Click_and_go
JF-Expert Member
- Nov 21, 2010
- 451
- 6
Mheshimiwa huyu wa Singida asipoangalia vema umaarufu wake utamomonyoka vibaya. Mfano. kwa kitendo chake cha jana bungeni kuomba bunge liahirishwe kwa kuwa jaji amem-issue summons ni kituko cha ajabu kuweza kufanywa na mwanasheria na msomi mahiri kama yeye.
Ili kuweza ku-maintain status yake ni lazima afanye utafiti kwa kila anachotaka kukifanya na kukiongea ktk ulimwengu huu wa siasa. Akitanguliza ushabiki na kutaka kujenga jina haraka haraka inawezekana mwaka 2015 jimbo lake likawa na mbadala.
Aige mwenendo wa Bosi wake Dr Slaa. Kila alichokuwa anataka kukiongea(Bungeni) alikuwa anafanya utafiti wa kina na akikiongea kinakuwa na mashiko.
Ni ushauri tu lakini
kwahiyo wewe unaona ni kawaida tu, yaani mbunge yuko kwenye kikao, afu anapewa sumons afu akae kimya, spika alitakiwa kuwa na busara, kwakumwambia kwasababu uko kwenye kudiscuss sensitive issue, basi naahirisha mjadala. Wana jf sisiem ni wajanja sana, walijua bila kumwondoa kwenye mood mh. Lissu ingekua balaa, kwahiyo ni hila za kimakusudi zilifanywa na sisiem kumdhoofisha lissu. Lakini pamoja na hilo kama mwanasheria aliebobea bado aliendelea kujaribu kupambana. Katika mapambano silaha yoyote ile unaitumia hata kama ni fimbo, jiwe au tawi la mti.
wewe umetumwa nini,yaani kwa namna yoyote mnatafuta kuwarudisha nyuma wapigania uhuru wetu,wewe sawa na wabunge wengi wa chama chako nadhani mnafikiri kwa makalio wala si kichwa kama unahisi Tundu kakurupuka wewe umefanyaje!!mwanaume mzima akili kama za Kilango!!umenchefua tu yaani!
Hata mie ambaye ni kilaza nilishangaa sana. Nafikiri ana haraka au tuseme usongo sana, sijui nasubiri.
shida ya humu ndani ni ushabiki tuu, hawana ushauri kabisa kwa hao wanaowashabikia, huo si urafiki maana rafiki ni yule anayekushauri na kukuaripia kwa mabaya uyafanyayo.
kwa hiyo kuku anzaaa yai au yai linazaa kuku??kati ya summons na kuomba muongozo wa spika nini kilianza??
unaudhi
unakera
unaleta hasira
nyambafuuuuuu
hizi ndizo busara zangu zakwako zikowapi??wewe
Jamani hapa hoja hujibiwa kwa hoja, matusi na kashfa si sehemu ya kujenga hoja, kama huna la kuchangia nibora uipotezee thread kuliko kuongea ushabiki na upenzi kama wa simba na yanga.
Kama sijakose hii ni mara ya nne sasa toka siku ya bunge la kwanza kumona lisu akiomba muongozo kwa jazba na kukurupuka na mara zote mama makinda amekuwa anambeat vibaya kwa kuonyesha hajui anachoomba.
mfano jana amepewa samansi kimakosa wakati bunge linaendelea lakini kama msomi wa sheria angeatafakari kwanza namna ya kuhandle issue ile na si kukurupuka na kuanza kuomba eti dharura, na alipotakiwa asome kifungu alichemka kwanza akaambiwa kaa chini soma jipange tena, na hata baada ya kujipanga akasoma kifungu ambacho aliulizwa je kinafit kwa unavyoomba, akabaki ametoa macho.
Wito bado mapema mno atulie, au achukue mifano ya wenzake zito na dr walivyofanya
Acheni ujinga mheshimiwa alichemka. Alitaka kusikilizwa kwa manufaa ya uma. Uma wake na uma wa bunge zima ni upi. Was that important. Mimi huku niliko nilishangaa kuona ametoa mipua yake ati anataka kuahirisha bunge kwa umaarufu wa jazba. CHADEMA wasipo angalia wataonekana wacheza majoka bungeni na nje ya bunge. Wasomi waliopo CHADEMA wajifunze kujenga hoja kwa utafiti na kuondoa jazba kama za kijinga. Bungeni ni mahali pa maana bwana. Sio mahali pa mijadala ya kitoto....unauliza kirefu cha SADC bungeni kwa manufaa ya nani??
Mheshimiwa huyu wa Singida asipoangalia vema umaarufu wake utamomonyoka vibaya. Mfano. kwa kitendo chake cha jana bungeni kuomba bunge liahirishwe kwa kuwa jaji amem-issue summons ni kituko cha ajabu kuweza kufanywa na mwanasheria na msomi mahiri kama yeye.
Ili kuweza ku-maintain status yake ni lazima afanye utafiti kwa kila anachotaka kukifanya na kukiongea ktk ulimwengu huu wa siasa. Akitanguliza ushabiki na kutaka kujenga jina haraka haraka inawezekana mwaka 2015 jimbo lake likawa na mbadala.
Aige mwenendo wa Bosi wake Dr Slaa. Kila alichokuwa anataka kukiongea(Bungeni) alikuwa anafanya utafiti wa kina na akikiongea kinakuwa na mashiko.
Ni ushauri tu lakini
Tundu Lissu na wenzake ma Novice wa Chadema wanatafuta Cheap popularity bungeni hawajaenda pale kutatua matatizo ya wananchi wao.