Tundu Lissu naye aitwa polisi kwa mahojiano, ahojiwa kwa saa moja

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,814
34,196
Tundu Lisu.jpg


TUNDU LISSU NAYE AITWA POLISI KWA MAHOJIANO AHOJIWA KWA SAA MOJA

TUNDU Lissu, Mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pia Mbunge wa Singida Magharibi leo jijini Dar es Salaam amehojiwa na Jeshi la Polisi kuhusu hoja alizozitoa kwenye Gazeti la MAWIO.

Lissu amehojiwa kwa zaidi ya saa moja Makao Makuu ya Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam baada ya kuhitajika kutoa maelezo kwa madai ya kutoa kauli za uchoelezwa zilizoandikwa kwenye Gazeti la MAWIO zilizohusu mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Habari iliyoandikwa na gazeti hilo iliyobeba kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Zanzibar’ inaelezwa kuwa sababu ya serikali kulifungia gazeti hilo tarehe 15 Januari mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kutoa maelezo Lissu amesema, serikali inajaribu kumziba mdomo asizungumzie kuhusu suluhu ya mgogoro wa kisiasa unaoendelea visiwani Zanzibar wakati wahusika hawazingatii misingi ya demokrasia.

“Wale waliobebwa kwenye uchaguzi leo wanataka kutufumba midomo tusizungumzie masula ya uchaguzi wa Zanzibar kwani machafuko yanaweza kutokea visiwani humo kwa tahadhari hiyo wanatuita wachochezi,” amesema Lissu.

Amesema kuwa, wao wametoa tahadhari ili yasitokee machafuko na umwagikaji wa damu na kwamba, Rais John Magufuli atawajibika kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kama alivyowajibishwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.

Amesema, mahojiano yake na Gazeti la Mawio ndio yaliyosababisha yeye kuitwa na kuhojiwa na polisi na kwamba, mtazamo wake ulioandikwa kwenye gazeti hilo ndio umechangia kufutwa kwa gazeti hilo.

Amesema kuwa hatokubali kuzibwa mdomo hata kama watatumia nguvu ya polisi.

Amesema, hatua ya Rais Magufuli kukakataa kujihusisha na mgogoro wa Zanzibar haikubaliki kwa kuwa ndiye ndiye atakayepeleka jeshi pale vurugu zitakapotokea.

Lissu amefika polisi hapo akiwa na mawakili wa watatu wa Chadema ambao ni Peter Kibatala, Fedrick Kiwelo na Hekima Mwasibu.

Amesema, baada ya mahojiano hayo polisi watapeleka jalada lake kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa hatua zaidi.

Chanzo : Mzalendo.Net
 
Yetu macho lissu is the man to watch he is great sio kina kubenea type the government should not play with this man
 
Magu anaikataa Zanzibar lkn fujo ikitokea yupo tayari kupeleka wanajeshi kwenda kupiga watu ila kwenye kuzuia fujo zisitokee hayupo. Akili matope hizi

Aseme hadharani yeye ni rais wa
Tanganyika. Full stop.
 
Hiyo ICC mpaka leo wanaiongelea hawa bwege?? Besigye anagongwa kila siku na Mu7 hajapelekwa ICC, mtasubiri sana na Magufuri atawagonga kwa tabia mbovu kama Hizo.
 
Si gazeti lilishahukumiwa tayari (kwa kulifuta)?

Sasa wanawahoji watu wa nini tena?

Na ikitokea kesi ikaenda mahakamani na mshtaki akashindwa, Nape atalifungulia "maisha" gazeti?
 
Kama wameleta uchochezi wafundishwe jinsi ya kutii sheria bila shuruti!

Wakileta fyoko fyoko washikishwe..
 
Si gazeti lilishahukumiwa tayari (kwa kulifuta)?

Sasa wanawahoji watu wa nini tena?

Na ikitokea kesi ikaenda mahakamani na mshtaki akashindwa, Nape atalifungulia "maisha" gazeti?
Kipeperushwi cha Mawio hakijafungiwa KIMEFUTWA
 
Katika maadhimisho ya CCM huko Singida, ni JINA moja tu la kiongozi wa Upinzani lililotajwa bila kificho kutoka mdomoni mwa kiongozi mwandamizi wa CCM, nalo si lingine bali la TUNDU LISSU. Wengine waliitwa "yule jamaa, bwana mkubwa."

Hii inaonyesha UTISHIO wa Mbunge huyu Kwa Chama tawala.
 
Hiyo ICC mpaka leo wanaiongelea hawa bwege?? Besigye anagongwa kila siku na Mu7 hajapelekwa ICC, mtasubiri sana na Magufuri atawagonga kwa tabia mbovu kama Hizo.

Tabia nzuri ni kutetea mwizi na mdhulumati wa kura za wananchi siyo?????????!!
 
Hiyo ICC mpaka leo wanaiongelea hawa bwege?? Besigye anagongwa kila siku na Mu7 hajapelekwa ICC, mtasubiri sana na Magufuri atawagonga kwa tabia mbovu kama Hizo.
mkuu marekani na washirika wake huingilia migogoro ambayo huona kwao ina maslai, yani kama burundi, zimbabwe na uganda zingekuwa na rasilimali kama za kwetu, mbona marekani ashadidndisha kitambo, sema hizo nchi ni tupu
 
Lissu kitu gani banaa asicheze na serikali..huyu mkichaa ndio mnataka kutuaminisha ni mtetezi wa wanyonge??? huyu ni mwizi alie upande wa upinzani period.
 
Binafsi sikubaliani na kauli ya Magu alipokuwa akiongea na wazee wa Dar juu ya suala la Zanzibar. Kama wapo waliomshauri sidhani kama walitumia busara. Kusema tume za uchaguzi ziko huru wakati tunajua kabisaa katika ubunge huwa wakienda mahakamani mwishowe inadhihirika haziko huru ni kuinamisha kichwa upepo ukivuma ukijua vumbi likija halitaugusa mwili wako maana hauonekani. Suala la kwenda mahakamani alilolisema anasahau kuwa matokeo ya urais yakishatangazwa hayapingwi mahakamani. Hapa naona Magu amekuwa more of CCM kuliko Mr President na hii si salama kwa mstakabali wa amani ya nchi yetu. Mbona ilipofika kupeleka majeshi alisema kwa nguvu zote na jeuri yote wakati wahenga walishatueleza 'kinga ni bora kuliko tiba'? Naamini kuna kitu nyuma ya pazia katika uchaguzi wa Zanzibar ambacho kila huyu anaogopa kukigusa na ndicho bila shaka kilimfanya Jecha aamue kibabe na kuendelea kupata support ya kibabe toka wa walio na fahamu ya kitu hicho. Mi bado naamini sheria zipo kutusaidia na si kila kitu lazima kiamriwe kwa sheria tu, busara pana inahitajika hasa pale tunapotambua kama kwa kufuata sheria tu tutapoteza kikubwa zaidi na kwangu umoja wa taifa letu ni kitu kikubwa zaidi kuliko madaraka ya kugombaniwa na CUF na CCM katika visiwa hivyo vya Zanzibar
 
Back
Top Bottom