Tunalipishwa Tsh 200 kupanda Daraja la Ubungo (UDART), ili uweze kuvuka ng'ambo ya Barabara

Inanambo

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
4,037
2,839
Leo nimelipa 200 kupanda Daraja la UDART kupitia Ubungo Bus Terminal. Vijana getini wamenizonga wakinilazimisha kulipa 200 kwa kuwa nimekanyaga Ubt. Eti watajuaje usafiri wa mikoani na wa UDART? Nikaenda tena kulipa 650 kwenda mjini. Jumla 850

Ni halali kulipa Geti la Ubungo ilihali sisafiri? Vijana mwenyewe Wa getini washari kweli.

Nimeshuka kwenye basi la haraka kituo cha Ubungo terminal napita darajani nivuke barabara naona jamaa wananidai pesa.

Nikawabia mimi sisafiri navuka barabara hawataki. Ikabidi nitudi nyuma,je mh Makonda kupita kwenye hili daraja tunalipia?
 
Ile Zabuni ya Ukusanyaji Ushuru pale UBT itazamwe upya,imekaa kijambawaazi sana,haiwezekani mtu upo na mabegi lukuki unawahi basi na tiketi unakatia ndani watu wadai 200
Pana wizi mkubwa sana pale...siku nikija Dsm ntanunua "ugomvi" pale
 
Hao ni mateja tu; Makonda atupie macho hapo.
siyo mateja ni wale wahudumu sijui wakata ushuru pale getini, yaani wanavyodai hizo pesa utafikiri ni za kwao.
kuna siku nilikuwa nasafirisha mzigo na nilikua nakimbizana na muda, nimefika pale nina 10000 tu nikawapatia wanasema nafanya kusudi hivyo nibakie nisubiri,
niligombana nao mnoo uzuri nilikua na jezi ya mule ndani nikatumia ubabe kuingia,

Pale panahitajika mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato,
na sijui ni kwa nini wanalipisha mtu kuingia katika kituo cha mabasi???.
 
Bado tu kuna watu wanafanya ufisadi pamoja na nguvu kubwa iliyopo kutokomeza hili janga nchini
 
siyo mateja ni wale wahudumu sijui wakata ushuru pale getini, yaani wanavyodai hizo pesa utafikiri ni za kwao.
kuna siku nilikuwa nasafirisha mzigo na nilikua nakimbizana na muda, nimefika pale nina 10000 tu nikawapatia wanasema nafanya kusudi hivyo nibakie nisubiri,
niligombana nao mnoo uzuri nilikua na jezi ya mule ndani nikatumia ubabe kuingia,

Pale panahitajika mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato,
na sijui ni kwa nini wanalipisha mtu kuingia katika kituo cha mabasi???.

Kwanini wanashindwa ku-digitize hayo mambo yote kama kule uwanja wa ndege ili kuwaondolea kero raia - isitoshe huwa wapo selective sana wanachagua watu wa kuwaharas
 
wajenge terminal ya ukweli waache ukanjanja huo na wapi kuingia terminal unalipia...hiyo imekaa kama garage au parking za maroli harafu mnaibia watu kisheria...
 
Leo nimelipa 200 kupanda Daraja la UDART kupitia Ubungo Bus Terminal. Vijana getini wamenizonga wakinilazimisha kulipa 200 kwa kuwa nimekanyaga Ubt. Eti watajuaje usafiri wa mikoani na wa UDART? Nikaenda tena kulipa 650 kwenda mjini. Jumla 850
Ni halali kulipa Geti la Ubungo ilihali sisafiri? Vijana mwenyewe Wa getini washari kweli.
Wapumbavu sana. Next shika hata kipande cha gazeti mkononi mkuu utapita kirahisi tu.
 
ukipandia upande wa depot ya tbl hakuna charge yeyote mkuu.
Sio kila mtu anatokea upande wa depot. Kumbuka lile daraja lilijengwa kuvusha watu. Sasa mimi sielewi wanashindiwa nini kukusanyia hizo 200 zao kule ndani ili kutenganisha anayeenda UBT na UDART. Jambo doooogo lkn lazima watu washikane mashati ndio kazi ifanyike.
 
hukuweza kupandia upande wa TBL depot?
Natokea Chuo kikuu, nikashuka kwenye foleni darajani. Hivyo ikabidi nitembee kupita hao vijana wasumbufu wanaokera abiria wa Mikoani. Upande huo kuna Daraja sikutaka kuvuka barabara hatarishi za mwendo kasi. Wanaolipisha ushuru kwenye mageti ya Vumbi walinizonga sana wakidai no way bila 200. Polisi wako mbali ningewaomba msaada.
 
Watoe receipt za machine ujinga wa hizi tozo za 200 ziishe hawasomeki na ubungo Yao Kama gofu la kale wanatoza pesa wapita njia hii Sio sawa
 
Pole sana. Nami imenikumba hiyo mi nilikuwa nakwenda kukata ticket ili nisafiri kesho yake. Jamaa wakusanya 200 wapo juu ya daraja la DART nilibishana nao,wakaniambia kama vipi nirudi nikapite upande wa depot ya TBL. Yaani niwasumbufu sana. Mh Mkuu wa Mkoa liangalie hili tafadhali.
 
Sio kila mtu anatokea upande wa depot. Kumbuka lile daraja lilijengwa kuvusha watu. Sasa mimi sielewi wanashindiwa nini kukusanyia hizo 200 zao kule ndani ili kutenganisha anayeenda UBT na UDART. Jambo doooogo lkn lazima watu washikane mashati ndio kazi ifanyike.
uko sahihi.
 
Back
Top Bottom