"Tundu Antiphas Lissu, live muda huu Startv"

"Tundu Antiphas Lissu, live muda huu Startv"

buhange

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2011
Posts
505
Reaction score
110
Kamanda Lissu ni mgeni mwalikwa muda huu STAR TV, Ktk kipindi cha MEDANI YA SIASA NA UCHUMI
 
Kamanda Lissu ni mgeni mwalikwa muda huu STAR TV, Ktk kipindi cha MEDANI YA SIASA NA UCHUMI
Naona mwendesha mjadala anajionesha kuwa ki-magamba magamba vile maana jinsi anavyoikomalia chadema si kawaida. Hata hivyo amezidiwa sana na Mh. Lissu yaani kwa ufupi siyo level yake kabisa. Nimeudhika jinsi alivyoshindwa hata kutaja RED BRIGADE (Mwandishi gani huyu wakuu??). Fani hii ilishavamiwa na makanjanja!!
 
Huyu dada ananifurahisha kujiamini kwake anajaribu kuuliza maswali magumu. Lissu Angekuwa mtu dhaifu angegalagazwa n huyu mdada. Mwiteni gamba yeyote uone kama hatakimbia studio
 
Namchek kamanda Lisu. Anajua sana huyu jamaa
 
Kwa Lisu mbona! nadhani maswali yataisha,then kipindi kitaisha ghafla,kikiendelea maswali yatakuwa yanajirudia
 
Ukihitaji kushinda Urais huhitaji kura za Zanzibar- Tundu Lissu
 
"ukitaka kushinda uchaguzi zanzibar is not a factor" kauli ya mh. Lissu, anasema hakuna sababu ya CDM kujilaumu eti haikubaliki zanzibar kwa sababu kuru zote zanzibar hazizidi hata laki 5 wakati jimbo la Ubungo peke yake lina zaidi ya kura laki 4 na 32 elfu, so Vision of competition ni kila kitu kuipeleka CDM mbele
 
"Siasa ya tanzania inatawaliwa na ushamba" watu wengne hufikilia eti kutoka nje ya bunge ni dhambi ambayo haijawahi kutokea duniani, mbona mabunge mengne watu wanapigana?" kauli ya mh. LISSU
 
"Michango inayoendeshwa na serikali ni UPUUZI, Eti michango ya mwenge, mtoto wa afrika, mchango wa maendeleo n.k". Michango inachangshwa bila mwisho wa siku kutoa taarifa ya nini kimefanyika juu ya michango hiyo, badala yake wajanja wachache kujinufaisha". Kauli ya Mh. Lissu ktk ugeni wake Star TV
 
"Michango inayofanyika kwa sasa ktk nchi yetu ni wizi" maana tayari tuna kodi zinazotozwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo
 
Nimefurahi sana hapa aliposema kuwa viongozi waserikali wanapenda kusema kua nchi hii inaongozwa kwa Mujibu wa Sheria. Sasa km ndivyo ilivyo basi hakuna sheria inayosema watu lazima watoe michango ila sheria inasema kuwa lazima ulipe kodi.
Anasema kuwa Duniani kote nchi haiendeshwi kwa Michango ila huendeshwa kwa Kodi. Hili ni darasa tosha.
 
Katika hali halisi ya kisasa ktk mabunge mengi ya duniani "Viongozi wakuu wa bunge ni 1.SPIKA WA BUNGE 2. KIONGOZ WA SHUGHULI ZA KILA SIKU BUNGENI[pm] na 3. KIONGOZI WA KAMBI RASMI BUNGEN. Lakini bunge la nchi hii limeendelea kuendeshwa kienyeji kwa kutumia wingi wa idadi ya uwakilishi kichama ktk bunge". Kauli ya mh. LISSU
 
Tumekaribia kwenye ngome ya ushindi.. Asante kamanda.
 
Mh Tundu Lissu anasema CHADEMA imekaribia ngome ya adui au kukamata dola ndo sababu wanafunguliwa kesi kila kukicha
 
Kwa kumalizia kipindi Mtangazaji kamuuliza Lissu kwanini wabunge wengi wa chadema wana kesi kila uchapo? Afu Mh. Lissu akajibu "NDUGU MTANGAZAJI, CHADEMA IMEKARIBIA NGOME YA ADUI[ ikulu] hii ndiyo sababu ADUI AMEKUWA MKALI SANA NA ANATUMIA KILA AINA YA MBINU KUJILINDA.
 
ukiona giza nene ujue kumekaribia kucha.sasa tumeifikia ngome maccm yamedata .big up sn TUNDU MWANA WA LISSU
 
Back
Top Bottom