Tunaomba viongozi wetu muwe serious!

SueIsmael

JF-Expert Member
Dec 11, 2013
932
1,282
Tunaambiwa tusitende jambo au kusema jambo ukiwa na hasira, furaha sana au taharuki, lakini yamenishinda! Kila siku mambo yanatendeka kama michezo ya kuigiza isiyo hata na miongozo sawia. Kila kiongozi atajiibukia na kutamka la kwake na wakati mwingine hakuna hata mantiki.

Lililonishtua, kunipa simanzi na hata kunitia hasira ni hii 'sarakasi' nyingine inayopewa promo ya Naibu Waziri wa Afya+ kutangaza vita ya ushoga kama kipaumbele chake cha sasa. HIVI KWELI WAZIRI MSOMI NA TENA KIJANA KAMA WEWE KIPAUMBELE CHAKO NI KUKIMBIZANA NA WATU WAZIMA WANAOJIFUNGIA NDANI YA KUTA NA KUFANYA MATENDO YAO KWA MAKUBALIANO YAO WENYEWE?!!! IS THIS TRULY YOUR PRIORITY?!!

Dr. Kigwangalla, H. (@HKigwangalla) | Twitter

Kweli kabisa katika 'changamoto' zote (kama hii nayo ni changamoto) zilizoko kwenye sekta ya afya, maendeleo ya jamii, zinazowakumba wazee na watoto; hii ndio changamoto inayochukua muda wako (na wengine pia) na rasili mali nyingine kupambana nayo?

Hebu tuwe serious japo kidogo. Yaani kodi yangu ninayoitolea jasho, inayokatwa kabla hata mshahara haujafika kwangu, inatumika kwa 'oparesheni' za namna hii. Kodi yangu ndio inatumika kukulipa wewe na watumishi wengine wa serikali mshahara ili muda wako na wakwao utumike kwa mambo kama haya!

It means five years down the lane, this is going to be an accomplishment you'll be proud of?!

Mfano mdogo tu katika moja ya mambo mengi ambayo yanastahili kukuumiza kichwa na kuchukua muda wako, ewe Mh Naibu Waziri:
- Mpaka 2014 Tanzania ilikuwa na vituo vya afya 7071 (List of health facilities with geographical location - List of Operating health facilities - 2014 - Open Data Tanzania) ambavyo ni mjumuisho wa hospitali kubwa hadi zahanati. Mpaka 2013 idadi ya watu ilikuwa zaidi ya milioni 49. Jumla ya watumishi wote wa afya mpaka 2014 ilikuwa 35,750 ( Number of health workers by region - Number o health workers - 2014 - Open Data Tanzania). Mpaka mwaka huu tuna idadi ya watu zaidi ya milioni 52, huku tukitegemea kuongozeka zaidi ya mara mbili ya idadi hii ifikapo 2030. Do the math and tell me what exactly are we expecting from the health system?!! As it is, the health system is inadequate, come 2025 we are in deep trouble! To make matters worse, we have more health issues as a result of climate change effects, population shifts, etc.

In the meantime, we have the minister running after consensual adults who do not even comprise of 5% of the population!

Inatia hasira sana!
 
Back
Top Bottom