Tundu Lissu na Mbowe wajibu makombora

Tundu Lissu na Mbowe wajibu makombora

Huey freeman

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2013
Posts
593
Reaction score
248
Msimamo wa UKAWA kuhusu Bunge la Katiba. "Wakati tunagomea Bunge la Katiba tulikuwa na sababu za msingi na bado zipo, hazijatatuliwa wala hazijafanyiwa Kazi, na kwa kkuwa hazijatatuliwa, tutaendelea kubaki nje ya Bunge.

"Lakini hatuwezi kurudi pale kwenda kutukanana, kunyanyasana na kuvunjiana heshima. Haileti maana kabisa, kitu ambacho si malengo ya Bunge la Katiba. "Msimamo wetu wa kususia Bunge la Katiba si wa kudumu, unasababishwa na mazingira. Watu wakae chini, watatue matatizo, na yakimalizika watu watarejea Bungeni, lakini kama hatukutatua, itakuwa kama watoto wadogo wasiofanya taathmini wala kujua athari ya kitu.

Kauli ya Mbowe kuhusu Kauli za Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mtungi.

*Sifa za kugombea tena!

Kuhusu nafasi zao kwenye vyama kuwa hawana sifa na wanabanwa na Katiba kama ilivyosema Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa, Mbowe aliiponda Kauli hiyo akisema kuwa anaweza kuzungumza chochote na kwa kuwa Msajili si mahakama, anaweza kutoa tafsiri yake kwa mtazamo wake, lakini uhalisia utaonekana katika vyombo husika.

*Kipengele cha Ukomo wa Uongozi!

"Hili nalitazama katika sehemu mbili;

Kwanza, kama ukomo ni kwa viongozi wote wa Nchi nzima katika nafasi mbalimbali, Mikoa hadi Kata, wapo viongozi wametumikia Chama kwa zaidi ya miaka 10 hadi 15 na Sheria zinatungwa, si kwa ajili ya Mwenyekiti na Katibu wake.

Pili, uamuzi wa ukomo na nani aongoze Taasisi kwa muda gani wanaamua wana-Taasisi kupitia vikao na kama inasemwa Mkutano Mkuu uliridhia, vinginevyo sijuiMsajili alikuwa na maana gani.Lakini si wakati muafaka wa kujiingiza katika malumbano yasiyokuwa na maana".

Kuhusu malalamiko kwa Viongozi kutotimiza majukumu ya Chama.

"Kuhusu jambo hili, watu wanaolalamika ni wasaliti kwa kuwa mambo ya Chama yanazungumzwa ndani ya vikao halali vya Chama. Kwa sasa ni wakati wa kwenda kwenye uchaguzi na mahasimu wanafanya mbinu mbalimbali kukidhoofisha Chama na ninataka kusema kuwa Chama kiko imara na hao wanaotaka kuleta chokochoko za kitoto na mambo ya kijinga, hawatakuwa na nafasi.

"Tumetoka hatua moja kwenda nyingine.Kwa muda mrefu tumekiimarisha Chama kwa gharama kubwa na tutakilinda Chama kwa gharama zote. Chama hiki kinaheshimu Katiba, kinapigania haki na ustawi wa Taifa la Tanzania.

"Hatutatetereka kwa watu wachache wanaotumika kwa mbinu mbalimbali eti kukipaka Chama matope ili Chama kiingie kwenye uchaguzi kikiwa kimejeruhiwa.Hatutaogopa Kikundi chochote kuichafua Chadema na tutapambana nacho".

Kuhusu UKAWA Kuzuia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Akizungumzia Kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyedai kwamba UKAWA wameuweka njia panda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Mhe.Mbowe alisema;
"Nashindwa kujua Waziri Mkuu alipozungumzia UKAWA na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa alikuwa akizungumza kwa namna ipi, nashindwa kumwelewa.

"Mabadiliko ya Sheria ambayo ni muhimu kufanyia marekebisho kabla ya Uchaguzi, hayafanywi na Bunge la Katiba, yanafanywa na Bunge la kawaida, kwa sasa hakuna Bunge na Bunge la kawaida linatarajiwa kukutana Novemba 4 mwaka huu, kipindi ambacho Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakuwa umeshapita.

