TUNATAKA HAKI KWENYE RASILIMALI ZA NCHI

nguyunguyu

Member
Sep 13, 2014
80
225
WALIOTUFIKISHA HAPA WAKO CCM NA CHADEMA |¦| Tumuunge Mkono Magufuli Ili Watoto Wetu Wasije Kutucheka Kama Sisi Tunavyomcheka Mangungo

Anayedhani serikali ya CCM chini ya Mh Magufuli haina uhalali 'legitimacy' wa kuongoza mapambano ya uhuru wa kiuchumi anakuwa hajui kwanini wananchi walimuamini Mh Magufuli kupitia chama cha mapinduzi na kukipa ridhaa ya kuunda serikali.

Anachokifanya Mh Rais ndicho kilichosababisha watanzania wakamuamini yeye na chama chake na kumpa ridhaa ya kuunda serikali. Anachokifanya Magufuli leo hii, ndicho alichokiahidi kwa watanzania wakati anaomba kura, tena akasema bayana kuwa 'nipeni kura niende huko juu nikayatumbue haya majipu yaliyotufikisha hapa'.

Anachokifanya Mh Rais Magufuli kwa saaa ndicho kinawafanya hata baadhi ya watendaji serikalini, wanasiasa, watumishi, na hata wanasiasa wa upinzani na wale wa chama chake kumchukia na hata kuanza kumbatiza majina ya hovyo kisa ameguza maslahi yao, ambayo kimsingi ni maslahi ya umma yaliyokaliwa na wachache.

Mpaka sasa tunakubaliana kuwa watendaji na wanasiasa waliokuwa wakitokana na CCM na serikali yake, wanasiasa na watendaji walioaminiwa na wananchi walitumia vyeo vyao kufanya maamuzi ambayo hayakuwa na maslahi kwa taifa letu. Hao wanasiasa na watendaji kwa sasa wengine ni wanasiasa, wengine ni marehemu, wengine wamestaafu siasa, wengine wanafanya biashara, wengine wamehamia vyama vingine vya siasa na wanapambana kushika dola tena huku wakijipambanua kuwa ni Malaika ilihali inajulikana kabisa kuwa mwanzo wa hiyo CCM kuchafuka ni wao.

Pia tunakubaliana kuwa miaka hiyo yote CCM ndiyo iliyokuwa madarakani, na pia tunakubaliana kuwa hata sasa, serikali iliyoamua kupigania maslahi ya kiuchumi ya taifa letu ni serikali inayoongozwa na CCM. Mpaka hapo unaweza kuelewa maana ya CCM Mpya inayoanza kuijenga Tanzania Mpya chini ya Mh Magufuli na serikali yake.
Kuna ambao walisikika wakibeza kuwa Mh Rais badala ya kuvunja mikataba anahangaika na makanikia/mashobo. Watu wa aina hii ni wa kuwadharau tu kama watoto maana huwezi kuvunja mkataba bila kuwa na 'binding legal defaults' ambazo zinaweza kukufanya uvunje mkataba bila kuathiriwa na vifungu vya mkataba husika.

Hii ina maana kuwa tangu siku ya kwanza Mh Rais alipozuia usafirishaji wa mchanga kupisha uchunguzi, kila Mtanzania mwenye akili timamu alipaswa kuunga mkono uamuzi huo, maana ndiyo msingi wa kwanza ktk kujua namna ya kuweza kuondokana na mikataba hiyo ya kinyonyaji. Maana mikataba ya kimataifa ya madini hairuhusu ukwepaji kodi, hairuhusu utapeli (Fraud) ukifanikiwa kuyabaini hayo kwa ushahidi wa wazi una uhuru wa kuuvunja huo mkataba bila madhara yake ku 'backfire'

Je ni kweli kwamba CCM haina haki wala uhalali wa kupigania uhuru wa kiuchumi? Binafsi naweza kusema kuwa CCM imepitia kipindi kirefu mno cha kuliongoza taifa hili tangu uhuru.Kila jema ktk maendeleo ya nchi hii limeletwa kutokana na uongozi imara wa chama hicho, na kila linaloonekana kama baya au changamoto limetokana na viongozi wasio waaminifu ndani ya chama na serikali yake.

