Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
Kwa mujibu wa Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola aliyoitoa January 17, mwaka huu wakati akizungumzia mwenendo wa kesi mbalimbali za rushwa zilizokuwa TAKUKURU (ikiwemo kashfa ya Lake Oil kudai kusafirisha mafuta nje uongo).
Mlowola alisema Serikali ilipoteza kodi ya Shilingi 487 kwa kila lita moja ya mafuta inayodaiwa kusafirishwa nje na Lake Oil lakini ikatumika nchini. Hali hii ilisababisha serikali kupoteza takribani Shilingi Bilioni 8.5 za kitanzania kutokana na usafirishwaji wa lita 17,461,111 kwa kipindi cha mwaka 2013 &2014.
Kwa sasa tozo hii imefika Sh.587/= kutokana na serikali kupeleka maombi bungeni mwaka jana kuomba bunge liidhinishe ongezeko la Sh.100/= kwa kila lita moja ya mafuta ili kuchangia fedha ktk mradi wa umeme vijiini (REA).
Wabunge wa upinzani walipinga kwa hoja na kuishauri serikali kutafuta njia nyingine ya kupata fedha za REA badala ya kukimbilia kuongeza bei ya mafuta, lakini wabunge wa CCM kama kawaida yao wakaunga mkono hoja 100% na kuidhinisha ongezeko hilo.
Hivyo basi kuanzia mwaka wa bajeti 2015/16 serikali ikaanza kutoza Sh.587 kwny kila lita moja ya mafuta (Petrol, Diesel &mafuta ya taa). Tozo hii inajumuisha kodi mbalimbali, ushuru wa forodha na mchango wa REA.
Maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba ukitaka kujua bei halisi ya mafuta nchini chukua bei unayouziwa kisha toa Sh.587. Kama unauziwa lita moja ya Petrol kwa Sh.1850, toa 587 utapata Sh.1263. Hii ndiyo bei ya mafuta kabla serikali haijatoza kodi. Yani ni bei ambayo tayari mfanya biashara anayo faida yake ndani.
Kwa mfano letz assume kwamba wafanyabiashara wa mafuta hupata faida ya Sh.100 kwa kila lita. Maana yake ni kwamba bei halisi ya mafuta ukiondoa kodi na faida ya wafanya biashara ni Sh.1163 kwa lita (1850 -587 - 100).
Lakini kwanini serikali imeamua kuweka tozo kubwa hivi ktk mafuta? Huku ni kuumiza mwananchi bila sababu yoyote. Kumbe tungeweza kununua mafuta bei rahisi tu ikiwa serikali ingeamua kupunguza wingi wa tozo kwny mafuta.
Lakini je hivi inaingia akilini mfanyabiashara apate faida ya Sh.100 tu kwa lita na serikali ijichukulie Sh.587 bila kufanya kazi yoyote. Yani mfanyabiashara anawekeza mtaji, anaagiza mafuta, anaingia risk ya kuyasafirisha na malori hadi mkoani kwake, kisha anaingia operational cost ikiwa ni pamoja na mishahara ya watumishi. Hapo hujaweka gharama za kujenga kituo. Lakini mwisho wa siku anakuja kupata faida ya Sh.100 tu kwa lita.
Halafu serikali ambayo haijachangia chochote inajitwalia Sh.587 kwa kila lita. Huu ni unyonyaji wa kiwango cha PhD. Unahitaji uwe na homa kali ya pepopunda ili uweze kuitetea serikali katika huu unyonyaji.
Kwanini serikali inataka kujishibisha kupitia migongo ya wanyonge? Ina maana imekosa kabisa njia nyingine ya kukusanya mapato isiyomuumiza mwananchi zaidi ya hii ya kuongeza tozo ya mafuta? Kwanini isiweke nguvu kwny madini, mbuga za wanyama, gesi, viwanda na sekta nyingine kuliko kubweteka kwa kuwanyonya wanyonge.?
Ikumbukwe mafuta yakipanda na gharama za maisha zinapanda mara dufu kutokana na shughuli nyingi za kiuchumi kutegemea nishati hiyo muhimu. Na yakipungua the vice versa is true.
Yani kwa mfano leo serikali ikiamua kuondoa hiyo tozo ya Sh.587 kwa kila lita ya Petrol na mafuta yakaanza kuuzwa Sh.1268 kwa lita tegemea gharama za maisha kupungua kwa kiasi kikubwa. Tegemea nauli kushuka, tegemea bei ya bidhaa kushuka (hasa bidhaa za viwandani na za kilimo ambazo husafirishwa kwa malori yanayotumia mafuta), tegemea humuma nyingi za kijamii nazo kupungua gharama.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 8.1 (b) inasema "lengo kuu la serikali litakua ni maendeleo na ustawi wa wananchi". Maana yake ni kwamba shughuli yoyote itakayofanywa na serikali inapaswa kuwa ya manufaa kwa wananchi.
Sasa je, kutoza Sh.587 kwenye mafuta sawa na asilimia 32% ya bei ya mafuta, wakati huohuo serikali hiyohiyo ikitoza asilimia 04% kwenye wawekezaji wa madini je ni sahihi?
Yani serikali kuwaumiza wananchi kwa kuwabebesha mzigo wa 32% kwenye mafuta huku serikali hiyohiyo ikiwaogopa "matycoon" wa sekta ya madini na kuwatoza 04% tu, kutaleta maendeleo na ustawi wa wananchi?
Nafikiri ni wakati muafaka wa serikali kuachana na vikodi vidogo vodogo vinavyomuumiza mwananchi na kutoza kodi kubwa katika sekta kubwa za uzalishaji. Mataifa yote makubwa duniani hufanya hivyo.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "serikali uchwara haiwezi kukusanya kodi. Itakimbizana na maskini barabarani lakini haiwezo kutoza kodi katika sekta kubwa za uzalishaji"
Sasa namshauri JPM arudie kusikiliza vizuri hotuba hiyo ya Mwalimu. Ainusuru serikali yake isiitwe "uchwara" kama Nyerere alivyosema. Aondoe kodi zote zinazomuumiza mwananchi ikiwa ni pamoja na tozo kubwa ya mafuta ya Sh.587 kwa lita. Hakuna serikali duniani inayoweza kupiga hatua kiuchumi kwa kumnyonya mwananchi maskini. Hakuna.
Nashauri JPM akae na washauri wake vizuri wamsaidie kuweka mikakati ya namna ya kusaidia maendeleo ya kiuchumi bila kunyonya wanyonge. Zipo sekta nyingi za uzalishaji ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuchangia pato kubwa zaidi la taifa kuliko hivi vikodi vya kuumiza maskini.
Toza kodi kwenye madini, gesi, makaa ya mawe. Promote sekta ya utalii, kilimo, uvuvi. Tutapiga hatua kiuchumi. Lakini kutoza kodi za kuumiza maskini na kutegemea Tanzania itakua nchi ya viwanda ni kujidanganya.
Hatuwezi kuwa nchi ya viwanda kwa kumnyonya bibi maskini wa kule Biharamulo kwa kumuingezea mzigo wa Sh.587 kwenye lita moja ya mafuta ya taa anayonunua kwa ajili ya kibatari chake. We need to change approach.
Ni aibu serikali kujisifu kukusanya mapato makubwa kwa kuumiza wananchi.
Malisa GJ.!