Tundu Lissu, kwa hili, kachemka


Mzee zimmerman, hivi huo uislamu ulikuwepo kabla ya waarabu hawajafika Afrika?! Yaani unataka kusema kwamba hao Boko Haramu wanaona uislamu ndiyo dini ya asili yao?! Kwa hiyo ideas za kimashariki ya kati na mbali ndizo sawa na ideas za ancient Africa?! Hawa jamaa hivi wanaelewa kwamba waafrika walikuwa na imani zao; kwamba uislamu na ukristo zote ni imani ngeni zilizoletwa na wavamizi - wawe wamisionari ama wafanya biashara (waarabu na waasia)?!
 
Last edited by a moderator:
lisu yupo sahihi 100%,tatizo ni muungano hapo hakuna lingino,zanzibar ni taifa la kislam na wakristo ni wakuja,hivyo wanachoma makanisa ili kuwaondoa wabara wabaki na zanzibar yao,zanzibar komaeni mpaka kieleweke,hakuna ugaidi ukiwa unadai haki yako
 
Nakubaliana na mheshimiwa Lissu kwa asilimia zote. Amejibu kitaalam, pengine ndio maana wengine wanapata ugumu kuelewa. Labda swali moja linaweza kusaidia katika kumuelewa. Je, mtu yeyeto anaweza kutaja mahali na wakati ambapo paliwahi kuwa na kitu kinachoitwa uislamu safi, katika maana ya kuwa dini pekee bila mchanganyiko wowote ule? Tena Lissu akisema frustration yuko sahihi kwasababu frustration haina mantiki. Ukiuliza mbona wanachoma makanisa tu, jibu ni kwamba ndiyo asili ya frustrations, mtu mwenye akili tulivu haelewi kirahisi anachofanya a frustrated person. Even the other groups that may be referred in this connection, basically they are not for doing proselytism, but they reflect a certain kind of political disillusionment. Hapa dini ni terminus operis(object) na si terminus operantis(intention). Ahsante mheshimiwa Lissu.
 

Twende Taratibu Kiongozi.
Usiongee kwa namna ambayo inamaanisha kwamba sheria zetu ni kamilifu bila chembe ya mapungufu, moja ya mapungufu makubwa ya sheria zetu ni poor penetration kwenye jamii zetu, jamii zetu nyingi zinajiendesha bila ufahamu wa kuwapo kwa sheria, na serikali yetu haijawahi kuchukumua maamuzi ya dhati ya kupropagate sheria za nchi yetu ili ziweze kuwa enforced nchi nzima, vyombo vyetu vya usimamizi wa sheria vinavyanya kazi kwa kuvizia, sheria inaonekana kuwapo baada ya kosa kutokea, hata washitakiwa wengi kwenye mahakama zetu wanashitakiwa kwa mujibu wa sheria wasizozifahamu, kwa hiyo unaposema watu waishi kwa mujibu wa sheria nashindwa kukuelewa unamaanisha nini exactly?

Ukweli ni kwamba Jamii zetu zinaongozwa na mila na desturi fulani fulani, na kwa bahati mbaya sana sheria nyingi zilizopo sasa hazireflect mira na desturi hizi,na ni mila na desturi hizi ndio zimeweza kuzihifadhi jamii zetu katika mazingira ya amani ya utulivu mpaka kufikia sasa, kumbuka kwamba, Mwalimu Nyerere aliona matatizo yanayoweza kujitokeza katika jamii yetu kwa uwapo wa vikabila vingi vingi, ndio maana alitumia nguvu na uwezo wake wote kuhakikisha kwamba elimu ya kuwawezesha watanzania kuishi bila kubaguana kwa misingi ya ukabila, rangi na dini inaingia akilini mwa kila mtanzania, hakuna sheria na maandishi hayo hayawezi kuitwa sheria kwa mtazamo wa kibinaadamu ambayo yanawaelekeza binaadamu kuishi kwa amani na utulivu. ndio maana nikalazimika kufanya reference kwenye maandiko ya kwenye biblia kwa namna yanayohimiza wakisristo kuishi na watu wa jamii zingine.

Hivyo hili sio swala la kisheria, ni swala la mila na desturi, na katika hili narudia tena, tunalazimika kujitune na matakwa ya jamii ya kiislamu,sasa wewe unakuza mambo, unadai kuheshimu mila na desturi za kiislamu ni sawa na kuwa mtumwa kwa uislamu au waislamu, unasisitiza kuheshimu uhuru wa mtu mwingine bila kuvunja sheria, sina nia ya kukushambulia, lakini sina namna ingine ya kuelezea kwamba hii ni hurka ya ushindani usio na maana yoyote ile, nimekueleza kwamba sisi mtaani kwetu ilikuwa na taratibu zetu kwa kuku kuchinjwa na muislamu, msingi ni kwamba if possible nao waje tujumuike nao kwenye chakula, kinyume cha hapo ni kufanya maandalizi ya chakula katika namna ambayo unajuwa jirani yako hawezi kukitumia, kwa nini uweke vikwazo kwenye chakula?
 

