WanaJF,
Baada ya polisi kumaliza mahojiano na wahariri wa gazeti la Mawio na kuwaachia huru, sasa jeshi hilo linaelekeza nguvu zake kwa Lissu, ambae inasemekana yeye (Lissu) ndio chanzo cha habari za uchochezi zilizo pelekea gazeti hilo kufutwa na waziri mwenye dhamana na habari, ndugu Nape.
Katika mahojiano ambayo jeshi la polisi limefanya na wahariri wa gazeti la Mawio, jeshi limebaini kuwa mtu ambae ametajwa mara zote na wahariri hao kuwa chanzo cha habari ya kizushi iliyopewa kichwa cha habari, "Zanzibar Pawaka" ni Tundu Lissu. Habari zinasema kuwa tayari jeshi hilo linae Tundu Lissu katika himaya yao tayari kwa ajili ya mahojiano na mwanasheria huyo wa CHADEMA na mbunge.
Aidha, Jeshi la polisi pamoja na mambo mengine, limejipanga kukomesha tabia ya kueneza habari za uzushi na kushughulikia mtu yeyote anayeeneza uzushi ambao utapelekea uvunjifu wa amani bila ya kujali nyadhifa ya mtu huyo au umaarufu wake kwenye jamii.
======
Chanzo: Mwananchi

Wahariri wa Mawio wachiwa, Lissu kuhojiwa leo
Kwa ufupi
Waliachiwa jana saa 6.40mchana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili kila mmoja ambao walisaini hati ya Sh20milioni.
Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam jana imewaachia kwa dhamana Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, Jabir Idrissa baada ya kuwashikilia tangu juzi.
Wakati wahariri hao wakiachiwa, imeelezwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ametakiwa kufika polisi leo kwa mahojiano dhidi ya tuhuma zinazowakabili Mkina na Idrissa. Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na wakili wa kujitegemea, Peter Kibatala wamesema Lisu anatarajia kuhojiwa leo na polisi.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alipoulizwa kuitwa kwa Lissu alisema hana taarifa hizo lakini Lissu mwenyewe alisema ameitwa na kwamba leo mchana atakwenda. Mkina na Idrisa walijisalimisha juzi mchana katika Kituo cha Polisi cha Kati baada ya kutakiwa kufanya hivyo kwa madai ya kuandika habari za uchochezi ambako walihojiwa kwa saa nane. Waliachiwa jana saa 6.40mchana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili kila mmoja ambao walisaini hati ya Sh20milioni.
Wadhamini hao ni Robert Katula, Michael Sarungi na Josephat Isango. Wakili wa wahariri hao, Peter Kibatala alisema ni busara kuwapa muda polisi kufanya uchunguzi.
Mkina alisema wamehojiwa na wametakiwa kuripoti kituoni hapo kila siku saa mbili asubuhi hadi hapo kesi yao itakapoisha. Idrissa alisema baada ya kujisalimisha, askari walianza kumhoji kuhusiana na habari iliyoandikwa katika gazeti la Mawio yenye kichwa cha habari Machafuko yaja Zanzibar.
Chanzo: Mwananchi