Tundu Lissu aituhumu serikali kuminya Mawakili nchini

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,733
239,352
Hayo yalisemwa bungeni na Mh Tundu Lissu ambaye ni waziri kivuli wa wizara ya sheria na katiba.

Kwamba Muswada wa sheria ya msaada wa kisheria uliowasilishwa bungeni jana na Mh Mwakyembe umelenga kudhibiti wanaotoa msaada wa kisheria kwa watanzania Masikini .

Alisema muswada huo unaweka udhibiti wa kuzitaka taasisi zinazotoa misaada ya kisheria kuomba usajili upya huku tayari wakiwa wanatoa huduma mahakamani .

" Hawa mawakili wanaofanya kazi sasa hivi sio makanjanja kama anavyosema waziri , maana ili uingie mahakamani unapaswa kuwa mwanataaluma uliyethibitishwa "

Chanzo - Mwananchi .

Dua yangu - Mungu mbariki Tundu Lissu .
 
Hivi huyu jamaa hana akili au huwa anajitoa ufahamu? Yaani hajui hadi mtu anakuwa Wakili anapitia ngazi zipi? Halafu TLS wakikaa kimya nitwashangaa sana. Au alikuwa anamaansha wale "Paralegal" ambao hata yeye anajua kabisa kwamba kwa tafsiri yoyote ile hawawezi kuitwa mawakili.
 
Ni yale yale ya kuwataka madereva kwenda kusoma upya na kupewa vyeti vipya.
Kuna taasisi zitafungwa kwa kutotimiza vigezo hapo.

Wale wanaoitwa Haki za Binadamu wakae chonjo....
 
Tanzania Gizaaaa Serikal hii ya Awamu ya Tano inafanya vitu bila kutafakari mwisho wa siku wanashindwa kuwa na ushawishi na hoja ktk ufinyu wa Miswaada wanayoileta hakika hii ni kukosa kufikil kabla ya kutenda na kama Wana nia ya kukandamiza uhuru wa Sheria Nchini wamechelewa kwani tuko Macho kuliko wanavyofikiria.
 
Swali - Hivi ni kweli Waziri wa sheria hajui kwamba Mawakili kabla ya kuanza kazi hiyo wanathibishwa kitaaluma ?

Anajua sana ila sasa anataka wakadhibitishwe kisiasa. Lazima wawe wanaweza kujipendekeza kwa serekali. Yaani sasa wafahamu kuna sheria za kutoka juu hivyo wasikomae sana maana hawana watakalofanya pindi sheria za kutoka juu zikitamalaki.
 
Jamani hapa kuna mambo mawili. Moja jamaa keshawatisha sana kiasi ambacho akisema tu fanya hivi wanafanya bila kufanya reference kwenye profession. Pili wanafanya makusudi kumharibia ili aonekane hafai. Yote haya yanayohusu negative impact kwenye hatima ya assessment ya wananchi juu ya utawala wake. Tuombe sana Mungu wa mbinguni atusaidie
 
Tanzania Gizaaaa Serikal hii ya Awamu ya Tano inafanya vitu bila kutafakari mwisho wa siku wanashindwa kuwa na ushawishi na hoja ktk ufinyu wa Miswaada wanayoileta hakika hii ni kukosa kufikil kabla ya kutenda na kama Wana nia ya kukandamiza uhuru wa Sheria Nchini wamechelewa kwani tuko Macho kuliko wanavyofikiria.
Unajua viongozi wa ccm wanaamini ni wao tu wenye akili kuliko watanzania wote hawa .
 
Ndio maana wameondoa Bunge Live,ili hawa Wasomi wa hovyo hovyo wanaojiita madaktari wa sheria wasionekane mubashara wakiongea pumba.

Tangu lini toka kuundwa kwa Taifa hili mahakama zilipokea mawakili "makanjanja"?
Yaani leo Dr Mwakyembe anawaita "learned brothers" kuwa ni mkanjanja?

Katika fani ambayo nchi hii zilizjisimamia ili kuwa na watu wenye uweledi wa kiwango cha juu,basi ni Sheria,Udaktari na Uhandisi.

Kinachofanyika sasa,serikali inaweka utaratibu wa hizi Taasisi za Kisheria kupata leseni toka wizara ya Katiba na Sheria,taasisi kama TAWLA,TAMWA na Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu cha kina Mama Kijo Bisimba vitatakiwa kujisajili upya.

Hapo ndio vitakutana na masharti ambayo yatavifanya vishindwe kabisa kuikosoaa serikali hata pale inapokiuka haki za binadamu.

Tundu Lissu alisema...UKUTA si kwa ajili ya UKAWA,bali kwa ajili ya Watanzania wote.Wakimaliza kwa UKAWA watakuja kwa wanasiasa nje ya UKAWA,watakuja kwa waandishi,watahamia kwa wanafunzi wa vyuo,baadae kwa wafanyakazi kutokupanda vyeo wala mishahara ili hali nchi nzima kanzi-data ya wafanyakazi wa umma ni 500,000,sasa unahakiki "ghost workers" wa idadi hiyo kwa miaka miwili?

Wakihama kwa makundi hayo,sasa wamekuja kwa mawakili,watakuja kwa machinga na mwisho wa siku hakuna atakayebaki.

