Chama cha wanasheria wataka tume huru kuchunguza majaji wa Tundu Lissu, wampinga Ngw'ilizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama cha wanasheria wataka tume huru kuchunguza majaji wa Tundu Lissu, wampinga Ngw'ilizi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Sep 21, 2012.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Chama cha wanasheria Tanzania, TLS, kimemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano kuteua tume ya kijaji, ambapo zaidi ya nusu ya hao majaji wanapaswa kutoka nchi za commonwealth nje ya Tanzania ili kuchunguza tuhuma alizozitoa Tundu Lissu kwani zinashusha kabisa hadhi ya mahakama zetu. Kauli hiyo imeto9lewa na mwenyekiti8 wa TLS ndg Stolla. Alisema kauli ya Ngwilizi kuwa watu wasizungumzie madai ya Lissu haina msingi kwani Bunge halina mamlaka ya kuichunguza mahakama bali mahakama inachunguzwa na tume huru iliyoundwa kwa mujibu wa sheria.

  Source: Daily News ya leo

  My take: TLS ikiendelea kushikia bango hao majaji wote wanaotuhumiwa wataondolewa. Tatizo tu ni kuwa wanaogopa kisiasa itakuwa na madhara. Habari za ndani ya mahakama zinasema baada ya CJ kumwondoa Jaji wa mahakama ya rufaa (sic) Mborouk katika kesi ya Lema hatapangiwa tena kazi ya kuamua kesi maana ukweli sio jaji kisheria. Aliondolewa baada ya Lissu kutishia kuwa kabla ya kuanza kusikiliza kesi hiyo angeweka pingamizi kuwa mbele pamekaa majaji wawili badala ya watatu wanaostahili kukaa kisheria, angeulizwa mbona wapo watatu angesema huyo mmoja hakustahili kuwa jaji maana uteuzi wake ulivunja katiba. Baada ya CJ kupelekewa ujumbe akaamua kumwondoa ili kuepuka aibu. Hili ndio tatizo la uswahili unateua watu kishkaji ambao hawana uwezo wakati kuna brains nzuri sana Tz
   
 2. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Te te te! kwi kwi kwi kwi!
   
 3. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  huo ndo ukweli wenyewe. lisu ni noumaa.
   
 4. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Chadema wapo makini sana na game of politics wanaicheza vyema sana.kwa ujumla wanafurahisha
   
 5. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  mkuu kwanza asante sana umenifumbua macho nilikua sijui mchezo mzima unaoendelea nyuma ya pazia..
  kwa hiyo lisu kawaumbua wakubwa?? hali iliyopelekea wachukue maamuzi magumu kisheria ili kulinda katiba au kulinda hadhi yao kisiasa??
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Ninakubaliana na wewe kuhusu nafasi ya TLS. Tumeona ni jinsi gani wanasheria Kenya wanavyopaza sauti kila mara serikali inapokwenda kinyume na katiba. TLS kwa muda mrefu imekuwa inakaa kimya kiasi sasa wanasheria wanaokana kama mashuhuda kama si washiriki wa ujambazi unaondelea nchi hii. Pengine kwa kababu baadhi yao wanapata 'tender'/kazi huko huko serikalini. i.e Rex attorneys.

  Ukificha maradhi kifo kitakuumbua, TLS sasa wanaona aibu iliyoikumba upande wao. Unakuwaje na jaji wa mahakama ya rufaa asiye hata na degree ya sheria? This is a scandal of biblical propotions! Ni aibu mno na itabakia kuwa aibu kwenye vitabu vya historia ya nchi hii. TLS wanatakiwa sasa wapambane to restore the badly damaged reputation ya taaluma yao.
   
 7. F

  Froida JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  TLS wasimamie haki wafanye kama vyama vingine vya kisheria vinvyofanya kazi wasiendekeze siasa bwana
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kama TLS wataamua kwa dhati kabisa kushikilia msimamo huu na pengine wapige hatua moja mbele kwa kukataa kufanya kazi na majaji wote wasiostahili kufanya kazi za ujaji, ambao uteuzi wao umefanywa kinyume na misingi ya katiba na sheria. Kwa kufanya hivyo naamini kabisa watawala hawatathubutu tena kuteua ndugu, jamaa na marafiki katika nafasi nyeti kama hizi za mhimili wa mahakama.
   