"Kwa maana hiyo kuanzia sasa hadi Novemba 4, Bunge la kawaida halitakutana, labda kuwe na Bunge la dharura, sasa Waziri Mkuu anaposema kutorejea kwa wajumbe wa UKAWA katika Bunge la Katiba kutakwamisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ni kitu ambacho si cha Kweli hata kidogo.

"Serikali yenyewe imechelewa kuleta Muswada wa marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi kwa maksudi na imechelewa kurekebisha Kanuni za Uchaguzi na sasa inataka kuleta ama kutafuta kisingizio cha nini kinachelewesha na sasa imeamua kusingizia kuwa wajumbe wa UKAWA ndio watakaochelewesha Uchaguzi huo, hakika hatutaikubali danganya toto kama hii. Lakini ni vyema ikumbukwe kuwa, Uchaguzi na UKAWA ni vitu viwili tofauti kabisa kiuhalisia".

Alisema,
Mhe.Freeman Aikael Mbowe
Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani
Bungeni ambaye pia ni
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.
*****************
Tundu Antipus Lissu (Mb),
Dar Es Salaam,
Tanzania.
03/07/2014.
 
asante sana kwa taarifa kamanda
 
Mbona sioni cha maana zaidi ya malalamiko ya siku zote?
 
Wow! ama kweli Uongozi ni kipaji kutoka kwa Maanani pekee... I understand kwanini CCM wanaweweseka sana wakisikia kauli ya Mbowe...
 
Mkuu unaweza kupangilia vema ila wamesomeka vema makamanda
 
Hawa watu wanaotunga mbinu za kuidhoofisha CDM kwanini wasipewe pia kazi ya kutunga na kubuni njia mpya za kuongeza pato la Taifa maana inaonekana wanaumiza sana vichwa kubuni hizi mbinu, mimi nawashauri kwa sababu hawatafanikiwa kwa CDM basi wahamie kwenye kuimarisha uchumi.
 
Safi sana katiba ya zamani hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
 
Mkuu unaweza kupangilia vema ila wamesomeka vema makamanda
Cha kushukuru ni kwamba vyovyote itakavyokuwa jk alisema wakileta ujinga katiba ya zamani iko palepale.
 
Wakati Mwingine ni vema kushirikisha Ubongo unapoandika badala ya kuendeleza uliberali wa kujitekenya na kujichekesha mwenyewe...
Umeandika nini we mburula unatakiwa upate adhabu kama hii ili utulie.
 
