Tundu Lissu: Sisitiza Iundwe Tume Huru Kuchunguza Uteuzi wa Kishkaji wa Majaji

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,545
550
Madai uliyotoa ni mazito sana. Ila ukweli hili si jambo jipya kwani watu wengi wanalalamikia kitendo cha JK akipelekewa majina ya watu wanaofaa kuwa majaji anaongeza majina yake.

Mimi nilishawahi kumsikia jaji Ramadhani kabla hajastaafu akilalamika pia. Kwa kuwa kwenye tume kuna uwakilishi wa TLS, ni rahisi kupata ushahidi wa kutosha.

Kuteua majaji kishkaji kuna madhara makubwa sana kwa nchi. WATANZANIA TUSICHUKUE MAMBO KILAINI, HILI TAIFA LINAZIKWA.

HUWEZI KUACHA VICHWA VIZURI VINAVYOFAA KUWA MAJAJI NA KUANZA KUTEUA WATU KWA KUWA NI WASHKAJI WAKO
 
Ushahidi upo wazi kuna majaji hawawezi hata kuandika hukumu na nakala za hukumu tunazo ambazo hata mwanafunzi wa mwaka wa pili sheria hataandika hivyo.

Watu wanaokotwa tu barabarani na wengine wamebakiza muda mfupi kustaafu wanapewa fadhila.

Mfano jaji shahidi alikuwa dpp akastaafu akapewa ujaji hakufanya hata miaka miwili akastaafu na akalipwa marupurupu yote ya ujaji.

Kwanini tuingie gharama kama nchi kuteua watu wamebakiza muda mfupi sana ili wapate marupurupu, maana wanalipwa asilimia 80 ya mshahara hadi wafe
 
Watu wanadhani Tundu Lissu anajisemea mwenyewe tu. Wahafidhina wa muhimili huu wa Dola wamepata pa kutolea madukuduku yao.
 
Katika hotuba yake bungeni, Mhe. Tundu Lissu alisema hivi, namnukuu
1. Kwanza, wapo Majaji ambao – kwa sababu ya kutokufanyiwa vetting na Tume ya Utumishi wa Mahakama – hawana uwezo wa kuandika mwenendo wa mashauri na hukumu zinazosomeka kwa sababu ya, ama kutokuwa na uwezo na ujuzi wa sheria, au kutokuwa na weledi wa lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo lugha rasmi ya mwenendo wa mashauri na hukumu.
2. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inazo taarifa kwamba wapo Majaji ambao – kwa sababu hizo hizo za kutokufanyiwavetting juu ya uwezo na ujuzi wao na mamlaka husika ya kikatiba – wameshindwa kabisa kuandika hukumu za kesi walizozisikiliza na hivyo kusababisha mlundikano wa kesi mahakamani usiokuwa na sababu yoyote ya msingi.
Mimi naamini kabisa kuwa hoja za Mhe. Lissu ni kweli, lakini hizi ni shutuma nzito sana, kwa hivyo, Mhe. Lissu angewaaminisha zaidi Watanzania kwanza kwa kuwataja Majaj husika ambao wameteuliwa na Raisi bila vetting, pia angaweka mifano hai ya maandiko hayo mabovu ya majaji husika.

Kama angefanya hivyo, kusingekuwa na haja ya kuunda tume kulichunguza hilo, na hata kama ingeundwa, basi tume hiyo ingekuwa inachunguza ushahidi uliowasilishwa. Pia, angekuwa ameweka kikwazo kwa "Nyundo ya CCM" wanayoitumia siku zote ya "Lete ushahidi."

Na hapo kwenye blue, ninawashauri wabunge, hasa wa kambi ya upinzani, wapeleke pendekezo la kubadilishwa hiyo
lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo lugha rasmi ya mwenendo wa mashauri na hukumu na badala yake tutumie Kiswahili kuwa ndio lugha ya hukumu. Utaandikaje hukumu kwa lugha ya Kiingereza wakati kesi ilisikilizwa kwa Kiswahili na pengine mshitakiwa / mhukumiwa hajui hata cha kuombea maji?
 
I Agree with you, Lisu anaweza pia kupeleka hoja binafsi juu ya uteuzi wa rais kwa ujumla
 
Watu wengi wanadhani Tundu anaropoka kwenye hoja zake lakini mimi namfahamu huyu jamaa. Ni mtu makini na haogopi chochote humu duniani ikiwa ni suala la kutetea haki!!

Rais Kikwete anajulikana kwa sifa ya kutokuwa mwangalifu katika mambo muhimu ya Taifa. Inawezekana sana akawa anaongezea majna kwenye list inayopelekwa!! With our president, this is very possible!!
 
Tundu is right kabisa. Hata majaji wenyewe wanalalamika. Tena hata hawa wapya 10 yumo
mmoja ambaye JK inasemekana kamchomeka. Lakini, Maspika wetu wawe na ustaarabu,
kwani kambi nzima ya upinzani si kila wanachosema ni uongo. Na ukiwasikia wana ccm
haraka haraka wanakanusha taarifa ya wapinzani ujue kuwa jambo hilo ni kweli kabisa.

Tundu si mjinga hata aende akasome kitu kisicho na ushahidi, lazima kapewa data na wahusika.
Kwa kazi kubwa ya Ujaji inayohitaji jaji kusoma mafail yasiyopungua 4 kwa siku, haihitaji lelemama ya
kuweka mtu mchovu au asiyependekezwa na mahakama. Ikumbukwe kuwa mahakama ndiyo inayojua
ugumu wa kazi yake. Unapowaweka watu ambao haijawapendekeza ni kupeleka mgogoro wa kichini chini
ndani ya chombo hicho tukufu.
 
Na hapo kwenye blue, ninawashauri wabunge, hasa wa kambi ya upinzani, wapeleke pendekezo la kubadilishwa hiyo lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo lugha rasmi ya mwenendo wa mashauri na hukumu na badala yake tutumie Kiswahili kuwa ndio lugha ya hukumu. Utaandikaje hukumu kwa lugha ya Kiingereza wakati kesi ilisikilizwa kwa Kiswahili na pengine mshitakiwa / mhukumiwa hajui hata cha kuombea maji?

Sawa kabisa! Katika mambo ya kijinga Tanzania hilo la kutumia Kiingereza mahakamani ni mojawapo. Yaani ni ujinga, ujinga, na ujinga mwanzo mwisho.

Wanatumia Kiingereza kwa faida ya nani? Na afadhali basi Kiingereza chenyewe wangekuwa wanakijua.
 
hivi JK ana washkaji wangapi? maana kuanzia mawaziri, wakurugenzi wa mashirika ya umma, wakuu wa mikoa na wilaya kila sehemu tunasikia kaweka washkaji/ndugu/ zake..anao wangapi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom