GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,652
- 14,247
nianze kwa kumshukuru mh rais kwa kunipatia nafasi hii ya kuwa hapa nilipo.maana bila yeye ningekuwa wapi mimi? namshukuru sana na kwa kweli anisaidie nidumu muda mrefu. rais huyu kama wale wengine waliopita pia ameletwa na mungu.kama si mungu unadhani atakuwa nani?kwa binadamu sisi hatuwezi.hatuwezi kabisa.usibishe ni mungu ndo aliamua kutuletea naye rais ni mpenzi wake mungu kabisa kama ambavyo mara nying husema"msema kweli ni mpenzi wa mungu" naamini kama ambavyo rais hupenda kusema kweli nasi anataka na atapenda tuseme ukweli daima, fitina kwetu iwe mwiko. (ahadi za mwana TANU zaman lakini si sasa )
mungu alitutizama watanzania akiwa huko aliko akatutizamaaaaaa... akaona hawa niwapelekee magufuli. basi akamleta nasi tunashukuru kwa kuwa tumempokea.tumempokea maana hatuna namna kama mungu ametuamulia hivi.basi tumempokea mh rais wetu dr mtukufu.
wanaosema maisha ni magumu hawa ni wachochezi na wavivu, si hivyo tu ila wana hatarisha kabisa usalama wa nchi. wanachochea njaa matumboni mwetu. na pia rais hapiki chakula watu waelewe hili. lakini ukiacha hayo chakula ni kingi sana. kila sehemu nikiangalia naona chakula kimepangwa kama ni chapati,maandazi,vitumbua,mihogo,wali,ugali n.k au nafaka kama mahindi,mchele,karanga,ngano n.k. halafu mtu anakuja kutuambia maisha ni magumu au kuna njaa...unataka rais akuchukulie hicho chakula huko unakokiona akupe? au utashangaa mwanaume na nguvu zake anaona vyakula hivyo nlivyotaja vipo sehemu mbalimbali lakini bado analalamika njaa. eti anataka rais akamchukulie ampe.
toka rais alipokuwa waziri alikuwa anayasoma matatizo ya watanzania.na aligundua kuwa tatizo kubwa sana la watanzania ni ukosefu wa ndege. yes. watanzania tulikuwa hatuna ndege.wenzetu wana Kenya Airways, Kuna Rwandair,Ethiopian Airlines n.k na kweli sisi maskini tulikuwa tunapata shida sana kusafirisha mazao yetu, tulipata shida sana kusafiri kuwahi shughuli za kilimo, tulilazimika kupanda garimoshi,meli na mabasi kutwa kucha tukihatarisha maisha yetu na kupata ajali. akaona isiwe shida. akaamua kutuletea bombadia. hapa nampa heko sana. kuna wapinzani hawalioni hilo kuwa ni mapinduzi makubwa sana.wapinzani wanapinga. hawataki kumwona twiga wetu akiwa amepanda ndege zetu. hawataki wanapinga tu.kule nyuma ya ndege kuna twiga.miaka ya nyuma watu walilalamika twiga wanasafirishwa nje.sasa twiga anaenda na kurudi sehemu mbalimbali za nchi na muda si mrefu mataifa mengine.
hapa kazi tu. hakuna kulalamika kazi tu na kazi ni kazi bora mkono uende kinywani.anasisitiza tufanye kazi.kila kazi inayowezekana tufanye.na anasema hata kufyatua tufyatue tu ile kazi yetu pendwa tufanye awamu yake hamna shida.tufyatue tu..tupige kazi wanaume tuache ulalamishi. kusema maisha magumu ni uchochezi wa kiwango cha PHD na wahusika wasiachwe hiv hivi.... sheria zifuate mkondo wake.wasiachwe kabisa.
maisha yamekuwa mazuri mtaani na wengi waliokuwa wanaringia vijikazi vyao wamerudi tupo nao mtaani wana buzi buzi tu.sasa watu wapo level. na sisi wenye tuvibarua tumenyooka kwa maboss hivi sasa tunawaheshimu na kazi tunaziheshimu sana. tuzidi kumwombea mh rais maombi chanya. na tumwombee pia azidi kutenda na kuwa alivyo mpaka mwisho. huko tunakoenda wengine hata namba watafikia kushindwa kusoma maana macho yao tayari yatakuwa yamepofuka. zidumu fikra za mwenye kiti. kidumu chama cha mapinduzi. tanzania mliianzisha mtaendelea kuwa nayo.
sasa ole wenu ninyi mnaochochea.