Msimamo wa UKAWA kuhusu Bunge la Katiba.
"Wakati tunagomea Bunge la Katiba tulikuwa
na sababu za msingi na bado zipo,
hazijatatuliwa wala hazijafanyiwa Kazi, na kwa
kkuwa hazijatatuliwa, tutaendelea kubaki nje
ya Bunge.
"Lakini hatuwezi kurudi pale kwenda
kutukanana, kunyanyasana na kuvunjiana
heshima. Haileti maana kabisa, kitu ambacho
si malengo ya Bunge la Katiba.
"Msimamo wetu wa kususia Bunge la Katiba
si wa kudumu, unasababishwa na mazingira.
Watu wakae chini, watatue matatizo, na
yakimalizika watu watarejea Bungeni, lakini
kama hatukutatua, itakuwa kama watoto
wadogo wasiofanya taathmini wala kujua
athari ya kitu.
Kauli ya Mbowe kuhusu Kauli za Msajili wa
Vyama vya Siasa Jaji Mtungi.
*Sifa za kugombea tena!
Kuhusu nafasi zao kwenye vyama kuwa
hawana sifa na wanabanwa na Katiba kama
ilivyosema Ofisi ya Msajili wa vyama vya
Siasa, Mbowe aliiponda Kauli hiyo akisema
kuwa anaweza kuzungumza chochote na kwa
kuwa Msajili si mahakama, anaweza kutoa
tafsiri yake kwa mtazamo wake, lakini
uhalisia utaonekana katika vyombo husika.
*Kipengele cha Ukomo wa Uongozi!
"Hili nalitazama katika sehemu mbili;
Kwanza, kama ukomo ni kwa viongozi wote
wa Nchi nzima katika nafasi mbalimbali,
Mikoa hadi Kata, wapo viongozi wametumikia
Chama kwa zaidi ya miaka 10 hadi 15 na
Sheria zinatungwa, si kwa ajili ya Mwenyekiti
na Katibu wake.
Pili, uamuzi wa ukomo na nani aongoze
Taasisi kwa muda gani wanaamua wana-
Taasisi kupitia vikao na kama inasemwa
Mkutano Mkuu uliridhia, vinginevyo sijui
Msajili alikuwa na maana gani.
Lakini si wakati muafaka wa kujiingiza katika
malumbano yasiyokuwa na maana".
Kuhusu malalamiko kwa Viongozi kutotimiza
majukumu ya Chama.
"Kuhusu jambo hili, watu wanaolalamika ni
wasaliti kwa kuwa mambo ya Chama
yanazungumzwa ndani ya vikao halali vya
Chama. Kwa sasa ni wakati wa kwenda
kwenye uchaguzi na mahasimu wanafanya
mbinu mbalimbali kukidhoofisha Chama na
ninataka kusema kuwa Chama kiko imara na
hao wanaotaka kuleta chokochoko za kitoto
na mambo ya kijinga, hawatakuwa na nafasi.
"Tumetoka hatua moja kwenda nyingine.
Kwa muda mrefu tumekiimarisha Chama kwa
gharama kubwa na tutakilinda Chama kwa
gharama zote. Chama hiki kinaheshimu
Katiba, kinapigania haki na ustawi wa Taifa la
Tanzania.
"Hatutatetereka kwa watu wachache
wanaotumika kwa mbinu mbalimbali eti
kukipaka Chama matope ili Chama kiingie
kwenye uchaguzi kikiwa kimejeruhiwa.
Hatutaogopa Kikundi chochote kuichafua
Chadema na tutapambana nacho".
Kuhusu UKAWA Kuzuia Uchaguzi wa Serikali
za Mitaa.
Akizungumzia Kauli ya Waziri Mkuu Mizengo
Pinda aliyedai kwamba UKAWA wameuweka
njia panda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,
Mhe.Mbowe alisema;
"Nashindwa kujua Waziri Mkuu
alipozungumzia UKAWA na Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa alikuwa akizungumza kwa
namna ipi, nashindwa kumwelewa.
"Mabadiliko ya Sheria ambayo ni muhimu
kufanyia marekebisho kabla ya Uchaguzi,
hayafanywi na Bunge la Katiba, yanafanywa
na Bunge la kawaida, kwa sasa hakuna Bunge
na Bunge la kawaida linatarajiwa kukutana
Novemba 4 mwaka huu, kipindi ambacho
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakuwa
umeshapita.
"Kwa maana hiyo kuanzia sasa hadi Novemba
4, Bunge la kawaida halitakutana, labda kuwe
na Bunge la dharura, sasa Waziri Mkuu
anaposema kutorejea kwa wajumbe wa
UKAWA katika Bunge la Katiba kutakwamisha
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ni kitu
ambacho si cha Kweli hata kidogo.
"Serikali yenyewe imechelewa kuleta
Muswada wa marekebisho ya Sheria ya
Uchaguzi kwa maksudi na imechelewa
kurekebisha Kanuni za Uchaguzi na sasa
inataka kuleta ama kutafuta kisingizio cha
nini kinachelewesha na sasa imeamua
kusingizia kuwa wajumbe wa UKAWA ndio
watakaochelewesha Uchaguzi huo, hakika
hatutaikubali danganya toto kama hii.
Lakini ni vyema ikumbukwe kuwa, Uchaguzi
na UKAWA ni vitu viwili tofauti kabisa
kiuhalisia".
Alisema,
Mhe.Freeman Aikael Mbowe
Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani
Bungeni ambaye pia ni
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.
*****************
Tundu Antipus Lissu (Mb),
Dar Es Salaam,
Tanzania.
03/07/2014.
Majibu ya andiko lako haya hapa.
 
Inaonekana cdm na ukawa kwa ujumla hawataki katiba mpya. Jk vunja bunge la katiba tuendelee na katiba ya zamani tuone nan atakaye lalamika
 
Heko lissu! Heko kila mwanachadema hakuna kugeuka nyuma ni mashambuli kwa adui yetu namba one c.c.m hadi atapike kila alichotuibia sisi wana wa taifa hili.
 
Back
Top Bottom