Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Kitandani hujabanduka
Siku, wiki hadi miezi,
Kichwani mawazo tele
Matarajio na mipango
Majeraha alokupa
Ni rahisi kukujibu
Japo sikukulenga shabaha
Damu yako nilimwaga
Damu mbichi ardhini
Tayari nimekutupa
Nyumba yako naikimbia
Dhabihu siitambui
Nikulilie hadharani?
Nikuimbie ushujaa?
Nikuombee kwa Mola?
Na talaka ugenini?
Kukulaki natamani
Na aibu naiona
Nini nikuzawadie
Walolia kuzomea?
Ajili yangu usilie
Juu yangu usinene
Nyumbani yamekwisha
Ajili yako urudi
Siku, wiki hadi miezi,
Kichwani mawazo tele
Matarajio na mipango
Majeraha alokupa
Ni rahisi kukujibu
Japo sikukulenga shabaha
Damu yako nilimwaga
Damu mbichi ardhini
Tayari nimekutupa
Nyumba yako naikimbia
Dhabihu siitambui
Nikulilie hadharani?
Nikuimbie ushujaa?
Nikuombee kwa Mola?
Na talaka ugenini?
Kukulaki natamani
Na aibu naiona
Nini nikuzawadie
Walolia kuzomea?
Ajili yangu usilie
Juu yangu usinene
Nyumbani yamekwisha
Ajili yako urudi