Katika haya mapambano mapya ya uhuru wa kiuchumi tumeshuhudia jinsi ambavyo wanasheria tuliowaamini wakijaribu kupita mlango wa nyuma ili kumsaidia mwekezaji kukwepa mkono wa sheria na kutaka kuwasaliti watanzania wasipate haki yao iliyopotea kwa muda mrefu. Hiyo yote ni kuhakikisha kuwa serikali ya CCM Mpya inashindwa ktk mapambano haya ya kuusaka uhuru wa kiuchumi.

Katika vita hii, wahanga wa wizi wa rasilimali madini zetu wapo ndani ya serikali, wapo ndani ya CCM tangu 1995 wakijiita wanamtandao, wapo nje ya siasa, wapo ktk mahakama zetu, wako ktk vyombo vyetu vya kutunga sheria/bunge, wapo ktk wizara zetu, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, takukuru nk.

Historia inaonyesha jinsi baadhi ya wakosoaji na wapinzani walivyokuwa mstari wa mbele miaka ya 2000-2007 ktk kupambana na kile kilichoitwa kuwa ufisadi katika mikataba ya madini nchini. Lakini tumeona jinsi watu hao hao walivyotugeuka na kuanza kujipenyeza kwa mwekezaji ili wakwamishe jitihada za Magufuli na serikali yake. Kuna wanasiasa ambao kwa miaka mingi wamejipambanua kama wazalendo, nk lakini tumeona jinsi ambavyo walipinga vikali zuio la mchanga kupisha uchunguzi. Sasa unajiuliza bial uchunguzi utajuaje iwapo unaibiwa? Hawa wanasiasa walikuwa wanapinga kwa maslahi ya nani??

Kwa upinzani hiyo ni furaha kubwa kwao maana watapata cha kuzungumza majukwaani kuwa walijaribu, wameshindwa. Lakini wasisahau kuwa huu siyo muda wa kumtafuta 'star'au mshindi wa kisiasa ktk haya mapambano bali ni muda wa kuweka silaha zetu za uchadema na uccm chini na kulikomboa taifa kutoka katika huu ukoloni wa kiuchumi

Ingekuwa ujinga, tuhuma au makosa ya watendaji au mtu mmoja mmoja ndani ya chama na serikali yanakifanya chama kizima kikose uhalali 'Legitimacy' wa kushughulikia mambo ya msingi au hata kukifanya chaka kiache kutekeleza wajibu wake basi ni dhahiri kuwa leo hii Lowasa, Sumaye, Kingunge nk ambao historia inaonyesha kuwa walikuwa sehemu ya CCM tena nyadhifa nyeti za kimaamuzi wasingekuwa Malaika wa upinzani wa nchi hii.

Anachokifanya Magufuli kinatoa taswira mpya kuhusu nchi yetu, kinatoa hofu na uongo ambao watanzania wamepandikizwa miaka na miaka kuwa nchi hii ni maskini ilihali siyo kweli. Kilichofanywa na Magufuli kinafungua mlango mpya katika mitazamo ya watanzania. Kuanzia sasa huwezi ten kuwaambia watanzania kuwa nchi yetu ni maskini wakakuamini kirahisi maana tayari Magufuli amewathibitishia kwa ushahidi wa kiutafiti kuwa siyo kweli

Hio nguvu inayotumika kuhakikksha kuwa Magufuli haufanikiwi ktk hii vita ya uhuru wa kiuchumi inatoa ushahidi kuwa wakosoaji na wapingaji wengi ktk nchi hii wanauchukia UFISADI kwasababu wamekosa nafasi ya kuwa MAFISADI. Ndiyo maana hata uliyemdhania ndiye kumbe siye.

Tuungane kwa pamoja katika kupigania maslahi mapana ya taifa letu na vizazi vijavyo. Sisi kwa kizazi chetu tunaweza kuwa tumechelewa kunufaika na maliasili za taifa letu, lakini hatujachelewa kuweka misingi imara ya kuhakikisha kuwa watoto wetu wananufaika na rasilimali hizi tulizozichezea kutokana na wasiowaaminifu wachache

Bonyeza Magoiga SN
 

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
44,073
2,000
Tuungane kwa pamoja katika kupigania maslahi mapana ya taifa letu na vizazi vijavyo....Asante
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom