ujumbe huo.
Wanajua hawana grounds za kumkamata wala kumshtaki kortini. Sasa wanamtesa tu kwa sababu ni mwanachama wa CHADEMA. Hivi ndivyo ulivyo utawala wa kidikteta wa JPM. Huyu anayejenga uwanja wa ndege mkubwa kwao bila haya yoyote sawa na Mobutu Sese Seko.
Huyu aliyeweka taa za barabarani katika Kijiji cha Chato wakati hazipo katika miji yote jirani kama Geita, Kahama, Bukoba, Kigoma, n.k. Huyu anayejenga ofisi ya TRA yenye ghorofa mbili kijijini kwake Chato wakati Kijiji hicho hakina mapato yoyote ya maana ukilinganisha na mji jirani wa Katoro.
Huyu aliyejenga jengo kubwa la MSD Kijiji cha Chato wakati Makao Makuu ya Mkoa hakuna duka la MSD. Huyu aliyemwajiri mpwa wake Dotto James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali ili watumie pesa za Serikali wanavyotaka bila kufungwa na taratibu za fedha za umma.
Ndio maana anakamata na kutesa wapinzani. Ndio maana hataki mikutano ya kisiasa ya vyama vya siasa. Ndio maana anataka kuua mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini. Wale wanaosema turudi kwenye mfumo wa chama kimoja hawajui walisemalo na Mungu awasamehe bure.