Tunauza maeneo yetu yapo jijini Dar es Salaam

Kupata majaliwa

New Member
Jan 26, 2016
4
0
Wasalaam waleikhu na bwana asifie kwenu, natumaini nyote mnaendelea vizuri na shughuli za ujenzi wa Taifa letu hili.

Dhumuni la kuandika thread hii ni kupenda kuwatangazia umma kuwa nauza maeneo yangu mawili, moja lipo Mbweni - Mpiji ambalo lina ukubwa wa Square Metre 1499 sambamba kabisa na hati yake, kutoka eneo lilipo sio mbali na barabarani, huduma zote za msingi zinapatikana kama vile maji, umeme na huduma za afya - Bei yake ni Milioni 85 maongezi yapo.


Eneo lingine lipo Madale kwenye viwanja vilivyopimwa ambalo lina ukubwa wa square Metre 530, Bei yake ni milioni 30 tu. Huduma zote za msingi zinapatikana.

Hili eneo la tatu sio langu bali ni la shemeji yangu ambaye nae analiuza ni shamba lenye heka 4 lipo madale kwa kawawa, kila heka ni shilingi milioni 35 maongezi yapo, bado halijapimwa, kutoka barabara ya lami ya wazo ni nusu kilometre.

Kwa Mawasiliano zaidi unaweza ukawasiliana nasi kupitia namba hizo hapo chini

0753 450 240

0683 56 28 87

au kwa barua pepe

Email : abdchandetz@gmail.com

Wote Mnakaribishwa
 
Kila mtu anajipangia bei itabidi serikali il été ki ewura au ki sumatra cha ardhi mtu anakurupuka tuu unasikia USD 2 m shenzy kama zinapaikana kirahisi na ww kuwa nazo
 
Kuna watu walikwenda kujenga mabondeni kwa kukosa viwanja vya kupimwa kutokana na watu kushika viwanja kwa lengo la kuviuza vitakapo panda thaman, nahisi kama hizi almashauri zilizouza hivi viwanja zingewanyang'anya vibali wote walioshindwa kuviendeleza.
Mkuu me si mnunuaji nasubir mika kuminambili ipite hujaendeleza nije nipaendeleze hapo maana itakua haki yangu.haaaah utani kweli.
 
Madale mil 35???? Mbweni nje ya Mji mil 85????? Una Akili wewe?? Natamani fegi ingeuzwa laki gunia la gomba lingeuzwa jero ccm wangetinga khaki chedema nao kijani na yellow.
 
aiseee bei zimenishinda uzianeni wenyewe kwa kwakweli
ingawaje nimependa maeneo hayo ila je sio yale ya dinga likija linabomoabomoa kweli
 
Hivi ni kuwa huna kabisa akili au unapost tu.. au madrassa imekuvuruga ubongo...!!? 530 sqm for 30mil... ww chiizi kabisa..!! 1486 sqm for 85 mil...!!???? wee tahira kabisa... hujui unaishi tu, dead walking...!!
 
mtu ambaye hajawai kushika hela anafikiri hela ni nyepesi kuipata so anajitajia tu ma bei ya ajabu..

mbweni milion 85.. hiyo bei unanunua nyumba kabisa nzuri maeneo yaliyoendelea tayari..
 
nawashangaa watu wanaotukana hapa, yeye ametaja bei akasema mazungumzo yapo, maana yake kuwa atashusha, kwani hata kama ni kubwa sana kwani umelazimishwa kununua?
 
HIZO Price Zenu, Kwa Makabwela Ni NDOTO Kumiliki Ardhi Na Kibanda Cha Kuweka UBAVU!! NDIO Maana Tukimbulia Vijijini Kila Uchao Na Miji Tunawaachia Ninyi Wenye NCHI!!
 
Back
Top Bottom