Tundu Lissu, kabla damu ya majeraha yako haijakauka ardhini...

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,210
2,000
Kitandani hujabanduka
Siku, wiki hadi miezi,
Kichwani mawazo tele
Matarajio na mipango

Majeraha alokupa
Ni rahisi kukujibu
Japo sikukulenga shabaha
Damu yako nilimwaga

Damu mbichi ardhini
Tayari nimekutupa
Nyumba yako naikimbia
Dhabihu siitambui

Nikulilie hadharani?
Nikuimbie ushujaa?
Nikuombee kwa Mola?
Na talaka ugenini?

Kukulaki natamani
Na aibu naiona
Nini nikuzawadie
Walolia kuzomea?

Ajili yangu usilie
Juu yangu usinene
Nyumbani yamekwisha
Ajili yako urudi
 

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
9,052
2,000
Aliyefanya mipango yote ya kumdhuru Lissu sijui anajisikiaje hivi sasa..

Damu yake haiwezi kupotea hivi hivi..

Aibu yako Pogba.
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,210
2,000
Okay, nimekusoma...
Ahsante Mkuu. Nina uhakika kwamba risasi alopigwa Lissu hazimuumi kama taarifa anazozipata kwamba wale aliodhani wako pamoja naye katika kuwapigania Watanzania sasa wanaikimbia nyumba yake wakati majeraha yake bado mabichi, na wataungana na wengine kumzomea siku akirudi nyumbani
 

Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
3,742
2,000
Katambi Katambi kwa dhihaka aliyomfanyia Lissu, eti anatoa press release ya kulaani waliompiga risasi Lissu kumbe ni unafiki tu. Dhambi hiyo itamtafuna hadi kizazi chake hata kama kwa usaliti huo atazawadiwa urais wa nchi. Hili jambo hata mimi linaniuma kuliko maelezo. kwa nini huyu katambi katambi alijitokeza kufanya hii dhihaka?
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,210
2,000
I will always pray for Tundu Lissu, huyu mwingine sina hata haja ya kumuombea
Mkuu, mimi nita pray for Lissu, but I think imefikia wakati naanza kuona akirudi nimwambie Lissu these Tanzanians are not worth fighting or even dying for. Go take care of yourself and family. From now on make your motto "Lissu First".

Kama wengi wa Tanzania wameamua they are fine with what is being dished out to them, then let them be. It is part of democracy to accept that. Community ikiamua kula kinyesi na ukafanya kila uwezalo kuwaambia ubaya wa kula kinyesi wakakuona wewe ndie hufai, basi acha waendelee kula kinyesi na isifike mahali ufe kwa ajili yao. May be one of these days they will wake up. For now lets just feel sorry for the few that have eyes and can see the the BS they are being fed in this country, and yet cant do anything about it because the majority of Tanzanians are hopelessly blind and enjoy living on BS..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom