Tunapoelekea Tanzania siko

Tunapoelekea Tanzania siko

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
6,909
Reaction score
4,057
NAPATA wasiwasi huko tunapoelekea sipo mfano kuhusu suala la gesi inabidi kufanyike mazungumzo ya kina na wananchi wa Mtwara lakini katika hali tete kama hii vitisho havisaidii nadhani huko tunapoelekea sipo serikali ifanye dialogue na wananchi
 
kuna watu wanalipwa ikiwezekana na mapampuni yanayofanya uchimbaji ili tuvurugane tuache kuangalia tunanufaika vipi. huyu anayesambaza vikaratasi ni nani? mtaji wa kuendesha hizi propaganda anapata wapi? atarudishaje gharama zake.

kihistoria kinachofanyika mtwara kimewahi kusaidia wapi kama sio hata wawekezaji ambao walikuwa waende kuanza kuogopa na kufuta mipango.

serikali fanyeni upelelezi maana swala la kusema wananchi wa mtwara ni bendera tu angalieni upepo unatoka wapi
 
NAPATA wasiwasi huko tunapoelekea sipo mfano kuhusu suala la gesi inabidi kufanyike mazungumzo ya kina na wananchi wa Mtwara lakini katika hali tete kama hii vitisho havisaidii nadhani huko tunapoelekea sipo serikali ifanye dialogue na wananchi

Kiongozi!

huko tunako elekea NDIKO. Tumesha zitambua haki zetu. Kwamba wote tufaidike na tugawane sawa matunda ya rasilimali zetu. Walafi wachache wametambua kwamba sasa walinao kosa kufaidi wameshaamka kudai haki zao. Nao hawataki.

Kilicho bakia ni kupigania ile haki yetu kwa namna yoyote ile. Na kama ni kukosa basi tukose wote.
 
kutowasikiliza wananchi ni kuruhusu vurugu ziendelee
 
ogopa sana unapoona mambo yanapelekwa kasi ili watu wasahau
 
Back
Top Bottom