Tundu katika kuta za chini za moyo (ventricular septal defect) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu katika kuta za chini za moyo (ventricular septal defect)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Oct 4, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280


  [​IMG]

  Makala ya leo ni muendelezo wa magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo, na ugonjwa wa leo hujulikana kama Tundu katika moyo, au Tundu katika kuta za ventrikali za moyo, ni ugonjwa ambao hutokea mara nyingi zaidi.


  Watoto wenye tundu dogo katika moyo, huweza kukua bila matatizo yoyote, wakati wale wenye tundu kubwa huanza kuonesha dalili mapema.


  Vifuatavyo ni vihatarishi ambavyo vinaweza kupelekea kupata tundu katika kuta za chini za moyo


  • Maambukizi ya Rubella katika kipindi cha ujauzito
  • Ugonjwa wa kisukari ambao haujadhibitiwa kwa mama mjamzito
  • Matumizi ya pombe au madawa ya kulevya na baadhi ya dawa za hospitali katika kipindi cha ujauzito
  Dalili

  • Rangi ya ngozi, midomo na kucha hubadilika na kuwa bluu
  • Kunyonya au kula kwa shida sana, na ukuaji wa shida
  • Kupumua kwa shida
  • Kuchoka haraka
  • Kujaa miguu na kuvimba tumbo
  • Mapigo ya moyo ya haraka
  • Kwa mtaalamu anaweza kusikia ishara ya ongezeko la sauti ya ziada ya mapigo ya moyo ya mtoto hali ambayo wataalamu huiita holosystolic murmur kwa kutumia kifaa kitaalamu stethoscope
  Madhara ambayo yanaweza kutokana na Tundu katika kuta za chini za moyo

  • [​IMG]Eisenmenger syndrome: Ni hali inayotokea wakati shanti ya damu kutoka kushoto kwenda kulia inayotokana na tundu katika kuta za moyo huongeza mtiririko wa damu katika mishipa ya kwenye mapafu na kusababisha shinikizo la damu katika mapafu. Hali hii husababisha kuongezeka kwa shinikizo katika upande wa kulia wa moyo, na kusababisha kubadilika kwa shanti kutoka kulia kwenda kushoto. Matokeo yake ni kuwa damu isiyo na oksijeni ambayo ilitakiwa kwenda kwenye mapafu kwa ajili ya kusafishwa, huchanganyika na damu yenye oksijeni iliyoko upande wa kushoto na kusambaa mwilini.
  • Kiharusi
  • Maambukizi katika kuta za ndani za moyo (endocarditis)
  • Moyo kushindwa kufanya kazi vizuri
  Ujauzito na Tundu katika kuta za chini za moyo
  Kwa akina mama ambao wamezaliwa na tatizo hili, ambao walitibiwa bila madhara yoyote wanaweza kushika ujauzito bila kupata madhara yoyote kipindi cha ujauzito. Isipokuwa, wale ambao hawakutibiwa au ambao wameshapata madhara, hushauriwa kutoshika ujauzito kwa sababu ya hatari zinazoweza kutokea kipindi cha ujauzito.
  Vilevile kwa akina mama waliozaliwa na tatizo hili, uwezekano wa watoto wao kuzaliwa na tatizo hili huwa mkubwa. Kwa mujibu wa taarifa za taasisi ya moyo ya Marekani hatari ya kupata tatizo hili kwa mtoto huongezeka kwa kati ya asilimia 2 hadi 20 iwapo atazaliwa na mama mwenye ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa nao.
  Vipimo

  • X-ray ya Kifua
  • ECG
  • Echocardiogram
  • Cardiac catheterization
  • Pulse Oximetry
  Matibabu

  • Wengi wa wagonjwa wa tatizo hili huwa hawahitaji matibabu ya aina yeyote ile kwa vile tatizo hili hujirekebisha katika miaka ya mwanzo ya maisha yao. Hata hivyo kwa wale ambao watahitaji matibabu, hutibiwa kwa tiba au upasuaji kutegemea na ukubwa wa tatizo lenyewe.
  • Tiba huhusisha dawa zifuatazo:
   • ACEI¬ís ambazo hupunguza kazi ya moyo
   • Cardiac glycosides ambayo huongeza nguvu ya mapigo ya moyo
   • Diuretics ambazo pia hupunguza kazi ya moyo kwa kupunguza maji mwilini
  • Utaratibu wa kuziba tundu umegawanyika katika sehemu mbili, na hufanyika iwapo tundu ni kubwa sana, au tundu halikujirekebisha lenyewe wakati mtoto anapokua, au dawa alizopewa mgonjwa hazikusaidia.
   • Upasuaji - ambapo kifua hufunguliwa kuziba tundu
   • Catheter - ambapo mrija hupitishwa katika mshipa wa damu kufikia sehemu tatizo lilipo kwenye moyo na kuliziba kwa kutumia kifaa maalumu. Katika njia hii, huwa hakuna haja ya kufanya upasuaji wa kufungua kifua cha mgonjwa. Tundu Katika Kuta za Chini za Moyo (Ventricular Septal Defect)

   
 2. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,863
  Likes Received: 3,307
  Trophy Points: 280
  Some times huwa nasikia kitu kama kichomi sehemu za chini ya moyo wangu hadi nitulie na nisigeuke upande wowote kama dakika kadhaa hivi na nikipumua kichomi kinauma hadi nishike eneo la moyo tena kwa kuukandamiza hutulia ... nilishawahi enda kwa Pharmacist akaniambia sio moyo ni uchovu sana wa kazi bila mapumziko akanipa dawa fulani japo hazikusaidia sana na tatizo linajirudia kila baada ya kitu kama mwaka na limeanza kunitokea kama miaka saba iliyopita ila ndio vile once a year... je hili ni tatizo la Moyo au?
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mlaleo Nenda hospitali Kuu ya Muhimbili huko kuna Wataalamu huko wanaweza kukuchunguza zaidi ili wapate kujuwa nini chanzo chake usibahatishe kupata ushauri humu ndani.
   
Loading...