Tundu Lissu atangaza rasmi Zitto Kabwe kuvuliwa uanachama wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.
dah kwa kweli ni pigo sana kwa upinzani Zitto alishaonyesha mshikamano wake na upinzani na sijuwi ilikuwaje Chadema wasikubaliane nimemzoea anajenga hoja za ukweli. Lakini naamini issue ya Escrow ndio iliyoweka pump asirudi tena bungeni kwa vyovyote vile - ccm ni hatari sana

If anything, Zitto alikuwa na bahati sana kulipata sakata la escrow na alijua ndiyo nafasi yake kujisafisha na kurudisha imani juu yake iliyokishapotea. Maamuzi ya CDM kumfuta uanachama yalishapitishwa siku nyingi hata kabla Zitto hajahusika kushughulikia sakata la escrow.Pia, katiba iko wazi kuhusu uanachama wa mwanachama anayekishtaki chama mahakamani.
 
Inawezekana kweli zitto kuomba msamaha kwenye chama......?

Mimi namlaumu sana zitto my brother, angejishusha mapema na kuomba msamaha haya yasingetokea kabisa.Tatizo sijui ni kujisahau au alidanganyika?

angeomba msamaha naamini chama kingemsamehe. Haya yametokea na jimbo tumelipoteza zitto tumempoteza inaniuma sana yaani anyaway lets look movie itaishia wapi?

Hivi mkuu wewe unaweza kuomba msamaha wakati huna kosa? Au kosa lake kuonyesha nia ya kumtoa dikteta MBOOwe? Hadi pale alipoambiwa kijana tumia busara? Ndio maana ya Demokrasia hiyo kwenye chama chenu?

mkuu hii haihitaji kamati kuu ukishapeleka chama mahakamani automatically utakuwa umejifukizisha chamani

Kumbe katiba mnafuata baadhi ya vipengele tu? Vipi uwepo wa m/kiti wa sasa hivi ndugu Dj MBOOwe kuongoza kwa muhula wa 3 huu? Huoni mpkm anaenda kinyume na katiba aliyoiapa kuwa atailinda na kuitetea? Tatizo lenu CHAGGADEMA mnaongozwa kwa hisia na HISIA na VISASI na si lolote lile.
 
Lissu hana ujasiri huo wa kumfukuza ZITTO kwenye ubunge.

Think Big young Man.. Hakuna mtu mwenye mamlaka kisiasa kuweza kumfukuza mwenzake bali katiba husika. Hivyo Lissu hana nguvu wala mamlaka ya kumfukuza Zitto isipokuwa sheria na katiba ya chama.
 
Zitto anatoa mchango mkubwa sana Bungeni, na mara zote anaibua hoja nzito zinazokuja kusaidia japo kujua wizi unaofanyika, cdm kama chama kingemshauri na kumrudisha kundini aendelee kuitumikia nchi, hii timua timua haisaidii lolote...
 
Yeah, Zito amepoteza kabisa trust ya CHADEMA. Lakini mimi napoifikiria zaidi nchi nahuzunika sana kwa uthibitisho unaozidi kujitokeza kwamba mahakama zetu ni za ovyo kabisa (kangaroo courts). Yaani siasa za kifisadi ndizo zinazoendesha mahakama; just like the Italian or Russian mafia! Zito alipewa kinga kubaki CHADEMA walipopenda "wenyewe". Leo hii kawaudhi, kinga inaondolewa chapchap, kisa?, amepoteza umuhimu! Ndugu zangu CHADEMA mngelifikiria hilo kwanza, msingepoteza muda kujitokeza kutangaza rasmi kumvua uanachama Zito; mngemuacha tu adondoke mwenyewe taratibu kwa kanuni zilizopo. Hii Tundu Lissu kujitokeza kutangaza, ni kama kuipa mahakama hadhi isiyostahili kabisa. Msipofushwe na kero moja pekee. Mngechukulia kwamba wote: Zito na mahakama ni uozo mtupu. Huo uamuzi wa mahakama umetolewa katika mazingira ya ovyo sana; si kitu ch kujivunia wala kuchangamkiwa na chama kama CHADEMA.

Pamoja na kwamba nilikuwa nafurahishwa na uwezo na ujasiri wa Zito katika kujituma kufuatilia mambo muhimu ya taifa, hivi leo sijali sana kama kapata shule au la kwani nimeona baadhi ya binadamu, kwa namna ya kushangaza sana, wako tayari kuchezewa na wahuni - bila sababu za msingi. Mfano wangu best ni mama Tibaijuka. Mtu una karama bora kabisa; kazi zako za halali zinakupa kipato cha kujidai lakini unaamua kuwaachia "watoto wa mjini" wakupapase na kukupeleka arijojo kwa ujira wa ziada wenye kamba na idhara kibao. Inaniwia vigumu sana kuelewa kwa nini mtu awe hivyo?

