Tundu Lissu hajawahi kunyamaza na hatonyamazishwa kamwe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
119,590
223,177
Naomba hii iwe angalizo kwa wote wanaodhani wanaweza kumnyamazisha Tundu Lissu. Ukifuatilia tangu awamu ya 3 huyu mtu alikuwa mwiba halisi kwa kuanika ukweli kuhusu wachimbaji waliozikwa kibabe tena wakiwa hai kwenye mashimo ya madini huko kanda ya ziwa ili kupisha mwekezaji, Mh. Lyatonga Mrema na IGP Mahita wanalifahamu hili vizuri sana.

Pamoja na vitisho vyote Lissu hakuwahi kumpigia magoti mtu yeyote na mwisho wa siku ukweli ulikuja kubainika, Mungu aziweke mahali pema peponi roho za wahanga wale, Amina.

Awamu ya nne ya Mh Profesa Kikwete makali ya Lissu ya kusimamia ukweli wote mnayafahamu, kuna wakati Dk Kikwete alinukuliwa akisema " NI HERI DR SLAA AENDE IKULU KULIKO TUNDU LISSU AINGIE BUNGENI " Dr slaa hakwenda ikulu lakini Tundu Lissu aliingia bungeni kwa kishindo.

Huyu mtu hanyamazishwi na wanadamu, atanyamaza pale tu Mungu atakapomtwaa kwa hiyari yake lakini si kwa hila za wanadamu wenye mwili na nyama.
 
Hawa polisi na tiss pamoja na dpp hebu wakutane na mwanasheria mkuu waone na kupima hizi kauli za Lissu kama kweli zina chembe ya kichochezi.

Wafanye hivyo wakiwa na fresh mind na ukada au biasness havitawafikisha kwenye usahihi wa hiki kinachoendelea leo. Wawe na free mind tufike pazuri. Vinginevyo waachane na akina Lissu ili tupate nafasi ya kusikia mengine ya maendeleo. Aachiwe ahubiri tu kwani hampigi yeyote ngumi.
 
Kama yeye ni mbabe, saa hizi yuko wapi? Hakuna mtu anayeweza kushindana na dola, hasa katika kipindi hiki. Hata kama una pembe ngumu namna gani ni lazima hizo pembe zitang'olewa na hatimaye utashika adabu tu.
 
Naomba hii iwe angalizo kwa wote wanaodhani wanaweza kumnyamazisha Tundu Lissu. Ukifuatilia tangu awamu ya 3 huyu mtu alikuwa mwiba halisi kwa uanika ukweli kuhusu wachimbaji waliozikwa kibabe huko kanda ya ziwa ili kupisha mwekezaji, Mh. Lyatonga Mrema na IGP Mahita wanalifahamu hili vizuri sana.

Pamoja na vitisho vyote Lissu hakuwahi kumpigia magoti mtu yeyote na mwisho wa siku ukweli ulikuja kubainika, Mungu aziweke mahali pema peponi roho za wahanga wale, Amina.

Awamu ya nne ya Mh Profesa Kikwete makali ya Lissu ya kusimamia ukweli wote mnayafahamu, kuna wakati Dk Kikwete alinukuliwa akisema " NI HERI DR SLAA AENDE IKULU KULIKO TUNDU LISSU AINGIE BUNGENI " Dr slaa hakwenda ikulu lakini Tundu Lissu aliingia bungeni kwa kishindo.

Huyu mtu hanyamazishwi na wanadamu, atanyamaza pale tu Mungu atakapomtwaa kwa hiyari yake lakini si kwa hila za wanadamu wenye mwili na nyama.
Kama Lisu ni shujaa arudishe ile list of shame kwenye tovuti ya Chadema
 
kuna mtu alikuwa anaongea na kusumbua serikali kama Dr. ulimboka???
 
Back
Top Bottom