 9. i

  iseesa JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi hiyo kesi itakuwaje? Alute Mghwai upande wa MAGAMBA na Nduguye Tundu Mghwai upande wa CDM? Huu ndio ukomavu wa wanaoijua sheria. Wote wanatafuta ukweli (Kina Mghwai)
   
 10. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Ni ukweli uliowazi TLS wanatakiwa wapambane na hili suala mpaka huo uozo MAHAKAMANI usafishwe wajifunze wenzao wa nchi nyingine wanavyopambana mpaka tone la mwisho kupambania mambo yanayohusu TAALUMA ya SHERIA kenya wameweza na TLS inaweza kama vipi ifunguliwe kabisa kesi ya KIKATIBA sababu huo uteuzi ni UN-CONSTITUTIONAL na VOID ABNITIO.
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Sep 21, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,411
  Trophy Points: 280
  Hao TLS wapuuzi kabisa. Wewe utamuombaje mtu huyo huyo aliyewateua hao majaji ambao wanatuhumiwa kukosa sifa aunde tume ya kijaji ili iweze kuchunguza madai yaliyotolewa na Lissu dhidi ya hao majaji wasio na sifa?

  Yaani rais aunde tume ya kuchunguza appointees wake ambao wanadaiwa hawana sifa?

  That is a case of monumental stupidity if you ask me.
   
 12. N

  Noboka JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,144
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Heeeeeeeee, kulikoni huyo Tundu Lissu si ndiyo wakati wa kikao kilichopita wabunge wa magamba walikuwa wanasema ni mwehu? du Kweli anayesupport magamba anatakiwa kujilaumu lile ni genge la vibaka tu
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  tume tume tume
   
 14. mka

  mka JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu hivyo ndivyo Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inavyotamka, kuwa Rais ndio mwenye mamlaka ya kuunda tume ya kuchunguza majaji. TLS sio wapuuzi na hawajakosea wao wametamka namna ambavyo sheria za nchi hii zinavyosema, pitia katiba mkuu uone inasemaje. Hakuna chombo chochote chenye mamlaka ya kuunda tume ya kuwachunguza majaji zaidi ya Rais kulingana na katiba ya sasa. Labda utoe maoni ili katiba mpya iwe na utaratibu wa tofauti.
   
 15. M

  Mundu JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Walitakiwa wafanyeje mkuu?
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Sep 21, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,411
  Trophy Points: 280
  Katiba ina makosa. Sasa hao TLS hawajaliona hilo?

  Na kweli TLS wanategemea rais aunde tume huru ya kuchunguza appointees wake ambao wanadaiwa hawana sifa?

  Hiyo tume ikija kutoa ripoti yake na ionekane kweli hao majaji hawana sifa huoni kama hiyo itakuwa indictment kwa rais?

  Na unadhani rais yuko tayari kwa hilo?

  Mteuzi anateua tume ya kuchunguza wateuzi wake....wow!
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Sep 21, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,411
  Trophy Points: 280
  Hivi kabisa hakuna loopholes walau ya kuwa na at least bipartisan commission au hata kamati ya bunge yenye kushughulika na mambo ya sheria kuinda hiyo tume huru?

  TLS na usomi wao wote wameshindwa kabisa kutafuta hata ka loophole kamoja?
   
 18. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Lissu kila moto anaoanzisha watu lazima watafutane. Alianza na muungano, serikali ikasahau hoja zake na kuhamia kwa Lissu. Kahamia kwa majaji, leo hawataki tuongelee.
   
 19. p

  politiki JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  TLS is hopeless organization, mambo mengi yamefanyika kinyume cha sheria bila TLS kufanya chochote.
  cha msingi hapa ni kwa katiba mpya kuweka kipengele cha wateule wote lazima wapitishwe na bunge ili kujua
  kuwa wanafaa au vipi ? Obvious mtu kama mbarouk asingeweza kupita kabisa kwa sababu hana sifa ya kuwa judge.
  Rais wa nchi akijua wazi kuwa wateuliwe wake watakwenda kuchambuliwa na bunge atakuwa makini kwa maana anajua wakikataliwa ni aibu kwake lakini hivi sasa anafanya hivyo kwa maaana anajua vyombo kama TLS vimelala usingizi mzito mpaka wanatokea watu makini kama Tundu Lisu kufanya kazi ya TLS ni aibu kwa kweli.
   
 20. M

  Mundu JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Yeah, huo ni ushauri mzuri, maana naona kesi ya ngedere inapelekwa kwa kaka yake ngedere.
   
Loading...