Tunapoelekea na tulipo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunapoelekea na tulipo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Anfaal, Mar 26, 2011.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sasa imekuwa kawaida saana kila asubuhi watu kukejeli dini za watu humu jamvini na hasa waislam wakizidi kukejeliwa kila kukicha.
  Hivi sasa cha muhimu si hoja bali ni nani kazungumza na imani yake ikoje. Ukipitia thread ya maandamano ya waislam suala hili lipo wazi saaana. Wengi wa waandamanaji pale wanatukanwa km hawajaenda shule nk lakini km yangekuwa maandamano ya CDM basi yale huhesabika kuwa ni maandamano ya wapigania haki ya maendeleo na nimaandamano yenye akili. Kumbuka kwenye lile kundi wapo waliompigia kura slaa na wabunge wengine wa cdm lkn wao maandamano hayo ndio msimamo wa maoni yao. Kwa hali ilivyo sasa ili uwe na akili lazima uandamane na cdm na usiwe kwenye yale maandamano ya waislam na hivyo kumaanisha through simple logic huwezi kuwa muislam ukawa cdm. Kauli zenye tafsiri za aina hii na comments za hivyo zinawaumiza saana wale walioipigia kura cdm na kisha kulipwa malipo ya kukashifiwa. Wengi wanaamini chaguzi hazijafika kikomo na kama hali hii haitanusuriwa basi kwao hawatakuwa tayari kupiga kura za kuwatusi mbeleni.
  Kwahiyo tunakoelekea ni kupoteza kura za cdm, cdm kuonekana hasa imevaa sura ya kidini km wafuasi hawatakoma lugha za kejeli na hivyo hata zile mbio za kuelekea ikulu kuzikwa mapema. Tunahitaji nini kukumbuka kule bukoba, mwanza, arusha nk waislam walikuwepo? Tunasahau kuna waislam walijeruhiwa na kupoteza maisha arusha? Km hatuwezi kujinasua kwenye ghalika hii basi tufanye juhudi ya kuonyesha kuwa cdm pamoja na wafuasi wake hawawakashifu waislam.
   
 2. b

  bnhai JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Bora wewe umenena. Huenda wengi wakaelewa kuwa adui yao si uislam na waislam.
   
Loading...