Mimi nimebukua kinoma na nimeona kwa macho yangu na kutembea mtaani kwa nchi 13 za mabara matatu ila nikatoka na theory moja tu "theory of population" , haya yaliyopo kwetu kwasasa ni kutokana na aina ya binadamu tuliopo hapa bongo na hulka zetu au tuseme "population composition" iliyopo ambayo imekaririshwa upumbavu wa "zidumu fikra za Nyerere", iliyojazwa utii wa kijuha kwa viongozi hata wawe wabovu na mizigo mengine mashangingi ya mjini na mahuni ya bongofleva , population yetu iliyojaa uoga wa kijinga eti ukikaidi na kuandamana utapigwa tu sababu stoo kuna mabomu na virungu!!si mtupige mtuue kabisa mridhike, population iliyojazwa upumbavu kuwa mkubwa hakosei na hakosolewi , nchi iliyojaa ujinga wa "nenda urudi mwezi ujao eti tutafute faili lako", nchi iliyojaa upumbavu wa "tumekusikia tutalifanyia kazi" , lini? Sijui wanafundisha mzungu mmoja yuko bomani anatawala mkoa mzima yaani mtoto ajifunze kuwa mzungu ni bora kuliko mtu mweusi!! shame on taasisi ya ukuzaji mitaala!!
Haya yote yataisha in 50 years to come hapo hawa watawala wengi "wanaonyanyua mabega" na kuongea kibabe wakiwa tayari huko mavumbini Allahu Aaalam of course labda nasisi pia tutakuwa skeletons tayari sababu shida tangu utotoni sasa life span ya mwafrika akitoboa 80 huwa kachoka sana.
Mazee mengi yanayoliibia Taifa letu yana 60+ years yako "jioni" kabisa! Mazee haya yamejaa kule Masaki na Oysterbay sijui Msasani ukiyatembelea home unacheka stori zao kutawala nchi huku yako hoi kwa uzee!
Naamini wanangu dot com school bus English medium hawamjui Nyerere wala ujamaa sijui mkoloni, kizazi hicho kikifikia utu uzima 50 years to come wamebaki wenyewe tu mazee yote mafisadi yamededi patachimbika, hawa hawatakubali tozo na ugumu wa maisha lazima wataenda kuogelea Magogoni na kubanika wale tausi!
Ni kweli wazee na vijana tuliopo sasa ya Sri Lanka hapa bongo ni stori tu hatuwezi kufanya kama wao!
Time , uzee na kifo ni kiboko ya mafisadi!!