Tunapompongeza Samatta, tusisahau kuipongeza Simba SC

MFUKUZI

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
933
699
Mimi ni miongoni mwa wapenzi wengi wa soka waliokuwa na furaha kubwa baada ya Mbwana Samatta kutangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Afrika wa Ndani.. Kwa kweli bila kutambua na kupongeza jitihada binafsi alizozifanya hadi kufikia hapo alipo basi utakuwa na chuki tu ambazo hazitamzuia yeye kuendelea kupaa katika ulimwengu wa Soka.

Samatta amedhihirisha kwamba kuwa kama kijana yoyote wa kitanzania mwenye kipaji cha soka anaweza kufika mbali na kuwa icon ya nchi na dunia kwa ujumla. Pia kwa tuzo hiii amekuwa fundisho kwa vijana wengi wenye ndoto kama zake kuwa.. Juhudi, maarifa, uvumilivu na nidhamu ndiyo nguzo kuu za kufikia ndoto zao.

Pamoja na pongezi nyingi kwa Samatta, nadhani ni busara ya kawaida kuipongeza CLUB ya Simba ambayo ndiyo ilimpa fursa ya kucheza na kuonekana kwenye soka la kimataifa. Bila SIMBA SC kupata kuwa bingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwa wakati huo na kufanikiwa kuiwakilisha nchi yetu katika michuano ya club bingwa Afrika na kukutanishwa TP Mazembe may be Samatta asingekuwa hapo.

Nakumbuka mechi ile iliyopigwa Uwanja wa Taifa, simba ilipoteza dhidi TP Mazembe.. pamoja na kuzomewa sana na mashabiki wa wapinzani wa jadi (YANGA).. Samatta hakukata tamaa.. alicheza soka safi na kuwadhihirishia TP Mazembe kuwa Samatta ni lulu na anaweza kuisaidia siku za usoni.

Haikuwa taabu sana kwa uongozi wa Simba chini ya Ismail Rage kukubali kumuuza Samatta TP Mazembe kwa sababu ndiyo falsafa ya Simba kuwaruhusu wachezaji wao wanapopata fursa sehemu nyingine. Hali ambayo ni tofauti sana na wapinzani wao wa jadi.

Lazima tuwe wa kweli.. pongezi tunazozitoa kwa SAMATTA tusisahau kuipongeza SIMBA SC kwa kumpatia fursa Samatta..!!
 
Well said Mkuu,umenena vyema kabisa Ila ngoja waje wale wenzetu wa upande wa pili lazima waharibu hali ya hewa.
 
Ni simba tu ndo timu yenye historia ya kimataifa na iliyouza wachezaji wengi nje, Samatta, Henry Joseph, okwi, machupa nk
 
Hivi Simba SC ilipocheza na TP Mazembe ilikuwa kabla au baada ya KUTOA ILE DOZI YA 5 - 0 kwa Yanga? NIMESAHAU, nikumbusheni!
 
Simba wanajua ku deal na soka la kisasa. Yanga wako too local ... hawana utaratibu wa kuuza au kuruhusu wachezaji wao muhimu kwenda kutafuta maisha nje. Walikuwa radhi hata kuweka Walinzi Airport kuzuia wasitoroke. Yanga ni wabinafsi sana.

Hata Nonda Shabani, aliamua kutoroka kwenda South Africa baada ya kubaniwa. Ndo maana Yanga waliambulia patupu alipoenda kucheza Ulaya ilhali wao ndio walimlea pale Yanga "B".

Sitasahau walichomfanyia Edibilily Lunyamila baada ya kupata dili la Kucheza Bundesliga! Kisa tu walikuwa na mechi na watani wao, hivyo walitaka Lunyamila acheze kwanza hiyo game halafu wamruhusu kuondoka. Baada ya game hiyo, Wajerumani wakamwambia nafasi yako tumeshaiziba tayari.

Hata Ngasa, kwenda West Ham kufanya majaribio ilikuwa taabu sana ... Kijana wa watu akakonda kwa stress, alipofika kule akaambiwa huna fitness ya kucheza EPL kwa sababu mwili wake ulionekana kukosa lishe. Yanga bhana ...!

Ngoja niishie hapa ...! Watani zangu msinirushie mawe, kuweni professional jamani!!!
 
Ikitoa kichapo cha 5-0 dhidi ya mtani wake ilikua tayari kisha cheza na TP Mazembe.
 
Back
Top Bottom