Tundu lissu baki huko ulipo; maana watu wasiojulikana bado wapo na hawajulikani.

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
2,476
2,651
Wasalaam, nimestushwa na taarifa kwamba watu wasiojulikana wameibuka kwa speed ya 4G na kumteka kada wa chadema ndugu mdude na mpaka sasa hajulikani alipo japo tuna jeshi la police Tanzania. Ukiangalia sababu za kutekwa kijana huyo inasemekana ni misimamo yake na ukosoaji dhidi ya serikali ya wanyonge ya ccm. Huwa najiuliza ni kwanini watu wasiojulikana wamewalenga viongozi wa upinzani? Maana sijawahi kusikia wamemteka kada wa ccm zaidi ya kumtishia bunduki mh nape.

Mwisho napenda kumshauri kaka yangu mtanzania mwenzangu TL kubaki huko alipo maana wasiojulikana bado wapo na hawajulikani. Hivyo ataporudi bila shaka hawa wasiojulikana safari hii watampoteza kabisa na hakika hawatakosea km mwanzo, maana hata ndugu mdude waliwahi kumteka na kumtesa hadi kuwa mlemavu hapo mwaka Jana, na hapa jana wamerudi wamemteka tena sina hakika km tutamuona tena nahisi yatakua ya been saa8. Mungu atunusuru kwani hakuna alie salama ndani ya taifa huru.
 
Back
Top Bottom