Yule "nduli" wa Ujerumani alianza kuuwa Wayahudi,wengine wakakaa kimya,akafuata kwa wanasiasa,wengine wakakaa kimya,akaja kwa wapinzani wake ndani ya serikali,watu kimyaaa,akahamia kaa viongozi wa dini,watu kimyaa!!Wakati wanafikiwa tabaka la chini..hakukuwa na mtu wa kutoa msaada,maana wote waliotakiwa kusaidia walikuwa wametangulia "kusulubiwa"...,

Hii ya kubana mpaka NGO za Kisheria...Ni aina nyingine ya dalili mbaya za Utawala wa kisheria.
 
Swali - Hivi ni kweli Waziri wa sheria hajui kwamba Mawakili kabla ya kuanza kazi hiyo wanathibishwa kitaaluma ?
Waziri ana mambo yake binafsi, mawakili hata baada ya kuanza kazi wana kamati zinazoshughulika na nidhamu yao..hizi zipo kisheria.

Pia kuna Rules of Professional Conduct and Etiquette hizi zimemzuia wakili kufanya ukanjanja wowote na kama akifanya ndio atapelekwa huko kwenye vyombo vya kinidhamu.

Huu ni muendelezo wa kutaka kuishushia hadhi UDSM.
 
Hata wale mawakili ambao sio wasomi nao wanathibitishwa kitaaluma? maana hapa JF kuna mawakili wasomi na sio wasomi according to Bavicha vichwa panzi mix kuku.
 
Ndio maana wameondoa Bunge Live,ili hawa Wasomi wa hovyo hovyo wanaojiita madaktari wa sheria wasionekane mubashara wakiongea pumba.

Tangu lini toka kuundwa kwa Taifa hili mahakama zilipokea mawakili "makanjanja"?
Yaani leo Dr Mwakyembe anawaita "learned brothers" kuwa ni mkanjanja?

Katika fani ambayo nchi hii zilizjisimamia ili kuwa na watu wenye uweledi wa kiwango cha juu,basi ni Sheria,Udaktari na Uhandisi.

Kinachofanyika sasa,serikali inaweka utaratibu wa hizi Taasisi za Kisheria kupata leseni toka wizara ya Katiba na Sheria,taasisi kama TAWLA,TAMWA na Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu cha kina Mama Kijo Bisimba vitatakiwa kujisajili upya.

Hapo ndio vitakutana na masharti ambayo yatavifanya vishindwe kabisa kuikosoaa serikali hata pale inapokiuka haki za binadamu.

Tundu Lissu alisema...UKUTA si kwa ajili ya UKAWA,bali kwa ajili ya Watanzania wote.Wakimaliza kwa UKAWA watakuja kwa wanasiasa nje ya UKAWA,watakuja kwa waandishi,watahamia kwa wanafunzi wa vyuo,baadae kwa wafanyakazi kutokupanda vyeo wala mishahara ili hali nchi nzima kanzi-data ya wafanyakazi wa umma ni 500,000,sasa unahakiki "ghost workers" wa idadi hiyo kwa miaka miwili?

Wakihama kwa makundi hayo,sasa wamekuja kwa mawakili,watakuja kwa machinga na mwisho wa siku hakuna atakayebaki.

Yule "nduli" wa Ujerumani alianza kuuwa Wayahudi,wengine wakakaa kimya,akafuata kwa wanasiasa,wengine wakakaa kimya,akaja kwa wapinzani wake ndani ya serikali,watu kimyaaa,akahamia kaa viongozi wa dini,watu kimyaa!!Wakati wanafikiwa tabaka la chini..hakukuwa na mtu wa kutoa msaada,maana wote waliotakiwa kusaidia walikuwa wametangulia "kusulubiwa"...,

Hii ya kubana mpaka NGO za Kisheria...Ni aina nyingine ya dalili mbaya za Utawala wa kisheria.
Mungu akulinde sana mkuu , waziri wa sheria na mimi tunatoka jimbo moja , naomba nikiri hadharani kwamba NAONA AIBU SANA KUJTAMBULISHA HADHARANI KWAMBA NATOKA KYELA .
 
Waziri ana mambo yake binafsi, mawakili hata baada ya kuanza kazi wana kamati zinazoshughulika na nidhamu yao..hizi zipo kisheria.

Pia kuna Rules of Professional Conduct and Etiquette hizi zimemzuia wakili kufanya ukanjanja wowote na kama akifanya ndio atapelekwa huko kwenye vyombo vya kinidhamu.

Huu ni muendelezo wa kutaka kuishushia hadhi UDSM.
Hivi Mwakyembe anadhani atakuwa waziri kwa miaka mingapi ?
 
Hayo yalisemwa bungeni na Mh Tundu Lissu ambaye ni waziri kivuli wa wizara ya sheria na katiba.

Kwamba Muswada wa sheria ya msaada wa kisheria uliowasilishwa bungeni jana na Mh Mwakyembe umelenga kudhibiti wanaotoa msaada wa kisheria kwa watanzania Masikini .

Alisema muswada huo unaweka udhibiti wa kuzitaka taasisi zinazotoa misaada ya kisheria kuomba usajili upya huku tayari wakiwa wanatoa huduma mahakamani .

" Hawa mawakili wanaofanya kazi sasa hivi sio makanjanja kama anavyosema waziri , maana ili uingie mahakamani unapaswa kuwa mwanataaluma uliyethibitishwa "

Chanzo - Mwananchi .

Dua yangu - Mungu mbariki Tundu Lissu .
Huyo Kichaa Uchwara hajui asemacho.
 
Nashindwa kuelewa kabisa huyu Waziri wa katiba na Sheria bado tuna safari ndefu sana huu nimesikitishwa sana hii kauli sijui kama kabla ya kupeleka hayo bungeni huwa hawajadiliani?
 
Back
Top Bottom