gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 790
- 1,372
Mheshimiwa Tundu Lissu salaam sana ama baada ya salamu. Mimi ni shabiki wako namba moja pia ni mwanachama wa chama chetu pendwa cha CHADEMA.
Nakuandikia barua hii nikiomba upokee ushauri wangu kwamba ama ujiuzulu nafasi yako ya ubunge wa kuchaguliwa na wananchi na ubaki kuwa huru au ujitoe katika kinyang'anyiro cha uraisi wa TLS.
Mheshimiwa Lissu, ulichaguliwa na wananchi wa Singida Mashariki ili uweze kuwatumikia kwa moyo wako wote na kwa nguvu zako zote lakini badala yake hao umewasahau kabisa na sasa umeamua kujiingiza kwenye mambo mengine yanayo kupotezea muda na kukufanya usahau wananchi wako walio kuchagua.
Je, mheshimiwa unaweza kueleza ni kwa namna gani unaweza kujigawa kufanya kazi kwa pandezote tatu yaani Ubunge wa singida mashariki, uwanasheria wa chadema na mwisho uraisi wa TLS? Bila shaka ni lazima kuna nafasi moja hutoitendea haki kwa maana huwezi kuwa na muda wa kutosha kutekeleza yote haya.
Mheshimiwa Lissu, Pamoja na ushauri wote uliopewa na viongozi wakubwa wa nchi akiwemo Dokta Harisson Mwakyembe kwamba ili kuepusha chama cha sheria kuonekana kuwa kinavamiwa nawanasiasa ni vyema wewe ukajiepusha kujihusisha nacho lakini wewe uliendelea kukaidi na kuhisi kwamba unaonewa!
Mheshimiwa nilidhani kwamba ungejipima tu kuwa hufiti katika nafasi hiyo kwasababu tayari wewe unamaslahi na mrengo fulani wa siasa kwa hilo tu linakuondolea sifa. Ni vyema sasa ukajipima na kuamua kukaa pembeni kwa kuwa hata kama ukishinda kuwa kiongozi mkuu wa TLS bado maamuzi yoyote utakayo yatoa yatakuwa na vikwazo vingi pia yatahusishwa na mrengo wako wa kisiasa.
Mwisho kabisa naomba nikuombe mheshimiwa ujipime tena katika hilo na pia naomba utambue thamani kubwa na heshima ambayo wanachi wako wa Singida Mashariki wamekupa kuwa mwakilishi wao Bungeni. Watumikie wao kwa nguvu zako zote maana wakichukia mwaka 2020 watakupiga chini.
Wako mwaminifu
Gstar