Shida yangu kuu na Uongozi wa CDM ni short term thinking stratergies zao. Yani ukiwafanyia tathmini, unaona kabisa hawa ni watu wanaoendeshwa kwa matukio,wasio na vision wala plan ya kuiongoza nchi.

Viongozi hawa wanasubiri iibuliew kashfa flani, ili waitishe maandamano nchi nzima, halafu wapigwe picha wakiwa kwenye landrover za polisi. Baada ya hapo, wakiwekwa lockup " makamanda" wengine waandamane kudai watolewe. wakitolewa wanaitisha press conference kushangilia kuwa makamanda wameshinda. Yani ni utoto upuuzi mwanzo mwisho.

Inasikitisha sana, kwani mwanzoni CDM walikuwa na substance flani, ila hiyo imepotea kama mshumaa unavyofifia kwenye upepo.

Kwa wasomaji wa historia, wanafahamu pia CHINA kulikuwa na mahasimu wakuu wa kuomintang na wakomunisti, hawa walipigana kwa muda mrefu, alipotokea adui wa kijapani, wakaweka kando tofauti zao, walivyo-mmaliza adui, wakarudi tena ulingoni. Wanahistoria wametoa ushuhuda kuwa bila hawa mahasimu wawili kuweka tofauti zao pembeni ingechukua miaka mingi sana kuwashinda wajapani, na labda wasingewashinda kabisa.

Masomo kama haya ya historia hayaingii kwenye vichwa vigumu vya wapinzani wa Tanzania, kwani wanaishi kwa "glory of the day". nasubiri makamanda kuandamana na kutoa matamko kuhusu ZITTO kufukuzwa. Baada ya hapo ukiwauliza "then what?" watabaki wanapepesa macho tu.

Nimewauliza viongozi wa CDM humu ndani si mara moja, bali mara kadhaa kuhusu mipango yao na dhamira zao za kutaka kuongoza nchi, hakuna majibu ya kueleweka. Kutafuta hizi taarifa kutoka CHADEMA ni sawa na kuuliza mshahara wa raisi wa jamhuri ya muungano. Unajua upo, na figures zipo, ila hakuna aliye tayari kuweka wazi. Ukijiuliza kwa faida ya nani?hupati majibu.

CHADEMA,kwa aina hii ya chuki za waziwazi zinazooneshwa na viongozi wenu kwa viongozi wengine na kuitana majina ya kebehi na kejeli mitandaoni na kwenye magazeti, mtaendelea kukosa kura nyingi za "level headed" Tanzanians,ambao pamoja na kuichoka CCM, hawaoni "substance" kutoka CHADEMA. Ofcourse, mnao wapiga kelele wa kutosha kujaza mikutano na kuendeleza soga mitandaoni, bila kusahau asilimia kubwa ya watanzania sio "confrontational" in nature. Ni aina ile ya watu wanaoomba chakula wakifika hotelini, baada ya kutoa pesa yao kununua. Sijui stratergists wenu ni kina nani? maana a simple "Know Your Voters" Analysis would have revealed the kinds of strategies that bears dividends, and this Lissu Chap is doing everything that is possibly wrong.
 
Yeah, Zito amepoteza kabisa trust ya CHADEMA. Lakini mimi napoifikiria zaidi nchi nahuzunika sana kwa uthibitisho unaozidi kujitokeza kwamba mahakama zetu ni za ovyo kabisa (kangaroo courts). Yaani siasa za kifisadi ndizo zinazoendesha mahakama; just like the Italian or Russian mafia! Zito alipewa kinga kubaki CHADEMA walipopenda "wenyewe". Leo hii kawaudhi, kinga inaondolewa chapchap, kisa?, amepoteza umuhimu! Ndugu zangu CHADEMA mngelifikiria hilo kwanza, msingepoteza muda kujitokeza kutangaza rasmi kumvua uanachama Zito; mngemuacha tu adondoke mwenyewe taratibu kwa kanuni zilizopo. Hii Tundu Lissu kujitokeza kutangaza, ni kama kuipa mahakama hadhi isiyostahili kabisa. Msipofushwe na kero moja pekee. Mngechukulia kwamba wote: Zito na mahakama ni uozo mtupu. Huo uamuzi wa mahakama umetolewa katika mazingira ya ovyo sana; si kitu ch kujivunia wala kuchangamkiwa na chama kama CHADEMA.

