Tunaongoza VPL, Msitegemee Yanga SC kupoteza hata "Alama" moja.

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,288
15,240
Naona mmejawa na furaha! Endeleeni tu kufurahia.....

Ila napenda kuwakumbusha kuwa kwenye Msimamo wa VPL mko nyuma ya YANGA SC kwa zaidi ya alama 1.....

The fact that

1. Uko nyuma kwa zaidi ya alama moja dhidi ya Wanajangwani.

2. Bila kusahau zimebaki mechi chache ligi kufikia tamati.

3. Kikosi kizima cha wapinzani wenu wako on-form.

Basi watani zangu msitarajie Yanga SC kupoteza hata "ALAMA" moja kutoka kwenye hizi chache zilizo salia....

"Naomba nitoe kiapo hiki mbele yenu..."

Dar es Salaam Young African SC ndio Bingwa halali wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2016/17.
 
yanga kuna mgomo baridi.
pesa hakuna. mshahara wachezaji hawajalipa
 
Mpaka sasa tunaongoza na point zetu za kagera tunapewa,mkishinda mechi zote bado tutawaacha point moja,usitegemee pia simba kupoteza mechi
 
Ukwendreeeeeee zako huko!Mpira unadunda,si wa kuapia hivyo.
Mpira unadunda lakini sio VPL ambapo GIANT kama Yanga SC anatafuta alama 3...........

Hakuna wa kumzuia... Na nyinyi hilo mwalijua kabisa...
 
yanga kuna mgomo baridi.
pesa hakuna. mshahara wachezaji hawajalipa
Hahahaha

Mgomo baridi MC Alger angepigwa cha "UKWEZI"...

Msije mkaanza kusema YANGA SC wananunua mechi.... Maana kwa jinsi tutakavyo anza kuzitafuna hizi mechi 5 zilizobaki.... Najua hamtapenda...

Ila nakusihi usije kuanza kulalamika Yanga SC ananunua game ikiwa kwa mdomo wako hapo umenena kuwa Yanga SC imefirisika kiasi cha kushindwa lipa Salaries...
 
Mpaka sasa tunaongoza na point zetu za kagera tunapewa,mkishinda mechi zote bado tutawaacha point moja,usitegemee pia simba kupoteza mechi
Mbona mnaota ili hali jua lime kwisha chomoza?

Nani amekuambia kuna alama za Mezani?

Endelea kuamini akina Hans Pope maana wamekuwa wakiwadanganya kwa miaka 5 sasa na nyinyi mnaendelea kudanganyika tu...

Eti alama za mezani!!!! Hahahah
 
Nilishasema bingwa wa mwaka huu atapatikana kwa staili ya nyota wa filamu ya kihindi. Kutokana na misukosuko, vipigo na maumivu mengine kuwa mazito kwa nyota wa filamu, huwa inafikia nyota huyo anaumiza watazamaji hadi wengine wenye roho nyepesi wanatoa machozi wakati filamu ikiendelea lakini wmisho wa siku anaibuka kuwa shujaa wa filamu.
 
Nakuona nakuona mtan unamwaga povu
Mtani! Hili sio povu....

Bali ni Ukweli uliopo....

Nangojea wakati wenu wa kuanza kuimba mapambia wanayo yaanzisha akina Hans Pope...

Yanga wanabebwa.

Yanga wananunua mechi.

Yanga wanaharibu soka pa bongo.

Manji anahonga wachezaji pinzania...

Malinzi anapendelea Yanga..

Hizo hapo juu ni baadhi ya mapambio ambayo najua si muda kabla hayajaanza kuimbwa na mashabiki wa MATOPENI FC wakiongozwa na Manara....
 
Back
Top Bottom