Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Nimepigwa na butwaa kubwa kuona mawazo ya Waberoya ya kwamba kumuua mtu nchini Tanzania ni rahisi sana, na kwamba haihitaji kumteka mtu kama Bashe ili kukamilisha mpango wa mauaji.
Mawazo haya ni mabaya sana, ya hatari sana na ya kigaidi yanayostahili kupingwa kwa nguvu zote kwa sababu uhai wa binadamu ni kitu kilichotukuka. Uhai wa binadamu ni sacred (ni kitu kitakatifu) yaani ni kitu cha kuheshimiwa sana. Kurahisisha mauaji ni mawazo ya ki-barbaric (kishenzi na kisheteni).
Ni mawazo ya kutaka kutisha watu kutetea nchi yetu na ni mawazo ya kuwatia kiburi watawala wenye mawazo kama ya Waberoya. Tangu kuubwa kwa ulimwengu, uhai wa binadamu ni kitu cha thamani kubwa.
Ni zawadi ya pekee ambayo binadamu tunaipata kutoka kwa Mungu. Hakuna mtu amewahi kumuumba binadamu. Ndiyo maana suala la kuua haliwezi kuwa rahisi.
Mtu mwenye mawazo ya kurahisisha mauaji si wa kawaida, aweza kuwa ni kichaa au mpumbavu kupita maelezo. Mawazo ya kurahisisha mauaji ni ya kigaidi.
Hata kama unamchukia mtu kupita kiasi, haijawa kitu rahisi kuua. Ndiyo maana wauaji hupanga njama ili wasijulikane kuwa wametekeleza kitu hicho. Ndiyo maana hata sasa kuna mjadala usiyokwisha kuhusu hukumu ya kifo.
Kuua si kitu rahisi na hata majaji wanaotoa hukumu ya kifo hawaitoi kirahisi kama Waberoya anavyofikiria. Kuna simulizi nyingi zinazoeleza kuwa hata mtu anapofanikiwa kumuua mtu kwa siri dhamira humuandama mpaka anajisema mwenyewe. Damu ya mtu isiyo na hatia inawaandama wauaji, inagharama kubwa kwa wauaji.
Bashe ni mtu aweye yoyote ni binadamu ambaye uhai wake unathamani isiyomithilika, na hivyo mauaji ya mtu hayawezi kamwe kuwa kitu rahisi. Hivyo wananchi tunaoheshimu uhai wa binadamu tuungane, tupinge na tulaani mawazo ya kurahisisha mauaji ya watu wa aina ya Waberoya.