Tunaomba serikali itusaidie wachimbaji wadogo

ukianza na kilimo,kilimo cha mahindi na mbaazi kinalipa sana
 
hapa babati mpaka madini ya uranium yapo tele!
Kama kuna mtu anataka anitafute.
 
kazi ya TMAA nikudhibiti utoroshwaji wa madini na uchimbaji holela usiofuata taratibu za kisheria,sasa mbona mmeacha baadhi ya watu wakichimba madini kiholela tena mchana kweupe,hivi suala hili mmeamua kulifumbia macho?
 
tunawaona mnavyopambana mikoa mingine,je huku manyara babati hamjawa na wakala?
 
heri ya mwaka mpya wana jf wote,
mm nawakumbusha tu hawa TMAA kuwa huu mwaka mpya tunawaomba basi mtukumbuke sisi wachimbaji wadogo hapa babati.
 
Tunawaomba TMAA mje hapa babati muweke vituo vyenu vya ukaguzi.
 
babati inajengeka sana njoon mkague mwone je wafanya biashara wa madini ujenzi wanafuata taratibu na sheria za uchimbaji madini?
 
tukianza na madini ujenzi kama mchanga unachimbwa hovyo bila taratibu huku viongozi wa serikali wakiwatazama bila kuchukua hatua yeyote
 
 
 
Mkuu wa mkoa wa Manyara mkoa wako wa manyara unavyanzo vingi vya mapato moja wapo ikiwa ni madini ujenzi
 
Sisi tumepeleka malalamiko kwa mkuu wa wilaya,hajatusaidia kitu,tukaenda halmashauri ya wilaya nayo pia haijasidia,tukaenda halmashauri ya mji babati wenyewe ndio wanasapoti wenye magari wabebe mchanga na mawe bila kulipiwa
 
Duhh maskini sisi wanyonge pesa zetu zinateketea hivihivi huku tukiona bila kupata msaada wowote
 
jamani tusaidieni sisi wachimbaji wadogo wa madini ujenzi hapa babati
 
mkuu wa wilaya tunaomba utusaidie sisi wachimbaji wenye leseni tuweze kuchimba madini na serikali iweze kupata mrahaba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…