Tunawarithisha nini watoto wa kiafrika

Tunawarithisha nini watoto wa kiafrika

tatum

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
5,786
Reaction score
4,494
45237214_306103469991716_2281227997589536768_n.jpg


Afrika zamani liliitwa bara jeusi limekuwa katika harakati za mabadiliko kwa miongo kadhaa sasa kutoka katika mila za kishenzi na kuingia katika mila za kistaarabu,kutoka katika utumwa na kuingia katika kujitambua na kujisimamia mambo yake kutoka katika kutawaliwa na mataifa ya kizungu na kujipatia uhuru wake.

Na sasa tupo katika kutoka teknolojia za zama za mawe na chuma na kuingia katika zama za teknolojia za kisasa ili kurahisisha utendaji wa shughuli nyingi lakini na kuunda vifaa vya matumizi ya bindamu ambavyo vitarahisiha maisha yeke.

Lakini bado kwa nchi nyingi za kiafrika bado ni kitendawili kikubwa hasa vijijini kuwatoa watoto na hata watu wazima katika mila zao na kuwafanya waishi maisha ya kisasa zaidi kwa kujua mengi ambayo yanaendelea huko duniani.

Urithi wetu mkubwa umekuwa mila na destruri za kiafrica ambazo zimepitwa na wakati bado tunasafari ndefu sana kufikia maendeleo ya kweli kwa hili bara letu.Tunahitaji uelewa ulio mmoja ili kujinasua na hali hii ya umasikini wa bara hili la africa.
 
Back
Top Bottom