Sawa mimi nitamtetea sababu ni wa chama changu, embu mlete huyo wa chama chako amung'unye tumsikie na wewe umtetee.

Tatizo lao ni kweli lahusu Muungano na wao wanaamini bila muungano wakristo wasingekuwepo na wao wanashambulia kiunganishi kimojawapo cha Muungano. ***** dot ukuda
 
mtoa hoja.. Thread n kilaza tuu.. Hukumuelewa komando lissu vizuri akakuacha njia panda.. Take care
 
%kubwa ya wazanzibar wazawa ni waislam, na wakristo wengi walioko zanzibar ni wahamiaji toka bara, kuwachomea makanisa, baa, nyumba ni ishara ya kuwafukuza warudi kwao bara, na yote hii inatokana na wazanzibari kutokuuhitaji muungano.

Hivi Enjo, kwa kumbukumbu zako ukristo na uislamu ni upi ulianza duniani? nia yangu ni kupima nani mvamizi, nani kati yao anajua maana ya IMANI!!!!
 

[MENTION]Mungi [/MENTION]kwa mara ya kwanza nimeanza kukuamini kuwa wewe ni great thinker.
 

Kwa kumkumbusha ourstory not history, ni kuwa IN THE BEGINING AFRIKA WAS CALLED ALKEBULAN- MEANS THE LAND OF THE BLACKS, kwa hili kuna sababu ya kuwahusudu wapagani kwani hawakulazimishi uelewa wao uwe wako pia hasa kwa maswala ya imani.
 
Last edited by a moderator:
hata mimi nakuunga mkono kwa asilimia 100 kwani busara alizotumia mh lissu ndiyo hiyo na hakuna nyingine

namuunga mkono lissu mnataka aseme halafu mpotoshe kama mlivyopotosha kauli ya mzee mtei.shame on you magamba
 
hivi wewe na elimu yako ya kuunga unga unaweza kumzidi tundu lisu? walikolalia ccm ndiko cdm walikoamkia.kwa nini itv hawakuita vyama vingine
 
Lissu alikua sahihi, japo wenzetu dini na siasa vinakwenda sambamba lakini lengo lao kuu la vurugu ni siasa kwa maslai ya dini..!lakini kaa ukijua wazanzibar wakilala wakiamuaka wanawaza uarabuni.!
 
Lisu yuko saws, uchomaji wa makanisa kunaueezekano mkubwa ikawa ccm wamefanya hivyo ili kuizima hoja ya kupinga muungano inayoongozwa na uamsho.
 
kisiasa yuko sahihi kabisa amesema kuokoa cdm, hasa nyakati hizi mbaya

kihalisia wale jamaa hawaupendi ukristo
 
Kwenye keyboard ya computer kila button ina kazi yake, wacha kutetea ujinga, wewe ndio mvivu wa kufahamu. Binafsi siwezi hata kupoteza muda wangu na kujiumiza macho kusoma thread ya namna hii isiyokuwa na mpangilio.

Kama hujaisoma mbona unachangia? bwana ee kama unaweza unaruhusiwa kuedit sio issue kuaibishana hapa.mi napita tu.
 
tuliza munkari bro na ondoa bias zako za u ccm utaelimika zaidi.
 
Zimmerman na Wana JF,
Ukweli siku zote Unauma, Kwa mimi sioni ubaya wa Tundu Lissu, alichoongea ni maoni na mawazo yake, tukubali tukatae kuna elements za ukweli, tukumbuke kwenye Hotuba yake kama Waziri Kivuli, wengi walimbeza kama sio kumpinga. Tatizo ninalilioona na naona Hasira za Wanzanzibar ni kunyimwa Haki ya kuhoji na kupiga kura ya Maoni kuhusu huu Muungano, walichopewa ni kutoa Maoni, na hawajui kama hayo Maoni yao yatafanyiwa kazi au la. Ikumbukwe Mkuu wa Kaya alishasema kwenye Katiba Mpya Muungano usiguswe, so naona kama kuna maswali mengi juu ya Muungano ambayo yanajificha nyuma ya Pazia. Kikubwa kinachonipa maswali ni kauli ya Serikali kukubali kulipa gharama zote za huaribifu wa mali huko ZNZ. Hata hotuba ya Rais ya mwisho wa mwezi ameongelea hilo.
My take: Kuna matatizo makubwa kufanya mambo nyuma ya Pazia, mambo yasiyofuata Sheria na Kanuni za Nchi na Katiba ya Nchi.
Nawakilisha




 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…