Pamoja na kwamba nilikuwa nafurahishwa na uwezo na ujasiri wa Zito katika kujituma kufuatilia mambo muhimu ya taifa, hivi leo sijali sana kama kapata shule au la kwani nimeona baadhi ya binadamu, kwa namna ya kushangaza sana, wako tayari kuchezewa na wahuni - bila sababu za msingi. Mfano wangu best ni mama Tibaijuka. Mtu una karama bora kabisa; kazi zako za halali zinakupa kipato cha kujidai lakini unaamua kuwaachia "watoto wa mjini" wakupapase na kukupeleka arijojo kwa ujira wa ziada wenye kamba na idhara kibao. Inaniwia vigumu sana kuelewa kwa nini mtu awe hivyo?
Tatizo maamuzi ya hiki chama yamejaa mhemko usio na Faida kwa chama bora japo wangekuwa na subira wakasoma hata sura za watu kabla ya kuja na matamko yasiyo na tija kwa jamii.
 
Zito alishapanga kuchomoka CDM mwisho wa mwezi huu! CDM ni kama wamemuwahi vile! Strategically, endapo Zito angeiwahi CDM na kujiuzulu uanachama wa CDM, angekuwa na upper hand na angekuwa na wigo mpana wa kuisulubu CDM ki-propaganda huko anakokwenda.

It is for this reason CDM wameamua kumuwahi Zito ili ku-neutralize sumu yake mapema.
 
Hivi mkuu wewe unaweza kuomba msamaha wakati huna kosa? Au kosa lake kuonyesha nia ya kumtoa dikteta MBOOwe? Hadi pale alipoambiwa kijana tumia busara? Ndio maana ya Demokrasia hiyo kwenye chama chenu?

Kumbe katiba mnafuata baadhi ya vipengele tu? Vipi uwepo wa m/kiti wa sasa hivi ndugu Dj MBOOwe kuongoza kwa muhula wa 3 huu? Huoni mpkm anaenda kinyume na katiba aliyoiapa kuwa atailinda na kuitetea? Tatizo lenu CHAGGADEMA mnaongozwa kwa hisia na HISIA na VISASI na si lolote lile.
Sasa mkimpa funguo za magogoni si mtakuwa mnaandaa identical twin ya Mugabe?????
 
Tunasikitika kumpoteza mpiganaji zitto bungeni maana mchango wake n mkubwa sana lakini tatizo la undumilakuwili alilonalo ni bora afukuzwe tu...

ni bora angekuwa amekufa kabisa watu wanajua WAMPOTEZA MPIGANAJI KIKWELII lakini kuasi chama na kuendelea kubakia ndani ya CHADEMA HIO NI HATARI ZAIDI KWA USALAMA WA CHADEMA.

Zito kutangazwa sio mwnachama tena wa CDM hio ni sauti sahihi kuisikia pa wapenda mabadiliko ya kweli.

Kwa wanafiki kwao itakuwa ni chukizo.
 
Zitto alishaonywa sana lakini hakusikia.
Nakumbuka mapokezi tuliyompa alipofukuzwa bungeni kwa issue ya buzwagi.Nakumbuka hamasa ilivyokuwa juu.
Lakini ngazi hiyohiyo aliyopandia ndio hiyohiyo aliyoshukia!
Alipata umaarufu kupitia Buzwagi scandel,na umaarufu ukamjengea kiburi ambacho na hamu ya mkwanja alioanza kuupata kupitia tume ya rais.
Inauma sana lakini anastahili pia.
 
Mimi narudia mwisho wa chadema ni uchaguzi wa mwaka huu. Iki chama kitapotea hamtaamini. nilikipenda sana iki chama lkn kwa upuuzi huu basi. mtu kuomba kugombea u/kt kosa? haya mengine yooote ni uzushi mtupu.sababu kuu ndo hiyo. Yamesemwa mengi ya Mboe mbona kimya? Silaa vp kujikopesha Ruzuku ya chama mbona hayo hayasemwi?

nijuavyo mm ilikufa tokea mwaka jana.
kwa taarifa yako chadema itazidi kupaa,hata isiposhinda urais itachukua majimbo kibao na udiwani.
 
Mimi narudia mwisho wa chadema ni uchaguzi wa mwaka huu. Iki chama kitapotea hamtaamini. nilikipenda sana iki chama lkn kwa upuuzi huu basi. mtu kuomba kugombea u/kt kosa? haya mengine yooote ni uzushi mtupu.sababu kuu ndo hiyo. Yamesemwa mengi ya Mboe mbona kimya? Silaa vp kujikopesha Ruzuku ya chama mbona hayo hayasemwi?

Huna lolote...unaabudu watu...Chama kwanza...
 
Kwa upande wake Zitto Kabwe amesema hawakuwa na wito wa mahakamani leo na Jaji wa kesi kahamishiwa Tabora na hawana taarifa ya Jaji Mpya, pia kaongeza kuwa Mwanasheria anafuatilia na atatoa statement.:flypig:
Zito kachanganyikiwa..anataka tuamini kuwa jaji wake angekuwepo angeshinda kesi.sio mbaya bado miezi minne tu bunge livunjwe.ila jamaa wamemuadhiri
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom