1. Kwanza, wapo Majaji ambao – kwa sababu ya kutokufanyiwa vetting na Tume ya Utumishi wa Mahakama – hawana uwezo wa kuandika mwenendo wa mashauri na hukumu zinazosomeka kwa sababu ya, ama kutokuwa na uwezo na ujuzi wa sheria, au kutokuwa na weledi wa lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo lugha rasmi ya mwenendo wa mashauri na hukumu.
2. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inazo taarifa kwamba wapo Majaji ambao – kwa sababu hizo hizo za kutokufanyiwavetting juu ya uwezo na ujuzi wao na mamlaka husika ya kikatiba – wameshindwa kabisa kuandika hukumu za kesi walizozisikiliza na hivyo kusababisha mlundikano wa kesi mahakamani usiokuwa na sababu yoyote ya msingi.