Tunda nimelitungua!



Hata mimi nimelitungua......! Japo nimeshindwa kuelezea kwa uhondo huo!
 
Tunda nilotungua
Jinale sitofichua
Uale lilochanua
Kokwaye nikabanjua!

Si chungwa nawaambia,
Si fenesi naapia
Si embe mkadhania
Tunda la Kitanzania!

Mtini nililiona,kiukweli lilinona,
Nikatamani limenya,mdomoni limun'gunya
Hisia zkasema tulia'
Tunda langu tajilia.

Mwakijiji nlomjua.shaka sikumtilia,
Kuwa tunda akilona,atataka litungua,
Kumbe nayejatulia,
Ndio keshalitungua,

Mate nlilimezea,pindi macho yakilona,
Nikizidi vumilia,ipo siku talivuna,
Kila siku chekelea,nkilona siwezi nuna,
Mwakijiji katungua,analila kwa kuguna,

Tunda mithili ya epo,ama kiembe bolibo,
Natamani piga chabo,ulilapo kwa mpigo,
Labebeka kirahisi,haliwezi kuwa zigo,
Tunda sio nanasi,na halifanani na bungo,
Mwakijiji ulotungua,sio muwa wa mafundo,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…