ChekoFagia
Senior Member
- Sep 20, 2025
- 115
- 339
Kampeni iliyoanzishwa na wanachama na wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na na Maendeleo (CHADEMA) ya kumchangia Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu ambaye amekuwa kizuizini kwa zaidi ya siku 250 imeendelea kushika kasi na zaidi ya shilingi million 17 imechangwa ndani kwa siku Moja.
Kampeni hiyo iliyopewa jina la "Funga Mwaka na Tundu Lissu" ilianzishwa kwa lengo la kuchangisha fedha takribani shilingi milioni 20 ndani ya masaa 48.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na waanzilishi wa kampeni hiyo akiwemo Edson Mwakalebela(Sativa) na Godilisten Malisa wamthibitisha kupatikana kwa kiasi hicho cha fedha ambazo zimekuwa zikiwekwa katika akaunti za kaka wa Lissu Alute Mughwai Lissu.
Waendeshaji wa michango hiyo wameeleza fedha hizo ni ili kuinysha upendo na kumuunga mkono Lissu lakini pia kuiwezesha familia na wale waoweza kumfikia Lissu gerezani wasikwame kokote katika kumhudumia Lissu.
Godilisten Malisa ameandika “Jana GenZ walipotuambia wanataka kumchangia Lissu 20M kwa masaa 48 tuliona kama wanafanya mzaha. Lakini tukawakubalia. Tukasema hata isipotimia ndani ya masaa 48 basi tutaongeza muda. Tukaongea na mzee Alute (kaka yake Lissu) ili akubali ombi la GenZ apokee michango. Sasa hata masaa 24 hayajaisha tayari mzigo ushasoma 17M. Aisee nimewavulia kofi”.